jamii ishakueleweni nyinyi ni watu wa aina Gani
Precise Pangolin Mayu deecharity watu watu, mnafanya kisebu sebu na kiroho kiko papo, mnaolalamika ni nyinyi watatu tu, sasa nataka serial number za decoder zenu zote mlizonunua kwangu pamoja na email address zenu, ili niwafute katika database yangu baada ya kuwapatia idadi ya hizo account, wateja wengine hawajalalamika wala hawajaongea kitu chechote, mnanita tapeli la kipemba ila bado mnataka huduma zangu, mimi nataka niwape hizo account zenu nivunje mkataba na nyinyi hata wa kupokea sms notification zangu. Sababu siwezi kuvumilia maneno yenu na sitaki kabisa kuendelea kuwapa huduma ya aina yeyote ile baada ya kuwalipa hizo account mnazodai. Napenda sana niendelee na wale wale ambao hawajapata kulalamika maana kila mmoja anazo namba zangu za simu na malalamiko yao huwa wanapiga simu (na sio jamii forums) na kama naweza kuyatatua basi nayatatua na yanapokuwa nje ya uwezo wangu huwa nawapa jibu kuwa hilo liko nje ya uwezo wangu. Naomba Jamii Isome hili kwa umakini.
Kuna wangapi humu wameharibu remote zao, gprs module boards na main boards na hivo ni vitu vyenye ghrama kubwa kununua na kusafirisha na huwa nawapa buree hizo spare parts bila ya malipo yeyote na hicho ni kitu ambacho hakipo katika makubaliano bali nawafanyia ubinaadamu, wangapi humu wanaharibu decoder zao nawaambia waniletee niwatengezee bila ya kuwalipisha chochote, wengine nawaambia kabisa lipia gharama ya kusafirisha China then ninatumiwa decoder mpya na naitoa China kwa Gharama zangu na nawapa bila gharama yeyote ile ya ziada. Seuze account kitu ambacho nakinunua nakutumiwa kwa email tu hakuna hata gharama ya kusafirisha. Naomba tusichafuane nipeni SERIAL NUMBER na EMAIL zenu niwape account na NIWATOE KATIKA LIST YANGU then nitawaruhusu muongee mtakavyo.
Account ni kitu kidogo sana kwangu kwa wale ambao wananijua personaly na ambao washawahi kukutana na mimi. Wako wengine watatoa ushahidi wa hilo na wengi ambao mpaka kesho wanipigia simu wanataka pdproxyy vouchers na huwa nawagaia bure kama nilivyokuwa nikiziweka voucher humu JF bure na premium accounts bure humu JF wengi tu wamenufaika kwa uwepo wangu.
Dah umejitetea hadi unatia huruma
Binafsi nakusamehe bure wewe na njunwa manyoko
Vitu vilivyonifanya kuwa mkali ni kauli zako na kunifanya nionekane tapeli
Tuache yaliopita tuongee ukweli tupu
Ahadi:
Ulituahidi acc za mwaka kwa G6
Ulituhakikishia G6 hazitakaa zije kubuma hata siku moja
Matokeo
acc zilikua za miezi 6 na si mwaka
ukaahidi utatoa bure unaleta sound tuuu
G6 hivi sasa zinaonyesha kama bahati nasibu tuchannel kiduchu full kuganda
Sisi wateja wa mwanzo mwanzo ulitudanganya sna mkuu na kutuaminisha ukiwa na ving'amuzi hivi umemaliza wakati ukweli ni kwamba ukiwa na hivi ujue kuona au kutokuona nikawaida,
Hii si kitu useme ununue eti special kwaajili ya world cup hapo utakuwa unadanganya mkuu maana inaweza kukaa mwezi mzima server down......u know that
Si wote watundu wa teknolojia wengine wetu ni watu wa plung and play
Hivi vitu vinataka watundu wa teknolojia lakini kama mwenzangu na mimi kamwe huwezi kupata unacho haidi
Hitimisho
Waambie watu ukweli kwamba hivi vitu vinakwenda kiwizi so anytime wenyewe wakiziba unahitaji muda kuzibua na ni asilimia chini ya 60 ya uhakika wa kuwa hewani chaneli zote
Pia sio bisara kuporomosha matusi kwa wateja wako ambao hawajaridhika hata kama wao wanatoa maneno ya maudhi binafsi nimetukana baada ya wewe kuanza kushusha matusi mazito
Hataka kama dini yako inakuruhisu lakini changanya na zakwako maana sidhani kama dini yako inaruhusu kutoa huduma unayotakiwa kuilipia kihalali lakini ina bypass
Nilisha uzaga hiyo g6 baada ya kutotimiza nilicho tarajia sina habari na aliyenunua anaendeleaje maana ni fundi madish
Ukiona wateja wako wanalalama jua mybe kunatatizo usipaniki deal nao taratibu, wapo wawili unasema ukinitoa mimi naomba watumie acc kwa pm imalize mzozo