Usikate tamaa bado mapema

NDORANGA

JF-Expert Member
Feb 6, 2021
216
371
Wasalaam,
-Kama ilivyo ada, leo nimeona ni vyema kuchangia hapa jamvini mawazo ambayo yatatupa moyo wa kusonga mbele, za pale tunapokutana na changamoto za kibiashara tukiwa Kama wajasiriamali.

-Unapokua mjasiriamali ni ngumu kukwepa changamoto za kibiashara zinazokuja mbele yako,hivyo basi ni vyema kupambana na changamoto za kibiashara ili uzidi kujengeka zaidi. Sasa basi unapokutana na changamoto zikakupelekea kuhusu kukata TAMAA,kamwe usisahau ;
1. Sababu iliyokufanya uanze Safari ya ujasiriamali.
2. Kutopunguza matarajio yako sawa na utendaji wako wa kazi,bali kuongeza utendaji wa kazi kuyafikia matarajio yako.
3. Kujifunza mbinu mpya kila iitwapo leo(binafsi napenda kujifunza kutokana na makosa yangu na ya wafanyabiashara wengine pia...) itakusaidia Sana kuweza kupambana na baadhi ya changamoto zijazo.
4. Furaha ya maisha haipo katika kutokuanguka bali kuinuka katika kila uangukapo, kusonga mbele kuelekea kwenye kutimiza zaidi.

-
 
Mniwie radhi wakuu,nimeandika nikiwa sijatulia,nawapenda Wana jf wote muwe na siku njema....by NDORANGA
 
Nikipata nafasi nitaeleza kinagaubaga jinsi jinsi nilivyopoteza mtaji kwenye kuku wa nyama (broilers).
 
Wasalaam,
-Kama ilivyo ada, leo nimeona ni vyema kuchangia hapa jamvini mawazo ambayo yatatupa moyo wa kusonga mbele, za pale tunapokutana na changamoto za kibiashara tukiwa Kama wajasiriamali.

-Unapokua mjasiriamali ni ngumu kukwepa changamoto za kibiashara zinazokuja mbele yako,hivyo basi ni vyema kupambana na changamoto za kibiashara ili uzidi kujengeka zaidi. Sasa basi unapokutana na changamoto zikakupelekea kuhusu kukata TAMAA,kamwe usisahau ;
1. Sababu iliyokufanya uanze Safari ya ujasiriamali.
2. Kutopunguza matarajio yako sawa na utendaji wako wa kazi,bali kuongeza utendaji wa kazi kuyafikia matarajio yako.
3. Kujifunza mbinu mpya kila iitwapo leo(binafsi napenda kujifunza kutokana na makosa yangu na ya wafanyabiashara wengine pia...) itakusaidia Sana kuweza kupambana na baadhi ya changamoto zijazo.
4. Furaha ya maisha haipo katika kutokuanguka bali kuinuka katika kila uangukapo, kusonga mbele kuelekea kwenye kutimiza zaidi.

-
God bless u
 
Mniwie radhi wakuu,nimeandika nikiwa sijatulia,nawapenda Wana jf wote muwe na siku njema....by NDORANGA
Awali ya yote asante kwa kutupenda.
Pili, nilitarajia umeandika your life experience bt naona uzi uko kimotivasheno sana anyway Barikiwa

Amani iwe nawe.
 
Back
Top Bottom