Waafrika: Tunaweza kutatua changamoto/matatizo makubwa kwa Akili zetu tusiogope kushindwa

article

Senior Member
Sep 10, 2016
176
331
Nchi za Afrika kwa muda mrefu zimekabiliwa na changamoto/matatizo makubwa ya kiuchumi,kisiasa,kiafya,kimazingira,kiteknologia na nyingine nyingi zisizosemeka huku zikiaminishwa kwamba hazina rasilimali Watu yenye uwezo wa kiakili wa kutosha kutatua changamoto hizi.Inasikitisha!

Utatuzi wa changamoto/matatizo haya makubwa kwenye nchi za kiafrika kwa kiasi kikubwa umekuwa si endelevu kutokana na fikra zilizojengwa na waliotutawala hapo awali kabla ya kupata uhuru kutujengea mazingira ya kuamini kwamba hatuwezi kutatua matatizo makubwa kwenye nchi zetu kwa kutumia akili zetu jambo ambalo halina ukweli ndani yake hata chembe.Tunaweza bila ya utegezi wa kiakili kwao.

Kuna Waafrika wenzangu ambao naamini wanaweza kubeza mtizamo na mwongozo jengefu na tatuzi wa uzi huu na kutolitilia maanani yaliyomo .Sitawashangaa wala kuwaona tofauti kwani wapo weusi wengi sana wenye fikra kama hizo ambazo kiuhalisia sio za kwao na hawapaswi kulaumiwa kwa hili bali ni wa kujengewa uwezo wa kujitambua na kuwakomboa na fikra potofu za wale wenye hila nasi Waafrika.


Waafrika tumeumbwa kupambana na kutatua changamoto kubwa hilo lipo wazi na wao wanalitambua kama utatupilia mbali joo la akili bandia ambalo Waafrika tumevikwa kwa muda mrefu na kuangalia uhalisia wa mambo tangu tulipojitambua kuwepo kwenye hii sayari.

Waafrika tumetatua changamoto nyingi kubwa ambazo hazisemwi kwa uwazi kwenye historia.Sitaki kurudi nyuma sana,Naomba nitoe mifano michache ya hivi karibu ambayo Waafrika kwa akili zetu tumeweza kutatua changamoto kubwa lakini bado Wakoloni wetu wa kizamani na wanaotaka kuja kisasa wakijaribu kwa kila namna na hila kuonyesha kwamba hakuna lolote linalohusisha akili kubwa ambalo tumelifanya.

Twendeni Rwanda tuone maajabu ya Mwafrika aliyoyafanya kwa kusonga mbele kwa kujiamini na mafanikio makubwa licha ya historia inayotisha ya changamoto kubwa za kisiasa,kiusalama na kiuchumi zilizotokana na hila kutoka nje ya bara letu.

Angalia Tanzania tulivyoweza kupambana na tishio la "Covid-19" ,hata hivyo bado kuna baadhi ya wenzetu ambao wameathirika kwa kiasi kikubwa na akili zisizo za kizawa wanaamini kwamba hatukuwa sahihi kwenye mapambano ya tishio hili kubwa kwenye historia ya majanga angamizi duniani wakati matokeo ya maamuzi yetu yapo wazi kwa Walimwengu wote bila kificho na rejea ya janga hili litadumu milele kutokana na uwepo wa "media" na vyombo vingine vya kisasa na kizamani vya kutunza kumbukumbu ambavyo vimeshiriki kutunza kumbukumbu hii muhimu.

Uwezo wa kutatua changamoto kubwa kwa akili yako kuna fursa kubwa ya kukufanya kuaminika na kupata fursa nyingi za kupewa majukumu ambayo yatakunuafaisha kwa namna moja au nyingine.Ndio maana Waliotutawala hapo awali wanaposikia changamoto yoyoye kubwa wao hujifanya ndio wana suluhisho hata kama siyo kweli kwa kuwa wanajua ukweli kwamba kwenye changamoto kubwa ndipo kwenye fursa kubwa ya kiuchumini na nyinginezo

Waafrica wenzangu tuachane na fikra rudisha nyuma za kukabidhi changamoto kubwa mikononi mwa watu wa mabara mengine kwani kwa kufanya hivi tunaamisha fursa kubwa kwenda kwao na sisi tukibakia watupu.

Tujifunze kuwa kushindwa ni sehemu kubwa ya kufanikisha, hivyo tusitishwe na hali hii kwani ukweli unoonyesha kwamba matatizo makubwa ambayo yametatuliwa hapa Duniani kwa kiasi kikubwa yalitanguliwa na majaribio mengi ya kushindwa yanayotia aibu , kufedhehesha na kukatiza tamaa.

Hivyo basi,Nawasii Waafrika Wenzangu kuacha mara moja kuamiashia matatizo makubwa kwa Wenzetu kutoka nje ya bara letu kwani kufanya hivi ni kuendeleza unyonyaji wa maliasili zetu na kujinyima fursa ya kuendelea kwenye nyanja zote.Badala yake Waafrika tujifunge mkanda na tutafute suluhu ya matatizo yetu makubwa sisi wenywe kwa njia ambazo kwa kutumia akili zetu halisi tunaamini ndio sahihi bila kusita au kutishwa na yeyote na hii ndio njia pekee ya kujitawala kwenye nyanja zote.


Naomba kuwasilisha,

Article.
 
Back
Top Bottom