Usikae sana kwenye njia ya foleni katika safari ya kuelekea mafanikio au utajiri, utachelewa!

Apr 19, 2018
83
112
NJIA YA FOLENI (POLE POLE NDIYO MWENDO)

Njia ya foleni ni njia ya wazee wa “polepole ndiyo mwendo”, wao huamini kuwa ili kuelekea mafanikio au umilionea inakulazimu kuwa na mvumilivu sana na mwenye subira. Watu hawa wana maarifa na wengi wao wamesoma sana, kiasi kwamba wanashindwa kujichunguza vizuri. Kuna wengine wanafikia hatua ya kujiona miungu watu, na hivyo akilini mwao siyo rahisi kujichunguza na kuona makosa wanayoyafanya kuelekea mafanikio.

Ukimuuliza mtu; “Hivi Profesa X wa chuo fulani Y, na Diamond nani ana mkwanja mrefu?”, wote tunajua jibu la swali hilo, yamkini hata mtoto wa darasa la kwanza atakujibu hivyo hivyo ulivyofikiria msomaji. Lakini sasa unaanza kujiuliza, kwa nini Profesa X katumia muda mwingi shule, katumia ada nyingi na juhudi nyingi kutafuta hiyo Elimu mpaka amefikia umri wa kuwa na kipara au Mvi, Lakini kazidiwa na mtoto mdogo kama huyo msanii?

MKANGANYIKO WA WATU WA NJIA YA FOLENI(CONFUSION)

Watu wa njia ya foleni wanashindwa kutofautisha kati ya Shule na Elimu. Hivi ni vitu viwili tofauti kabisa. Wao wanaamini kuwa kwenda shule ndiyo kuwa na elimu hasa hasa ya Maisha. Ndiyo maana wakirudi huku mtaani wanakuwa kama kuku wa kisasa, wakijivunia kikaratasi kinachoitwa Cheti”. Wengi wao wanafikiri hiyo karatasi ndiyo itakayofanya kazi ya kuwalisha, kuwanywesha na kuwavisha ndiyo maana kazi fulani fulani kwao ni hapana! “Hizo ni za watu wasio na elimiu” utawasikia.

Hivi hilo karatasi linaloitwa “Cheti” lingekuwa lina maana na nguvu hiyo tunayoiamini watu wa njia ya foleni, ingewezekanaje Bill gates, Tajiri wa tatu wa sasa duniani, kulikimbia karatasi hilo chuo?. Haya sawa! Tuachane na huyo, unamzungumziaje Mkwasi mwingine Steve Jobs, aliyewatengenezea hizo Iphone ambaye naye alilikimbia hilo karatasi chuo?. Ni wakati wa kugundua kuwa shule, siyo Elimu!

Inasikitisha sana unapowaona watu wa njia ya foleni, wamekaa kwenye hiyo foleni yao, kwenye mlango wa kampuni “Z” wameshika hayo makaratasi yao, wakisubiri mmoja baada ya mwingine kungia. Imani yao ni “Maisha ni foleni, taratibu yanasogea”.

Wakiisha kukubaliwa na kujiunga na kampuni “Z”, Mwendo wao ni ule ule wa “Foleni” na “Taratibu”, anasubiri baada ya miaka 10, ili apandishwe cheo na kuongezewa mshahara kidogokidogo au akiona vipi anarudi darasani, miaka mingine minne, anaongeza karatasi lingine na kurudi kwa mwenye “Z”; Ili mwenye kampuni “Z” amuongezee mshahara na kumpandisha cheo. Miaka 14 kwenye foleni ili uongezewe mshahara mara mbili au tatu au upandishwe cheo? serious?

HADITHI YA WATOTO WAWILI WA FARAO

Farao ana watoto wawili nyumbani kwake, mtoto wake wa kwanza anaitwa Juwa, ambaye ni mtoto wa kumzaa, lakini pia kuna mtoto mwingine anaitwa Chuwa, ambaye ni mtoto wa mdogo wake yaani mpwa, lakini kwa maamuzi ya Farao na kwa kumpenda mtoto huyo anampatia haki ya kuwa mwanae hivyo basi anastahili kuja kuwa mrithi wake pia.

Umri wa farao umeenda, kwa hiyo anaona ni wakati wa kumuandaa mtu atakayekikalia kiti chake cha enzi baada yake. Kwa sababu kwa maamzi yake Farao, watoto wote wawili Chuwa na Juwa wana haki ya kukikalia kiti hicho, Farao anaamua kuwapa mtihani, ili yule atakayefaulu ndiye atakaye kuwa mtawala halali wa nchi yake.

Farao anawaita Juwa na Chuwa na anawaambia hivi “Wakati wangu wa kuwaachia nchi umekaribia, hakuna mtu anayeishi milele, hivyo ni busara kwangu kumuandaa mmiliki atakayekalia kiti kile cha ufalme badala yangu. Hivyo basi wanangu, ninawapa kazi; na yule atakayekuwa wa kwanza kumaliza kazi hiyo ndiye atakayezawadiwa dhahabu na tunu na kisha kuvikwa taji ya ufalme.

Ninahitaji kila mmoja wenu anitengenezee Piramidi, kimo cha mikono 100, upana mikono 100 na urefu wa mikono 100. Lakini piramidi hiyo mtaijenga kwa masharti yafuatayo. Sharti la kwanza, kila mmoja wenu atajenga piramidi yake kwa mikono yake mwenyewe bila, usaidizi wa mtu mwingine yeyote. Sharti la pili; Ujenzi wa piramidi hiyo usizidi miaka 10, kwa siku zinazohesabika kuanzia leo hii, ninapowapatia kazi hiyo.....................................................................................INAENDELEA!
 
Mkuu kwako mafanikio ni kitu gani?

Huoni mafanikio ya sehemu moja yanaweza kuwa tofauti na sehemu nyingine?

Kama sio uvumilivu na subira Unafikiri diamond imemchukua miaka mingap mpaka kufikia kuwa na mafanikio aliyokuwa nayo sasa?
 
Mafanikio yana tafsiri pana sana. Wapo watu ambao mafanikio kwao ni pesa (nahisi hata kwako ni hivyo), wapo ambao kuwa na jina tu mtaani kwao, kwao ni mafanikio, wapo ambao wakifikia kiwango fulani cha elimu, kwao ni mafanikio, na wapo ambao kuwapa wahitaji kwao ni mafanikio. Halafu usiwakatishe tamaa wanaopenda elimu kwa kutoa mifano ya akina Bill Gate, eti waliacha shule (chuo) kwa kuwa waliona ni kupoteza muda, hiyo sio sahihi kabisa!

Bill Gate (na wenzake), hawakuacha chuo eti waliona elimu haina umuhimu, hapana. Hawa walikuwa na msingi mzuri kitaaluma wakati wanaingia chuo kikuu. Tayari walikuwa ma-programmer wakati wanaingia, hivyo walivyoingia wakakuta masomo waliyofuata (interest zao) tayari wanajuwa. Hivyo walipoona mahitaji yao yametimia, wakaona ni wakati muafaka wa kwenda mtaani kutumia maarifa yao. Hapa tusidanganyane kuwa walitoka kihasara, hapana, walitoka na mtaji wa maarifa. Hivyo basi nawashauri watu waende vyuoni wakapate maarifa na sio kuamini eti shule inapoteza muda. Narudia tena, tusikatishane tamaa.
 
Mkuu tuache siasa, unaamka asubuhi unawahi kazini, kama ni chombo chako cha usafiri unaweka mafuta (pesa inatumika), kama ni usafiri wa public ni nauli (pesa inatumika), Breakfast inafika, unaagiza (pesa inatumika), baadae lunch (pesa inatumika) halafu jioni dina (pesa inatumika), unarudi nyumbani kwa mafuta au nauli (pesa inatumika), kama unafamilia utawakuta watoto na mke wana mahitaji kedekede (pesa inatumika).
Sasa hivi umecomment, lakini ni baada ya kutumia bando (pesa imetumika)!
Mambo yote uliyoyayakinisha hapo juu, ni lipi ambalo halihusiki na kuzama mfukoni?
Na kama mambo yote hayo uliyoyaelezea yanagusa Pesa, huoni kuwa kutumia kigezo cha Shekeli, kujipima kimaendeleo kuna umuhimu mkubwa?
 
Mafanikio yana tafsiri pana sana. Wapo watu ambao mafanikio kwao ni pesa (nahisi hata kwako ni hivyo), wapo ambao kuwa na jina tu mtaani kwao, kwao ni mafanikio, wapo ambao wakifikia kiwango fulani cha elimu, kwao ni mafanikio, na wapo ambao kuwapa wahitaji kwao ni mafanikio. Halafu usiwakatishe tamaa wanaopenda elimu kwa kutoa mifano ya akina Bill Gate, eti waliacha shule (chuo) kwa kuwa waliona ni kupoteza muda, hiyo sio sahihi kabisa!

Bill Gate (na wenzake), hawakuacha chuo eti waliona elimu haina umuhimu, hapana. Hawa walikuwa na msingi mzuri kitaaluma wakati wanaingia chuo kikuu. Tayari walikuwa ma-programmer wakati wanaingia, hivyo walivyoingia wakakuta masomo waliyofuata (interest zao) tayari wanajuwa. Hivyo walipoona mahitaji yao yametimia, wakaona ni wakati muafaka wa kwenda mtaani kutumia maarifa yao. Hapa tusidanganyane kuwa walitoka kihasara, hapana, walitoka na mtaji wa maarifa. Hivyo basi nawashauri watu waende vyuoni wakapate maarifa na sio kuamini eti shule inapoteza muda. Narudia tena, tusikatishane tamaa.
Utakuwa unasoma d i g i r i i i ya tatu

Sio kwa ppvu hili aaseee
 
Back
Top Bottom