Usije ukadharau uwezo wa mtu kwa kigezo cha elimu aliyo nayo au ukaheshimu uwezo wa mtu kisa elimu kubwa

M2pc

Member
Jun 14, 2016
90
58
HIVI UNAJUA?

Na, Ikwataki Audax

Unajua, kuna wasomi wanawapuuzia watu ambao hawajasoma kama wao.. Yaani hawa wasomi hawataki kuwapa nafasi wenye elimu ya chini kushirikisha ideas, skills na knowledge waliyonayo kwa madai kwamba ni finyu isiyo na maana.

Lakini nakuhakikishia usije ukadharau uwezo wa mtu kwa kigezo cha elimu aliyonayo au ukaheshimu uwezo wa mtu kisa elimu kubwa. Maana kuna vitu ambavyo wakati wewe ukijipinda busy kusoma na kufanya kwa nadharia wenzio ambao hawajasoma kwa level yako walikua wanapitia kivitendo.

Na hawa ambao hawajasoma wakigundua unawadharau na kudharau ujuzi, maarifa na mawazo waliyonayo basi wanachofanya ni kukuridhisha kwa kusema ndio boss kwa kila kitu hata kama wanaona wazo lako litapeleka kampuni au biashara mtoni, wataitika tu ndio boss, sawa boss!!

Hivyo, kumbuka kila mtu ana maarifa, ujuzi au mawazo ambayo akiyashirikisha yanaweza kubuni, kuendeleza au kutoa huduma, bidhaa au suluhisho bila kujali kiwango cha elimu. Asante kwa kujua na kuelewa.

Na,
Ikwataki Audax
0765-090379
DAR ES SALAAM.
07.05.2018
 
Back
Top Bottom