Usijaribu kupiga picha za utupu

Usijaribu kupiga picha za utupu

koplo

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
574
Reaction score
153
Siku hizi umekuwa kama mtindo kwa wapenzi au hata mtu mmoja mmoja hasa mabinti kupenda kupiga picha za video au mnato wakionesha maeneo yao nyeti. Najua wengi wanaofanya mambo haya hawajui kuwa ni hatari sana kwani muda wowote picha hizo zinaweza kuingia katika mitandao ya kijamii au magazeti ya udaku. Ukweli ni kwamba picha ikiingia kwenye memory card yoyote hata kama utaifuta au ku format bado wataalamu wanaweza kuipata kwa kutumia special programs. Asije mtu akakwambia tupige halafu nazifuta hapa hapa kiukweli akiondoka anaenda kuzirudisha zote. Pia kuna risk za kupoteza ama kuibiwa cm .Pia wengine wana gawa memory card kwa jamaa au marafiki hivyo kupelekea siri kuvuja. USHAURI WANGU. Kama unataka mpenzi wako aone jinsi ulivyo umbika tafuta faragha umuoneshe kila eneo. Kama unataka wewe mwenyewe ujione tafuta kioo kikubwa ujiangalie kila eneo.ILA UPIGAJI WA PICHA ZA UTUPU NI HATARI
 
sasa kiwanini mpige picha za utupu wakati kila mtu anamuona mwenzie? yukiw ana hamu ya kumchungulia mwenzio si unamchunglia tu? hhhaaaa
 
Ni ukweli mtupu!!,asiyeamini ajaribu aone atakavyoumbuka

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
....waache wapige mpaka wanafanya maamuzi naamini wameshirikisha ubongo wao kufanya upuuzi huo,so let them face the consequence...
 
sasa kiwanini mpige picha za utupu wakati kila mtu anamuona mwenzie? yukiw ana hamu ya kumchungulia mwenzio si unamchunglia tu? hhhaaaa
Elli wengine hawapendi mwanga kwahiyo ni vigumu kuchungulia kote, inabidi umvizie umpige picha teh teh
 
Last edited by a moderator:
hahaaa haya mambo ya kupigana picha so ishu wala nini
mie enzi nasoma huyo dada alipigwa picha za utupu
na mpenziwe,siku ya siku wakagombana

yule kaka akampa option ampe 3Milion akishindwa picha zinaenda media
dada mwanafunzi 3M anazitolea wapi jamaa ni akazitoa zile picha za utupu
kwenye magazeti ya udaku............
 
Na unaanzaje kujipanga upigwe picha za hivi?....Na yawakute.
 
Some times wanaume huwa wanategesha laptop inakuwa inarekodi video bila wewe kujua. Ile window ya webcam inaiminimiz na kuacha window nyingine ikiwa top. We utajua hai record kumbe unarekodiwa . Au kamera inafichwa na nguo lensi tu inakuwa wazi, ki ukweli wasichana wengi wako kwenye risk ya kurekodiwa kwani eneola tukio boys ndio wanaandaa frequently
 
Back
Top Bottom