Usiipende rushwa hupofusha macho ya watu wenye akili

Samson Ernest

JF-Expert Member
Aug 28, 2014
404
651
‭‭Kum‬ ‭16:19‬ ‭SUV‬‬
[19] Usipotoe maamuzi; wala usipendelee uso wa mtu; wala usitwae rushwa; kwa kuwa rushwa hupofusha macho ya wenye akili, na kugeuza daawa ya wenye haki.

Agizo hili la kukatazwa kupokea rushwa walipewa maakida na waamuzi wa Israeli, waliagizwa wasipokee rushwa, maana rushwa ina tabia mbaya ya kuharibu viongozi, hawataweza kufanya yaliyo ya haki kwa wale wanaowaongoza.

Rushwa inapigwa marufuku sana hata siku za leo, hata kwa wana wa Mungu ambao wapo sehemu mbalimbali wana hatari ya kukumbwa na hili tatizo la kupokea rushwa, yapo mambo mengi yanayomshawishi mtu kutoa au kupokea rushwa.

Wale ambao Mungu amewapa nafasi ya kukalia viti mbalimbali katika nyanja tofauti tofauti, wamepewa angalizo hili mapema, kuepuka rushwa maana ni sumu mbaya sana inayoweza kuharibu maamuzi ya haki na kufanya udanganyifu au kumwonea asiye na hatia.

‭‭Mit‬ ‭29:4‬ ‭SUV‬‬
[4] Mfalme huithibitisha nchi kwa hukumu; Bali yeye apokeaye rushwa huipindua.

Ukitaka kuwa kiongozi mzuri epuka kuchukua rushwa, rushwa inaharibu mambo mengi na kuleta madhara kwa nchi au kanisa, ikiwa mna kiongozi ambaye anapenda rushwa, anaweza kuwaingiza kwenye eneo baya sana.

Tunaposikia rushwa tunaweza kuitazama kwa upande mmoja ila ukweli inaharibu mambo mengi sana katika maisha ya watu, wapo watu wanaweza kukosa haki zao kwa sababu ya rushwa.

‭‭Isa‬ ‭1:23‬ ‭SUV‬‬
[23] Wakuu wako ni waasi, na rafiki za wevi; kila mtu hupenda rushwa, hufuata malipo; hawampatii yatima haki yake, wala maneno ya mjane hayawawasilii.

Tusiwanyime wengine haki zao kwa kupindisha haki zao kwa sababu ya hali zao duni, wapo watu wamechukua mali za wengine, tusije tukapokea rushwa tukawapunja maskini haki zao.

Tusijiangalie sisi wenyewe, tujaribu kuvaa na viatu vya wengine, tunapochukua rushwa, tujue tumekuwa upande wa kuzulumu haki za wengine, vibaya kuzulumu haki ya mtu ambaye hakustahili kufanyiwa hivyo.

Tuwe makini sana, tusitangulize tamaa tukawaumiza wasiostahili kufanyiwa hayo, tutajichumia dhambi mbele za Mungu kwa kufanya mambo yasiyostahili mbele zake.

Karibu ujiunge na kundi la wasap la kusoma biblia kila siku na kutafakari, utapata fursa ya kuungana na wenzako wanaosoma biblia kila siku, wasiliana nasi kwa wasap +255759808081 ili uweze kuunganishwa kwenye kundi hili zuri.

Mwisho, nikukaribishe kwenye channel ya wasap kupata maarifa mbalimbali bonyeza link hii kujiunga=>>Samson Ernest

Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia yako
Mungu akubariki sana
Samson Ernest
+255759808081
 
Back
Top Bottom