Mimi ni mfwu tayari nina miaka 15 tu ya kupambana na humu nijenge nyumba, niweke akiba, na bado nifungue Bima.Usiogope pambana bila kuchoka
Miaka 60 ni mingi sana kibongo bongo......Nadhani ukifika 35 uwe ushajenga nyumba maana ukianza kusomesha ngumu sana kujenga ,kodi zinaumiza sana!Wengi wanapenda kuiongelea miaka 40 Ila Mimi nitakuwa tofauti kidogo
👇
KABLA HUJAfikisha MIAKA 60, HAKIKISHA UMEFANYA MAMBO HAYA 6:
1. Jenga nyumba yako.
Hata kama ni ya vyumba viwili, kuwa na makazi yako mwenyewe kunakupa utulivu, heshima na usalama wa maisha unapostaafu.
2. Weka akiba ya fedha.
Usisubiri upate kipato kikubwa ndipo uanze kuweka akiba. Hata kiasi kidogo unachoweka mara kwa mara kinaweza kuwa msaada mkubwa baadaye.
3. Kuwa na biashara au chanzo cha ziada cha kipato.
Usitegemee mshahara pekee. Biashara, kilimo au uwekezaji unaokuingizia kipato hata kidogo unaweza kukusaidia kuishi kwa utulivu.
4. Pata bima ya afya.
Afya ni mtaji wa maisha. Bima ya afya hukusaidia kupata matibabu kwa urahisi na kupunguza gharama kubwa zisizotarajiwa.
5. Wasomeshe watoto wako ikiwa umejaliwa kuwa nao.
Elimu ni urithi bora unaoweza kuwaachia watoto wako. Wape nafasi ya kujifunza na kufikia ndoto zao.
6. Weka malengo na ishi kwa amani na watu.
Kuwa na malengo yanayokuongoza maishani, fanya kazi kwa bidii, na jenga mahusiano mazuri na watu. Heshima, upendo na mshikamano ni sehemu muhimu ya maisha yenye mafanikio.
Maisha ni safari ya maandalizi. Anza leo kujenga kesho yako, kwa sababu kila hatua ndogo unayochukua leo inaweza kuleta tofauti kubwa baadaye.
40 unaishi kwa shemeji 😁, wewe husaidiki tena, rudi kwa baba ukaishi kabla hajauza nyumba ya familiaKwa hiyo mimi mwenye miaka 40 ninayeishi kwa shemeji unanishauri nianzie wapi?
Haya ngoja kesho nikachukue torori nianze kutembeza maji mtaaniMe mwenyewe Nina 40+ sielewi as long as upo timamu na unajua muda umeenda you can do something we live at the present.
Mzee ataniuwa japo ana miaka 60 ila bado ananguvu za kunifukuza40 unaishi kwa shemeji 😁, wewe husaidiki tena, rudi kwa baba ukaishi kabla hajauza nyumba ya familia
Endelea kuishi kwa shem ...muda badoKwa hiyo mimi mwenye miaka 40 ninayeishi kwa shemeji unanishauri nianzie wapi?
Au sio ili nije kukumbuka shuka uzeeni?Endelea kuishi kwa shem ...muda bado
Yeah Man sio kila mtu ata_achieve wengine wapo kusaidia wengine kuachieve.Maisha yana full of surprises, kuna wanaoweza kuachieve vyote ulivyosema lakini kwa wengine ni kizungumkuti, kila mtu na fungu lake
Upo sahihi, nakubaliana na wewe Lakini si unajua bongo nyoso? Sasa ushafika 40+ Lakini bilabila😁 ufanyeje ujinyongee???Miaka 60 ni mingi sana kibongo bongo......Nadhani ukifika 35 uwe ushajenga nyumba maana ukianza kusomesha ngumu sana kujenga ,kodi zinaumiza sana!