Nakadori
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 8,779
- 21,053
Nimelelewa katika familia ya kumcha Mungu. Sijawahi kumuona baba, mama, bibi, babu, au mjomba akienda kwa mganga. Ila dunia ilinifikisha na kunifundisha kwenda kwa mganga.
Katika kukabiliana na matatizo ya dunia aliyoniusia mama kwamba "Naka kua uyaone ya dunia" nilijikuta nimekabiliwa na tatizo la kimapenzi ambalo lilinikondesha kwa siku 3 kila nipitapo watu walikuwa wananishangaa. mama yangu alilia sana asijue ni kipi kilinisibu ila kamwe sikufungua mdomo kuelezea nini tatizo. Nilisugua kichwa bila jibu.
Asubuhi ,moja shetani akanipa wazo la kwenda bagamoyo kutafuta mganga (ilitokana na maelezo ya watu kuhusu uganga na bagamoyo) .Sikujua hata ni wapi kuna mganga ila nilielekea mwenge kupanda gari nisijue hata nitashukia wapi. Nikapata wazo la kumuuliza conductor kama anajua mganga yeyote huko bagamoyo. Alisema nisiwe na tabu.
Tulifika bagamoyo akanielekeza kwenye mganga. niliefika nikaambiwa nianda 40,000 kwa ajili ya vifaa kama nazi, kuku ubani, kitambaa cheupe, n.k. nilishuhudia nazi zikivunjwa na kuokotwa kwa ajili ya kitoweo.
Kuku alichinjwa bila kuchelewa mke wa mganga akaja kumchukua huku akiita watoto wachemshe maji tayari kwa kunyonyonyolewa. Wakati wa kuondoka nilipewa dawa inaitwa mlipu na maandishi ya kiarabu eti nikachome nikiwa naongea yale nitakayo.
Nilirudi mtaani badala ya tatizo kupungua ndio lilizidi mara 20 zaidi. Nikakata tamaa, ikabidi nimpigie tena yule kondakta (nilichukua namba yake). Alinielekeza mganga mwingine karibu na kawe beach. Mambo yakawa ni yale yale mwisho nikaagizwa mwingine wa kunduchi ambae na makalio huwa anashika (wengine hadi wameliwa papuchi) yakawa ni yale yale.
Katika mishe nilipatamarafiki wenye matatizo mbali mbali team ikaundwa . Tulipata twende kunduchi beach yupo mganga mwingine ila mafanikio yalikuwa ni sifuri.
Kote huko hela zinaliwa tena hadi laki 2 kwa mganga mmoja.
Safari ya mwisho ilikuwa ya tandika ambapo nilijiambia nisipofanikiwa bhaaaaaasss. Huko nilikutana na waganga 2 mwanamke na mwanaume dawa walizotoa ni zile zile ila waliongezea nipeleke nywele za mhusika, nguo/uzi wa nguo yake, na mabaki ya chakula kwenye sahani aliyokula. Pia nilkipewa maji ya kumuwekea kwenye chakula na mengine niweke kwenye maji yangu ya kuoga. Mafanikio hayakuwepo pia.
Mwisho nilijuta sana na kumrudia Mungu kwani niligundua uganga ni utapeli. Toka nilipoamua kumrudia Mungu nilipata amani ya kweli na afya yangu ilirudi. Niliamua kupotezea lile tatizo na nililikubali.
Ni kipi ninataka kuwausia:
1. Waganga wengi ni wezi na waganga njaa hivyo kwenda kwao ni kutafuta kuibiwa
2. Asilimia kubwa dawa ni zile zile hivyo kupita kuzunguka ni kujichosha.
3. Nilikutana na wachaga na watu mbali mbali. shida ya mchaga ilikuwa kuvuta wateja , kupata hela ila wenzangu na mimi tulipelekwa na ishu za mapenzi. angalau mchaga alienda kimaendeleo
4. Wanawake wengi huenda kwa waganga tatizo kubwa likiwa mapenzi. kote nilikopita 99% ya wateja ni wanake tatizo kubwa mapenzi. wenye sura nzuri shepu na walio kawaida. hili ni fundisho kwamba shida ya mapenzi ni kwa wote mapenzi hayana ufundi wala mwenyewe. kama unaoa muombe Mungu sana.
5. Hakuna jipya chini ya jua. ni ubatili na kulilisha upepo. nimemrudia Mungu ni baraka kwa kwenda mbele na amani ya kweli
6. Waganga wengi wa darisalam wana bei kuliko mikoani hii ni kwamba dar kuna hela ndefu ni kama bei za nyumba dar zilivyo juu kuliko mikoani.
7. Never say never. kabla hujafa lolote linaweza kukufika na ukajikuta unafanya usilotegemea.
Mwisho usidanganywe ni wizi mtupu.
Mungu anatosha