Usichukulie poa suala la uchumba, itakugharimu

Usichukulie poa suala la uchumba, itakugharimu

Mpaka hapa mleta uzi umefeli kwenye tasnia ya kupenda.
Upendo halisi ni pale unapompenda mtu kutokana na mapungufu yake.

Pili haya mambo ya kuchunguzana yalikuwa ya zamani sio leo.

Tuchukulie leo, unakuta wachumba wanatoa nchi tofauti. Familia Nazi ziko nchi tofauti; hivvi hapo utaweza kufanya uchunguzi kweli?
Kwahiyo ni mwendo wa kuoa tu, hakuna hata kumchunguza mwenza wako?
Hapo ndo baadhi ya watu wanaoa hadi jamii inaanza kushangaa kua imekuajekuaje.
All in all hiyo ndo demokrasia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahiyo ni mwendo wa kuoa tu, hakuna hata kumchunguza mwenza wako?
Hapo ndo baadhi ya watu wanaoa hadi jamii inaanza kushangaa kua imekuajekuaje.
All in all hiyo ndo demokrasia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukisoma vizuri mleta maada amelenga mda wa kuchunguza uwe mrefu, kwa kifupi amemaanisha miezi sita haitoshi.

Kwa kifupi point yangu ni kwamba kumchunguza mchumba sio lazima uwajue ndugu zake na familia kwa ujumla na si lazima utumie miezi 6+. Unaweza kutumia miezi 2. Na ukiwa smart unafanya maamuzi hata baada ya wiki
 
Nikweli Mkuu Ila watu hubadilika nakua wanaofaaa bila kujalisha tabia za ukooo.


So hapa Point iwe, kama ni mwema naunaona anafaa, basi Oa ,mengine yalobaki unawaachia ndugu zao.
 
Usidanganyike...sijasema kuna koo au familia perfect. Kuna familia zina tabia mbaya za kurithi zisizovumilika.

Ukiingia kwenye koo kama hizi, maisha yako mafupi yatakuwa na majuto.

Hakuna perfect...ila kuna watu wanaostrive kuwa perfect...vitu vidogo. vidogo ni vya kuvumilia tu!!!

Sent using Jamii Forums mobile app

Unakuta kuna ukoo ubakaji wa watoto ni normal

Ndugu hawaeleki
 
Hamjambo humu ndani, wakubwa zangu shikamooni, wadogo zangu marahaba.

Bila kupoteza wakati, ngoja nitiririke neno la usiku wa leo.

Katika haya maisha, kila kitu kina hatua zake. Mfano, unaingiza gia kwenye pikipiki kabla ya kushika krachi, unategemea nini?

Vijana wengi wa leo tunavunja ndoa zetu kwa sababu ya kuruka hatua muhimu ya uchumba. How comes, mtu umefahamiana nae miezi sita, unaamua kuishi nae kama mke au Mme?

Uchumba upo mahususi kwa ajili ya kufatilia historia ya binti au mvulana unayetaka kuingia nae katika ndoa. Uchumba sio kutambulishana tu na kwenda beach kujimwangia mchanga. Uchumba ni kipindi muhimu cha kuchunguzana.

Ukiona tabia zake huwezi zivumilia a hana nae. Fatilia familia yao ikoje. Kumbuka kuna koo au familia zina laana. Yaani unakuta ukoo wote, familia zimeyumba, mara mdgo mtu katembea na mke wa kaka. Mara mabinti wa ile familia wamepigwa mimba wote na hawaolewi.

Naomba uweke akilini kuwa: tabia urithishwa kutoka kizazi hadi kizani. Tumia kipindi cha uchumba vizuri...hicho sio kipindi cha kulana. Ni kipindi mahususi kwa ajili ya kujua A, B, C, za unayemtarajia.

Ile misemo ya kipumbavu ya " Ukitaka kumla bata, usimchunguze" itatugharimu sana vijana.

"MKUMBUKENI MKE WA STAMINA"



Sent using Jamii Forums mobile app

Tatizo tuliochunguza wanawake tumejikuta tunatengeneza tu single mothers,tukaamua tuje na kauli ya kujilipua


Sent using IPhone X
 
Ukisoma vizuri mleta maada amelenga mda wa kuchunguza uwe mrefu, kwa kifupi amemaanisha miezi sita haitoshi.

Kwa kifupi point yangu ni kwamba kumchunguza mchumba sio lazima uwajue ndugu zake na familia kwa ujumla na si lazima utumie miezi 6+. Unaweza kutumia miezi 2. Na ukiwa smart unafanya maamuzi hata baada ya wiki
Kuwajua ndugu au familia ni msingi Sana.
Vipi kama familia ni wezi, wanao wakienda ujombani watafundisha tabia.
Vijana acheni ubishi.
 
Kuwajua ndugu au familia ni msingi Sana.
Vipi kama familia ni wezi, wanao wakienda ujombani watafundisha tabia.
Vijana acheni ubishi.
Kumbe watoto wako unatunziwa na shemeji zako? Ili mtoto aige tabia ni mpaka ajae na mtu. Acheni ushamba wa kizamani. Na haoa hatujaongelea kuwafahamu familia Bali tunazungumzia mda wa kutumia kuwafahamu.

Kitu nitakuambia ukiwa na mchumba ukafunguka ukamwambia kila kitu kuhusu familia yako, hakika atafunguka kila kitu kuhusu familia yake. Hivyo basi uhitaji zaidi ya miezi 6 kumfahamu mchumba na familia yake.
Si ajabu wewe unaeniita kijana nakuzidi umri.
Acha kukariri babu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom