Usichukulie poa suala la uchumba, itakugharimu

Nebuchadinezzer

JF-Expert Member
Oct 1, 2018
1,403
2,545
Hamjambo humu ndani, wakubwa zangu shikamooni, wadogo zangu marahaba.

Bila kupoteza wakati, ngoja nitiririke neno la usiku wa leo.

Katika haya maisha, kila kitu kina hatua zake. Mfano, unaingiza gia kwenye pikipiki kabla ya kushika krachi, unategemea nini?

Vijana wengi wa leo tunavunja ndoa zetu kwa sababu ya kuruka hatua muhimu ya uchumba. How comes, mtu umefahamiana nae miezi sita, unaamua kuishi nae kama mke au Mme?

Uchumba upo mahususi kwa ajili ya kufatilia historia ya binti au mvulana unayetaka kuingia nae katika ndoa. Uchumba sio kutambulishana tu na kwenda beach kujimwangia mchanga. Uchumba ni kipindi muhimu cha kuchunguzana.

Ukiona tabia zake huwezi zivumilia a hana nae. Fatilia familia yao ikoje. Kumbuka kuna koo au familia zina laana. Yaani unakuta ukoo wote, familia zimeyumba, mara mdgo mtu katembea na mke wa kaka. Mara mabinti wa ile familia wamepigwa mimba wote na hawaolewi.

Naomba uweke akilini kuwa: tabia urithishwa kutoka kizazi hadi kizani. Tumia kipindi cha uchumba vizuri...hicho sio kipindi cha kulana. Ni kipindi mahususi kwa ajili ya kujua A, B, C, za unayemtarajia.

Ile misemo ya kipumbavu ya " Ukitaka kumla bata, usimchunguze" itatugharimu sana vijana.

"MKUMBUKENI MKE WA STAMINA"



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukitaka kupata mchumba anayetoka kwenye perfect family utamaliza dunia nzima usimpate.
Kila familia ina vinegativities vyake
Hakuna ukoo ulio 100% perfect.
Kikubwa mchunguze mwenza wako kama anafaa kuwa mke/mume oa.
Usimhukumu kwa uzinzi/ ulevi wa ndugu zake
 
Ukitaka kupata mchumba anayetoka kwenye perfect family utamaliza dunia nzima usimpate.
Kila familia ina vinegativities vyake
Hakuna ukoo ilio 100% perfect.
Kikubwa mchunguze mwenza wako kama anafaa kuwa mke/mume oa.
Usimhukumu kwa uzinzi/ ulevi wa ndugu zake
Usidanganyike...sijasema kuna koo au familia perfect. Kuna familia zina tabia mbaya za kurithi zisizovumilika.

Ukiingia kwenye koo kama hizi, maisha yako mafupi yatakuwa na majuto.

Hakuna perfect...ila kuna watu wanaostrive kuwa perfect...vitu vidogo. vidogo ni vya kuvumilia tu!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
you are NOT 100% perfect lakini unategemea mwenzako awe hivyo...tafuta ambaye hana kasoro kama hujazunguka dunia nzima kutafuta mchumba...
Sitafuti aliye perfect ila natafuta ambae tunaweza bebeana madhaifu madogo madogo yanayovymilika.

Sio kila mwenye K anafaa kuwa mke au mweny MB anafaha kuwa Mme.
I'm done!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom