Usiamini mtu yeyote, imenitokea soma itakusaidia

Usiamini mtu yeyote, imenitokea soma itakusaidia

kaka inamaana shule ya msingi ulisoma kwa miaka mitano!!?? 1996-2001... Ila nikupe pole huyo ukimtaka unampata kirahisi tu mchukulie RB kwanza halafu fuata ushauri wa wadau waliouweka humu Einstein
mkuu unashangaa jamaa kusoma miaka mitano shule ya msingi cheki kwanza id yake ndo utajua
 
Last edited by a moderator:
mkuu unashangaa jamaa kusoma miaka mitano shule ya msingi cheki kwanza id yake ndo utajua

the genius..alirushwa madarasa sio..sasa kama ndio hivyo hata mwizi wetu nae ni genius maana naye atakuwa alipandishwa madarasa..ila akafeli maisha
 
Mkuu hata mimi yamenikuta nilikutana na Rafiki yangu wa utotoni ambaye tulisoma primary pamoja na tuliishi majirani baadae wazazi wake walihama sababu pale mtaani kwetu walikuwa wamepanga hivyo walivyojenga wakahama.hivyo hata na shule alihama.sasa nikakutana naye muhimbili mwezi june akanipeleka ofisini kwake maana yeye ameajiriwa kama procurement officer pale muhimbili.tukapeana contact na wikend moja akanikaribisha nikaione familia yake.kiufupi urafiki ukarudi tena.sasa sikukuu ya IDD nakumbuka tarehe 29 July akanipigia Simu nimuazime 50000 sababu mshahara wa july haujatoka.kwa kuzingatia yeye na familia yake ni waislamu ile IDD inawahusu nikamtumia kwa tigopesa.basi mpaka tarehe 10 august kimya nikampigia anasema bado tarehe 15 nikampigia akasema atatuma yupo tight nikajua mshahara tayari atatuma.basi tokea aseme hivyo hajawahi kutuma na hata calls na SMS halerespond.nimepanga siku nikamuabishe ofisini kwake na urafiki ufe

Mkuu huyo muache tuu Mimi marafiki wasio waaminifu huwa nawapa mitego kama hiyo asiporudisha ushkaji utakuwepo ila msaada big NO
 
Aiisee, Pole sana mkuu. Wageni ambao hawasomeki wanapokua home ni kua nao makini sana.
Mtu akishakua na haraka haraka tu anatia shaka katika mambo yake ilihali ratiba nzima ya mipango yake anaijua!
 
Mbona unamchelewesha huyo? Kachukue RB fasta. Mtafute umpeleke polisi. Hiyo simu mbona atarudisha. Hata kama kauza utaipata tu. Tafuta polisi unayemjua au tafuta connection ya polisi. Utaipata tu. Ukiwa mpole hivyo huipati.
Ilikuwa ijumaa majira ya saa mbili jioni, nilipokea simu ya rafiki yangu wa karibu akanambia yuko Mlimani City akanambia anahitaji kuonana na mimi maana kesho yake alikua ana "interview" kwa hiyo alitaka kupata uzoefu wangu wa "interview". Nilikuwa nimechoka, ila sikusita, nikamkubalia aje ili niweze ongea nae mawili matatu.

Huyu jamaa alikuwa rafiki yangu wa karibu sana nimesoma nae shule ya msingi, 1996 mpaka 2001. Alikuwa ni kati ya marafiki tuliosaidiana sana katika masomo yetu ya shule ya msingi.

Basi, kwa sababu ya kuamini kuwa ni mtu makini, nilimkaribisha nyumbani, nikamwandalia msosi, tukala na baadae tukapata muda wa kuzungumza mawili matatu.

Ukafika muda wa kulala, tukaenda tukajipumzisha, ingawa ye alibaki kidogo sebuleni kuangalia TV na baada ya kama dakika 40 hivi nae akaja kulala.

Tumelala mpaka ilipofika mishale ya asubuhi, mie nikaamka kwenye saa moja hivi, nikawa napiga stori na mdogo wangu niliekuwa nae pembeni yangu. Ye huyo rafiki yangu alikuwa bado amelala, ingawa alikuwa anajigeuza geuza, nikidhani bado yuko kwenye usingizi.

Baada ya kuwa amejigueza geuza hivyo, kidogo tu akainuka, akaenda washroom kidogo, baadae akaaga hapo hapo.

Nikamwuliza mbona unaaga mapema sana, kwanini usisubiri tunywe chai ndo uende. Akasema hapana anawahi Mbezi kwenye interview kwa hiyo kama vipi atarudi baadae ili aje kunywa chai wakati akiwa njiani kurudi kwake Magomeni(alidai anaishi huko). Akanambia nimsaidie nauli kidogo. Nikarudi chumbani nikachukue vijisenti kidogo nikampatia. Tukaagana.

Mishale ya saa tatu kasoro hivi nikawa nahitaji kuingia kwenye internet kupitia simu yangu. Mara nyingi simu huiacha kwenye chaji, chini ya kitanda, kwenye kapeti.

Nilipoangalia pale sikuiona simu, nikiipiga haipatikani wakati nimeiacha kwenye chaji na ilikuwa ON. Simu yangu ilikuwa aina ya SAMSUNG GALAXY NOTE II, ambayo gharama yake ni kati ya laki sita na saba.

Basi nikatatufa weee nikawa siioni. Lakini nkajiuliza inakuaje kitu kipotee, tena ndani, na wakati nimekiacha kwenye chaji wakati nalala, halafu simu yenyewe ni kubwa, kwa hiyo ni rahisi kuiona, halafu mbaya zaidi haipatikani. Basi nikajua hii simu imeibiwa. Na mtu wa kwanza kumhisi ni huyo rafiki angu tulielala nae.

Nikaona nikimpigia moja kwa moja inawezekana namwonea. Nilichofanya, ikabidi nianze kuulizia tabia yake. Dah! Kumbe rafiki yangu alishabadilika siku nyingi amekuwa tapeli mkubwa. Katapeli watu kibao. Kila mtu akawa ananishangaa kwanini nakaribisha nyumbani mtu kama huyo. Nikasikitika sana, nikajua moja kwa moja ni yeye ndie aliechukua simu.

Nikampigia simu nikimwambia arudishe simu yangu. Akakataa kwamba hajachukua simu, na akasema, yaani yeye kufika kwangu siku hiyo inakuwa tabu mpaka naanza kumsingizia kaiba. Nikamwambia basi njoo nyumbani angalau tusaidiane kuitafuta maana tumelala wote. Akanikatia simu, nikawa nampigia hapokei, wala SMS hajibu. Nikasikitika sana.

Nikawa najiuliza nitaipataje hii simu yangu nzuri niliyokua naipenda, na bora simu unaweza nunua tena, ila kulikuwa na documents (nyaraka) muhimu niliziweka kwenye simu ile, na zilikuwa na assignment na projects zangu. Nitaipataje.

Basi, siku nzima ya jumamosi na jumapili nilijitahidi kuwasiliana nae bila mafanikio. Ingawa siku ya jumamosi usiku aliniahidi atakuja nyumbani baada ya kushauriwa na moja ya rafiki yangu wa shule ya msingi, lakini sikumwona kufika.

Jumatatu majira ya saa tano akanipigia simu, nilikuwa ndani ya training ya kiofisi, akanambia kuwa, simu yangu kaiweka bond (sidhani kama ilikuwa kweli) ya TSh elfu arobaini, kwa hiyo akataka nimrushie elfu arobaini ili aikomboe simu yangu ndo aniletee, na akanitishia kuwa, nikichelewa hiyo simu sitaiona tena.

Nikajiuliza, simu ni yangu, kaiiba, halafu kaiweka bond (naamini bond ni uongo), halafu nimrushie pesa akakomboe simu yangu? Duh! Kweli ujinga mzigo.

Ila kwa sababu niliihitaji sana hiyo simu, nikamwuliza, "Uko wapi??" akanambia, "Niko Africana.." .. Nikamwambia, hapo Africana, kuna tawi la ofisi yetu, kwa hiyo nenda pale ofisini, nitawaelekeza wafanyakazi wa hapo wakupe elfu arobaini na uwaachie simu yangu.

Akanambia, "Aiseee!! Mie naona unazingua, huyu jamaa(jamaa wa bond) nikimwacha hapa sitamwona tena, kwa hiyo inabidi urushe tigopesa fasta ili niikomboe simu (uongo)"..


Basi nikamwambia,
"Nielekeze mlipo ili nimtume mtu aje hapo akupe hela na achukue simu"..
Akanambia, "Huyu jamaa hataki mtu yeyote aje hapa..."
Nikamwambia, "Basi nipe namba ake nimpigie ili asiondoke na simu yangu"
Akanambia, "Hapana we tuma tu hela, halafu naona unazingua simu unaweza usiione tena.."
Nikamwambia, "Basi mie nakuja huko Africana ili kulishughulikia hilo swala"
Nikatoroka training nikaenda mpaka Africana, nilipofika, nikampigia simu ili aje anipe simu yangu. Kumpigia akanambia, "Tuma kwenye tigopesa yangu"..
Nikamwambia,"Sasa kama ntakutumia kwenye tigopesa hiyo simu naipataje (kupitia tigopesa)? "..
Akanambia, "J ... mie naona unazingua, mie nakwambia tuma kwenye tigopesa we unachelewa, hii simu utakua hauipati tena"..

Nikamwambia, "Hivi nimekukosea nini mpaka unanifanyia unyama wa aina hii, simu yangu halafu initese kiasi hiki??"..
Basi akanikatia simu.

Nikaenda mahali, nikakaa, nikawa nampigia hapatikani.. Ilinichukua kama masaa mawili hivi nikiwa nimekaa kwenye ki restaurant flani maeneo ya africana, nikijifariji na lunch kidogo, huku nikisubiri nikiamini huenda tukaonana nikachukua simu yangu.

Baadae nikajaribu kumpigia akawa anapatikana nikamwambia, nimekusubiri sana bila mafanikio. Nikaamua kurudi zangu home, na mpaka dakika hii sijaipata simu yangu.

CHA KUJIFUNZA.
Usiamini mtu yeyote, hata kama ni rafiki yako. Hakikisha unamjua vizuri kabla ya kumkaribisha nyumbani kwako. Ameniudhi sana, maana ni mtu ambae nimekua nae, tumezaliwa wote sehemu moja, tumekua wote, tumesoma wote, tulikua tukisaidiana enzi hizo halafu anakuja kuwa mtu wa kuniibia, kunipotezea documents zangu za mhimu ambazo ni za mhimu sana kwenye kazi zangu.

Kiukweli nimemchukia sana na itanichukua muda kumsamehe na kumsahau. Ipo siku tutakutana tu, na sheria lazima ichukue mkondo wake.
 
Roho inauma as if nimefanyiwa mimi huyo ukimtia mikononi mle kwanza kboga na condom lkn kisha tandika sanaa nyofoa meno yake mawili mkate kidole cha mwisho mguu wa kushoto alaf mwisho kabisa mpe tindikali achambie wrxcghjcfuonvxdje zake huyo

hahaaaaa...
!
 
pole ila matapeli huwa wanaboa sana, mimi nilitapeliwa na mama mtu mzima niliekuwa namuheshimu kumbe hana maana , aliniingilia kwa gia yakukopa nikamkopesha laki3 eti baada ya siku 2 ataniletea mara zikawa 2wks mara mwezi nikimpigia blabla za uongo kibao, kumfuatilia kwa watu wakaribu nikaambiwa ni tapeli wakimataifa nimechemsha sana kumpa hela dah nikatulia nitungesheria nimfanyeje maana kwenye cmu alikuwa anijibu atakavyo akijua sinapakumpata kumbe mimi nampeleleza nikajua anapofanya kazi, nilimtokea kazi kwake kichwa kikiwa bangee mentally bahati yake sikumkumkuta kaenda kazi za nje ila staff wenzie walimpigia wakati mwambia timbwili nililoliacha, nikiwa narudi ofisini kwangu mara cmu yake kawa mpoleeee ananiambia dear uko wapi nikupe ile hela yako nikamwamrisha nikukute ofisini kwangu ndio akanipa baada yakujua nimeshajua pakumpata.. kwahiyo huyo jamaa jifanye umemptezea huku unaendelea kumspy siku isiyo najina anashangaa unamvamia Kama jeshi nalazima aisome
 
kwanini uciitafute simu yko kwa njia ya mtandao kuna application kama ant lost cjui zlikuwepo kweny cmu yako?
 
Back
Top Bottom