Usiamini mtu yeyote, imenitokea soma itakusaidia

Usiamini mtu yeyote, imenitokea soma itakusaidia

Mkuu Einstein pole sana. Ila imeniuma sana. Kama uko willing, naomba unipe kazi ya KUKUKAMATIA huyu mtu. Mkuu mii nisaidie RB number, namba yake ya simu, na elfu 20 tu! Ntakuambia mahali pa kuja kumchukua mtu wako!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Einstein pole sana. Ila imeniuma sana. Kama uko willing, naomba unipe kazi ya KUKUKAMATIA huyu mtu. Mkuu mii nisaidie RB number, namba yake ya simu, na elfu 20 tu! Ntakuambia mahali pa kuja kumchukua mtu wako!

Mkuu unatisha.nikiwa na shida kama hiyo nitakutafuta
 
Last edited by a moderator:
Pole sana kwa kuibiwa!! Ila kabla hujafikia hitimisho la kutoamini mtu tafakari kwanza! Katika maisha ili kazi, biashara nk viendelee tunahitaji kushirikiana na watu. Huwezi kushirikiana na mtu/watu pasipo kuwaamini! Cha msingi ni kuwa makini katika hatua za kumuamini mtu kwa 100%. Imani hujenga imani.....!!! anza kwa kumuamini mtu kwenye vitu/mambo madogo kabla hujamuamini kwenye vitu/mambo makubwa!!
 
Ilikua ijumaa majira ya saa mbili jioni, nilipokea simu ya rafiki yangu wa karibu akanambia yuko Mlimani City akanambia anahitaji kuonana na mimi maana kesho yake alikua ana "interview" kwa hiyo alitaka kupata uzoefu wangu wa "interview". Nilikua nimechoka, ila sikusita, nikamkubalia aje ili niweze ongea nae mawili matatu.


Huyu jamaa alikua rafiki angu wa karibu sana nimesoma nae shule ya msingi, 1996 mpaka 2001. Alikua ni kati ya marafiki tuliosaidiana sana katika masomo yetu ya shule ya msingi.
Basi, kwa sababu ya kuamini kuwa ni mtu makini, nilimkaribisha nyumbani, nikamwandalia msosi, tukala na baadae tukapata muda wa kuzungumza mawili matatu.


Ukafika muda wa kulala, tukaenda tukajipumzisha, ingawa ye alibaki kidogo sebuleni kuangalia TV na baada ya kama dakika 40 hivi nae akaja kulala.


Tumelala mpaka ilipofika mishale ya asubuhi, mie nikaamka kwenye saa moja hivi, nikawa napiga stori na mdogo wangu niliekua nae pembeni yangu. Ye huyo rafiki yangu alikua bado amelala, ingawa alikua anajigeuza geuza, nikidhani bado yuko kwenye usingizi. Baada ya kuwa amejigueza geuza hivyo, kidogo tu akainuka, akaenda washroom kidogo, baadae akaaga hapo hapo. Nikamwuliza mbona unaaga mapema sana, kwa nini usisubiri tunywe chai ndo uende. Akasema hapana anawahi Mbezi kwenye interview kwa hiyo kama vipi atarudi baadae ili aje kunywa chai wakati akiwa njiani kurudi kwake Magomeni(alidai anaishi huko). Akanambia nimsaidie nauli kidogo. Nikarudi chumbani nikachukue vijisenti kidogo nikampatia. Tukaagana.


Mishale ya saa tatu kasoro hivi nikawa nahitaji kuingia kwenye internet kupitia simu yangu. Mara nyingi simu huiacha kwenye chaji, chini ya kitanda, kwenye kapeti. Nilipoangalia pale sikuiona simu, nikiipiga haipatikani wakati nimeiacha kwenye chaji na ilikua ON. Simu yangu ilikua aina ya SAMSUNG GALAXY NOTE II, ambayo gharama yake ni kati ya laki sita na saba. Basi nikatatufa weee nkawa siioni. Lakini nkajiuliza inakuaje kitu kipotee, tena ndani, na wakati nimekiacha kwenye chaji wakati nalala, halafu simu yenyewe ni kubwa, kwa hiyo ni rahisi kuiona, halafu mbaya zaidi haipatikani. Basi nikajua hii simu imeibiwa. Na mtu wa kwanza kumhisi ni huyo rafiki angu tulielala nae.


Nikaona nikimpigia moja kwa moja inawezekana namwonea. Nilichofanya, ikabidi nianze kuulizia tabia yake. Dah! Kumbe rafiki yangu alishabadilika siku nyingi amekua tapeli mkubwa. Katapeli watu kibao. Kila mtu akawa ananishangaa kwa nini nakaribisha nyumbani mtu kama huyo. Nikasikitika sana, nikajua moja kwa moja ni yeye ndie aliechukua simu.


Nikampigia simu nikimwambia arudishe simu yangu. Akakataa kwamba hajachukua simu, na akasema, yaani yeye kufika kwangu siku hiyo inakua tabu mpaka naanza kumsingizia kaiba. Nikamwambia basi njoo nyumbani angalau tusaidiane kuitafuta maana tumelala wote. Akanikatia simu, nikawa nampigia hapokei, wala SMS hajibu. Nikasikitika sana.


Nikawa najiuliza nitaipataje hii simu yangu nzuri niliyokua naipenda, na bora simu unaweza nunua tena, ila kulikua na documents (nyaraka) mhimu niliziweka kwenye simu ile, na zilikua na assignment na projects zangu. Nitaipataje.
Basi, siku nzima ya jumamosi na jumapili nilijitahidi kuwasiliana nae bila mafanikio. Ingawa siku ya jumamosi usiku aliniahidi atakuja nyumbani baada ya kushauriwa na moja ya rafiki yangu wa shule ya msingi, lakini sikumwona kufika.
Jumatatu majira ya saa tano akanipigia simu, nilikua ndani ya training ya kiofisi, akanambia kuwa, simu yangu kaiweka bond (sidhani kama ilikua kweli) ya TSh elfu arobaini, kwa hiyo akataka nimrushie elfu arobaini ili aikomboe simu yangu ndo aniletee, na akanitishia kuwa, nikichelewa hiyo simu sitaiona tena.


Nikajiuliza, simu ni yangu, kaiiba, halafu kaiweka bond (naamini bond ni uongo), halafu nimrushie pesa akakomboe simu yangu? Duh! Kweli ujinga mzigo.
Ila kwa sababu niliihitaji sana hiyo simu, nikamwuliza, "Uko wapi??" akanambia, "Niko Africana.." .. Nikamwambia, hapo Africana, kuna tawi la ofisi yetu, kwa hiyo nenda pale ofisini, nitawaelekeza wafanyakazi wa hapo wakupe elfu arobaini na uwaachie simu yangu. Akanambia, "Aiseee!! Mie naona unazingua, huyu jamaa(jamaa wa bond) nikimwacha hapa sitamwona tena, kwa hiyo inabidi urushe tigopesa fasta ili niikomboe simu (uongo)"..


Basi nikamwambia,
"Nielekeze mlipo ili nimtume mtu aje hapo akupe hela na achukue simu"..

Akanambia, "Huyu jamaa hataki mtu yeyote aje hapa..."
Nikamwambia, "Basi nipe namba ake nimpigie ili asiondoke na simu yangu"
Akanambia, "Hapana we tuma tu hela, halafu naona unazingua simu unaweza usiione tena.."
Nikamwambia, "Basi mie nakuja huko Africana ili kulishughulikia hilo swala"
Nikatoroka training nikaenda mpaka Africana, nilipofika, nikampigia simu ili aje anipe simu yangu. Kumpigia akanambia, "Tuma kwenye tigopesa yangu"..
Nikamwambia,"Sasa kama ntakutumia kwenye tigopesa hiyo simu naipataje (kupitia tigopesa)? "..
Akanambia, "J ... mie naona unazingua, mie nakwambia tuma kwenye tigopesa we unachelewa, hii simu utakua hauipati tena"..


Nikamwambia, "Hivi nimekukosea nini mpaka unanifanyia unyama wa aina hii, simu yangu halafu initese kiasi hiki??"..
Basi akanikatia simu. Nikaenda mahali, nikakaa, nikawa nampigia hapatikani.. Ilinichukua kama masaa mawili hivi nikiwa nimekaa kwenye ki restaurant flani maeneo ya africana, nikijifariji na lunch kidogo, huku nikisubiri nikiamini huenda tukaonana nikachukua simu yangu.
Baadae nikajaribu kumpigia akawa anapatikana nikamwambia, nimekusubiri sana bila mafanikio. Nikaamua kurudi zangu home, na mpaka dakika hii sijaipata simu yangu.


CHA KUJIFUNZA.
Usiamini mtu yeyote, hata kama ni rafiki yako. Hakikisha unamjua vizuri kabla ya kumkaribisha nyumbani kwako. Ameniudhi sana, maana ni mtu ambae nimekua nae, tumezaliwa wote sehemu moja, tumekua wote, tumesoma wote, tulikua tukisaidiana enzi hizo halafu anakuja kuwa mtu wa kuniibia, kunipotezea documents zangu za mhimu ambazo ni za mhimu sana kwenye kazi zangu. Kiukweli nimemchukia sana na itanichukua muda kumsamehe na kumsahau. Ipo siku tutakutana tu, na sheria lazima ichukue mkondo wake.

Roho inauma as if nimefanyiwa mimi huyo ukimtia mikononi mle kwanza kboga na condom lkn kisha tandika sanaa nyofoa meno yake mawili mkate kidole cha mwisho mguu wa kushoto alaf mwisho kabisa mpe tindikali achambie wrxcghjcfuonvxdje zake huyo
 
Aisee pole mkuu mi ilishawah kunikuta kwenye daladala jamaa tulikaa wote kitaa akaniomba nimsaidie kias fulan cha pesa nikampa ile anasema akatafute chenji jamaa hakurud tena......
Dunia imebadilika sana siku hzi hakuna wa kumuamin
 
Tena inawezekana yupo humu humu jamiiforums. cc Mwizi wa Einstein, rudisha simu ya watu unachofanya siyo deal wala nini.
 
Mzee mbona hiyo simu unaipata hata akibadil lain ime no.hazidanganyi hata mie nimepoteza simu kadhaa zote zikarud na kichapo nikawapa.
 
Next time report such cases to Police right away! Huyo jamaa Mnge mkamata fasta. How? Simple. As long as una namba yake ya simu. It was all over. How?. Report your cases to Police.
 
Roho inauma as if nimefanyiwa mimi huyo ukimtia mikononi mle kwanza kboga na condom lkn kisha tandika sanaa nyofoa meno yake mawili mkate kidole cha mwisho mguu wa kushoto alaf mwisho kabisa mpe tindikali achambie wrxcghjcfuonvxdje zake huyo


We mtu umeniogopesha!
 
wanasema ………….."anayedhulumu , na anaye kubali kudhulumiwa wote sawa"
 
Mzee mbona hiyo simu unaipata hata akibadil lain ime no.hazidanganyi hata mie nimepoteza simu kadhaa zote zikarud na kichapo nikawapa.

Ilikuwaje kiongozi? Share with us.
 
Nyie mnazidi kum entertain,mwanike hapa majina yake na picha yake kama ipo,uone fasta tu kama hujamtia nguvuni.
 
Ilikuwaje kiongozi? Share with us.

Simu zangu mkuu wala sihangaiki kuweka ma security.huwa kama binadamu napoteza na kuibiwa.lakin huwa nikipoteza hasa naangalia ime application kujua namba gan inatumika kwa simu sangu sasa hafu na tress location iliopo.kama kunabulazimu wa kufanya extraction of numbers ambazo zinawasiliana nafanya hivyo au laa kwakuwa namba ninayo basi natumia tu mbinu za kiintellegensia kukutana na jamaa nachukua changu na kichapo namwachia pia.kumbuka kwamba aliyeiba simu lazima akauze au abadil namba kwaiyo simu itatumiwa nabline nyingine tu.ni
 
pole sana, kama una details za hiyo simu niPM ntakusaidia tutaipata kwa mud mfupi bila jasho .
 
dah, pole sana mkuu, inasikitisha na inachukiza sana, anyways Mungu ni mwema sana, ameskia kilio chako.
 
Kosa kubwa tunalofanya wengi wetu ni kuwachukulia rafiki zetu wa kitambo kwamba bado wana tabia zilezile tulizowafaham mara ya mwisho tulipokua nao karibu. Tunasahau kwamba hao rafiki zetu wameshapitia mabmbo mengi na changamoto nyingi kwenye maisha ambazo zimewabadilisha kabisa tabia, misimamo na jinsi wanavyochukulia mambo.

cc The Boss

Loo umenikumbusha friends united ambayo iliharibu ndoa za watu wengi na hata baadhi kutapeliwa na kuuwawa eti kukutana kwa njia ya internet kwa uliosoma nao enzi. Watu wanabadilika na maisha
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom