ushuzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ushuzi

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by kilimasera, Apr 1, 2012.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Apr 1, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Jamaa fulani alikuwa na tabia ya kujamba kwa nguvu kila aamkapo asubuhi. Mkewe alikerwa sana na tabia hiyo, alimkataza akachoka, siku moja akamwonya kuwa iko siku badala ya pumzi, utumbo utakuja kumtoka. Jamaa alicheka sana kusikia hilo. Siku moja mke alilazimika kuamka alfajiri awatengeze kuku kwa ajili ya sherehe, alipowatoa utumbo wale kuku akakumbuka alichowahi kumwambia mumewe akaamua kumtisha

  , akamnyatia mumewe ambaye alikuwa bado amelala na kumuwekea utumbo kwenye pajama lake na kurudi jikoni. Muda si mrefu mwanaume aliamka na kufanya mambo yake kama kawaida, lakini akahisi kitu cha baridi ndani ya suruali, ile kuvuta si akakuta utumbo. Akapiga ukelele,’Mama yangu nimekufa’. Mke wake aliposikia akacheka peke yake. Kimya cha kama nusu saa kilipita. Hatimaye jamaa akamfuata mkewe jikoni akiwa amelowa jasho pajama nzima.
  JAMAA: Mke wangu yale uliosema leo yametokea.
  MKE: Yepi jamani?
  JAMAA: Mke wangu utumbo si umetoka kama ulivyosema
  MKE: Pole mume wangu, sasa?
  JAMAA: Namshukuru Mungu, nimejitahidi nimeweza kuurudisha ndani wote.
  MKE: Mungu wangu umefanyaje?
   
 2. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #2
  Apr 2, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,816
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Unajua kusoma?
  Haya soma thread yenye kichwa cha habari "asiye sikia la mkuu" kwenye page hii.
   
Loading...