Mtoto wa Bamkubwa Aliyefeli Kila Idara

Mtoto wa Bamkubwa Aliyefeli Kila Idara

baharia 1

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2019
Posts
2,989
Reaction score
4,369
Wakuu, nimeona leo niteme nyongo ya mwisho kabisa ili kila mtu humu ndani aelewe kiwango cha chuki na kichefuchefu nilichonacho rohoni dhidi ya huyu kiumbe.

Nataka niweke wazi mapema kuwa hata wakati ule nilipoanzisha uzi wa kuwasema na kuwatandika bodaboda humu jukwaani, picha iliyokuwa inajirudia kichwani mwangu, na mtu niliyemlenga kwa asilimia mia moja, alikuwa ni huyu huyu ndugu yangu ambaye ni mtoto wa bamkubwa wangu wa damu.

Kiumbe huyu ndiye kielelezo kamili cha jinsi mtu anavyoweza kufeli kuanzia malezi, shule, hadi akili ya kawaida ya kibinadamu, kisha akahamishia huo ujinga wake wote barabarani.

Alianza kuonyesha dalili za kuwa sifuri tangu akiwa shule ya msingi, ambapo wakati wenzake wanasoma yeye alikuwa bize kuchora mapikipiki kwenye madaftari. Malezi ya bamkubwa nayo yalikuwa ya kulegalega, mtoto akifanya ujinga anaachwa tu kwa kisingizio cha kwamba atabadilika akikuwa, na matokeo yake akaja kufeli vibaya mno kidato cha nne na kupata sifuri iliyonyooka utadhani imechorwa kwa bikari.

Baada ya maisha kumtandika makofi na kukuta kila mlango wa maana umefungwa kwa sababu ya ujinga wake, akakimbilia kule kulikofiti akili yake fupi kama ya kuku kwenye bodaboda. Bamkubwa kwa upofu wa mapenzi ya mzazi akajikamua, akauza hata kiwanja chake cha urithi na kumnunulia pikipiki mpya na hapo ndipo janga rasmi lilipoanza huku ule usemi wangu kuwa sekta hii ni kimbilio la takataka ukithibitika kwa asilimia mia moja.

Ukikutana na huyu ndugu yangu barabarani utatamani utapike utumbo wako wote kwa sababu jamaa ananuka vumbi kuanzia utosini hadi kwenye kucha za miguuni zilizojaa uchafu mweusi. Nguo zake hazijawahi kuona sabuni tangu mwaka uanze, zimekakamaa kwa jasho lililochanganyika na mafuta ya petroli na oili chafu hadi zinatoa uvundo usiovumilika ambao ukipishana naye ni kama mzoga uliokaa juani kwa siku tatu.

Inasikitisha na kutia kichefuchefu kuona jitu zima lenye mvi hadi kwenye kidevu linarudi nyumbani usiku likiwa limechoka hoi, linanuka uvundo kama dumu la chooni, huku mfukoni likiwa na buku tano tu ya mahesabu!

Ukiacha uchafu wa mwili, akili ya huyu ndugu yangu ndiyo sifuri kabisa kwani anapoingia barabarani na lile doli lake la chuma anakuwa kama kuku mwenye mdondo, haangalii kushoto wala kulia, hajali taa nyekundu, wala hajali gari kubwa linalokuja kwa kasi. Yeye kazi yake ni moja tu ya kuona wapi pa kupenyeza kichwa chake kigumu, hajui sheria, hajui ustaarabu, na matokeo yake anakuwa kichefuchefu tupu kwa watumiaji wengine wa barabara, Kila siku anagombana na trafiki, anakamatwa kwa ukaidi wa kijinga wa kukataa kuvaa kofia ngumu, au kubeba abiria watatu kwa ajili ya kupigania buku jero,

Kibaya zaidi ana ile tabia ya kishamba niliyoitaja ya ushirikiano wa kijinga wa kinyuki, ambapo siku aliyojigonga wenyewe nyuma ya gari la mtu kwa sababu ya uzembe wake, lile genge la wajinga wenzake lilijazana pale na makelele na fujo wakidai bodaboda ameonewa bila hata kujua chanzo cha tatizo.

Mwisho wa siku huyu ndugu yangu anaishi maisha ya hovyo, mke wake anateseka kwa njaa na upweke nyumbani, huku yeye akipiga umbeya vijiweni kuanzia asubuhi hadi usiku akisubiri ofa za elfu moja moja. Ni msiba mzito unaogharimu nguvu kazi ya taifa, na chuki yangu kwake haina kikomo kwa sababu sekta hii isipofutwa au kudhibitiwa kwa mabavu tutaendelea kujaza maiti mochwari na kuzalisha wajane na mayatima kila kona kwa sababu ya watu wenye akili fupi kama za huyu mtoto wa bamkubwa wangu,
 
Wakuu, nimeona leo niteme nyongo ya mwisho kabisa ili kila mtu humu ndani aelewe kiwango cha chuki na kichefuchefu nilichonacho rohoni dhidi ya huyu kiumbe.

Nataka niweke wazi mapema kuwa hata wakati ule nilipoanzisha uzi wa kuwasema na kuwatandika bodaboda humu jukwaani, picha iliyokuwa inajirudia kichwani mwangu, na mtu niliyemlenga kwa asilimia mia moja, alikuwa ni huyu huyu ndugu yangu ambaye ni mtoto wa bamkubwa wangu wa damu.

Kiumbe huyu ndiye kielelezo kamili cha jinsi mtu anavyoweza kufeli kuanzia malezi, shule, hadi akili ya kawaida ya kibinadamu, kisha akahamishia huo ujinga wake wote barabarani.

Alianza kuonyesha dalili za kuwa sifuri tangu akiwa shule ya msingi, ambapo wakati wenzake wanasoma yeye alikuwa bize kuchora mapikipiki kwenye madaftari. Malezi ya bamkubwa nayo yalikuwa ya kulegalega, mtoto akifanya ujinga anaachwa tu kwa kisingizio cha kwamba atabadilika akikuwa, na matokeo yake akaja kufeli vibaya mno kidato cha nne na kupata sifuri iliyonyooka utadhani imechorwa kwa bikari.

Baada ya maisha kumtandika makofi na kukuta kila mlango wa maana umefungwa kwa sababu ya ujinga wake, akakimbilia kule kulikofiti akili yake fupi kama ya kuku kwenye bodaboda,
Bamkubwa kwa upofu wa mapenzi ya mzazi akajikamua, akauza hata kiwanja chake cha urithi na kumnunulia pikipiki mpya na hapo ndipo janga rasmi lilipoanza huku ule usemi wangu kuwa sekta hii ni kimbilio la takataka ukithibitika kwa asilimia mia moja.

Ukikutana na huyu ndugu yangu barabarani utatamani utapike utumbo wako wote kwa sababu jamaa ananuka vumbi kuanzia utosini hadi kwenye kucha za miguuni zilizojaa uchafu mweusi. Nguo zake hazijawahi kuona sabuni tangu mwaka uanze, zimekakamaa kwa jasho lililochanganyika na mafuta ya petroli na oili chafu hadi zinatoa uvundo usiovumilika ambao ukipishana naye ni kama mzoga uliokaa juani kwa siku tatu.

Inasikitisha na kutia kichefuchefu kuona jitu zima lenye mvi hadi kwenye kidevu linarudi nyumbani usiku likiwa limechoka hoi, linanuka uvundo kama dumu la chooni, huku mfukoni likiwa na buku tano tu ya mahesabu!

Ukiacha uchafu wa mwili, akili ya huyu ndugu yangu ndiyo sifuri kabisa kwani anapoingia barabarani na lile doli lake la chuma anakuwa kama kuku mwenye mdondo, haangalii kushoto wala kulia, hajali taa nyekundu, wala hajali gari kubwa linalokuja kwa kasi. Yeye kazi yake ni moja tu ya kuona wapi pa kupenyeza kichwa chake kigumu, hajui sheria, hajui ustaarabu, na matokeo yake anakuwa kichefuchefu tupu kwa watumiaji wengine wa barabara, Kila siku anagombana na trafiki, anakamatwa kwa ukaidi wa kijinga wa kukataa kuvaa kofia ngumu, au kubeba abiria watatu kwa ajili ya kupigania buku jero,

Kibaya zaidi ana ile tabia ya kishamba niliyoitaja ya ushirikiano wa kijinga wa kinyuki, ambapo siku aliyojigonga wenyewe nyuma ya gari la mtu kwa sababu ya uzembe wake, lile genge la wajinga wenzake lilijazana pale na makelele na fujo wakidai bodaboda ameonewa bila hata kujua chanzo cha tatizo.
Mwisho wa siku huyu ndugu yangu anaishi maisha ya hovyo, mke wake anateseka kwa njaa na upweke nyumbani, huku yeye akipiga umbeya vijiweni kuanzia asubuhi hadi usiku akisubiri ofa za elfu moja moja. Ni msiba mzito unaogharimu nguvu kazi ya taifa, na chuki yangu kwake haina kikomo kwa sababu sekta hii isipofutwa au kudhibitiwa kwa mabavu tutaendelea kujaza maiti mochwari na kuzalisha wajane na mayatima kila kona kwa sababu ya watu wenye akili fupi kama za huyu mtoto wa bamkubwa wangu,
Umekosea sana, badala ya kukaa chini na ndugu yako na kumshauri kwa upole umekuja kumnanga huku? Hakuna asiye na ndugu yule mkorofi, wote tunao hao ndugu, lakini kuna namna nzuri ya kuwarejeza ili wawe watu wema, haipendezi kumuacha ndugu yako apotee pia usimseme mbele za watu, Mimi naamini ya kuwa katika ubaya wake ana mazuri yake pia, je umeshawahi kumuangalia kwa mazuri aliyonayo?
Siku zote binadamu hatukamiliki kwa hiyo tafuta njia nzuri ya kuongea na ndugu yako.
 
Nishaongea nae sana
 
haangalii kushoto wala kulia, hajali taa nyekundu, wala hajali gari kubwa linalokuja kwa kasi. Yeye kazi yake ni moja tu ya kuona wapi pa kupenyeza kichwa chake kigumu
Bodaboda mwenye tabia kama hii ndani ya masaa matatu tu barabarani anakua ameshapelekwa mochwari. Sasa kama yupo kwenye game kitambo basi jua ana akili sana ila anawachora tu
 
Nishaongea nae sana
Jenga urafiki na mkewe ili umsaidie ndugu yako, Mashemeji huwa wanatusikiliza sana na kama wewe ni mtu smart atakuelewa sana tu.
Mara nyingi mashemeji wanapenda zawadi zawadi, kwa hiyo unapokuwa na nafasi nenda na zawadi kwa shemeji yako ili uwe naye karibu kisha mpe ushauri wa kumsaidia mumewe.
Kama haogi na habadili nguo maana yake shemeji naye anachangia.
 
Mhindi mmoja Daktari wa mifupa akisikia Tu kuna mgonjwa amevunjika anauliza kapata ajali ya nini na anafanya kazi gani basi akijibiwa ni bodaboda Tu Utasikia akisema "Aaah, Kata guu Yake hiyo"...
 
Sawa mkuu
 
[emoji1787][emoji1787][emoji3]
 
Back
Top Bottom