Ushuhuda wangu: Ulimwengu wa Roho ni halisi (Yesu, malaika, shetani, mapepo na Mbingu ni halisi)

Kinengunengu

JF-Expert Member
May 3, 2021
1,719
4,309
UTANGULIZI:
Kwa majina naitwa Ndetyefose, napenda kutoa ushuhuda wangu binafsi wa Maisha yangu. Lengo la ushuhuda huu ni kueleza yale matendo makuu ambayo Mungu amenitendea kwenye Maisha yangu. Ushuhuda huu ni wangu binafsi na yale niliyoyapitia kwenye Maisha yangu. Kabla ya kutoa ushuhuda huu, napeda niweke wazi ya kuwa mimi sio Nabii,Mchungaji wala sisimamii kanisa ila ni Mzee wa kanisa huku nilipo Moshi

Natumaini ushuhuda huu utawasaidia baadhi ya watu humu. Sitajibu au kureply comment yoyote hadi nimalize Kuandika ushuhuda huu. Pia, nitaficha baadhi ya Personal details kwa sababu baadhi ya member humu nimesoma nao au kukutana nao katika hatua mbalimbali za Maisha yangu. Ushuhuda huu utakuwa na sehemu nne kama ifuatavyo:
1. Maisha yangu ya awali(utototni)
A. Kuzaliwa hadi kumaliza Darasa la Saba
Kuutana na Yesu mara ya Kwanza
Tatizo la Majini mahaba na Belzebul

B. Kidato cha kwanza hadi Chuo
Kubalehe na Majini Mahaba
Maisha ya Ujanani na zinaa

2. Majaribu ya Magonjwa na mauti.
Ugonjwa wa Pressure na sukari
Tishio/Kupandikizwa roho ya Mauti

3. Kutokewa na Yesu na majaribu ya mbalimbali
Kutokewa na Yesu(mara 3)
Kukataa kuhubiri na Mauti
Jaribu la kiuchumi
Kutokewa na Ibilisi na jaribu la kiuchumi

4. Mafunuo juu ya Mbinguni
Malaika na kunichukua
Mbingu na muonekano

SEHEMU YA KWANZA: HISTORIA YA MAISHA YANGU (KUZALIWA HADI DARASA LA SABA).
Kwa Majina naitwa Ndetefyose, ni mtoto wa mwisho toka kwenye familia ya Watoto 7 ambao kati ya hao, Watoto 5 ni wa mama mmoja na wawili ni wa mama mwingine. Nimezaliwa 1980s toka kwa Baba ambaye ni Mtumishi wa serikali na Mama ni mama wa nyumbani.

Familia yetu ilikuwa ni familia ya uchumi wa kati kwani mzee alikuwa mumishi wa serikali na pia alikuwa mkulima maarufu sana huko Morogoro alipokuwa anafanya kazi. Nilianza darasa la kwanza kama kawaida ya Watoto wengine. Katika elimu yangu Mungu alinipa uwezo mkubwa darasani kwani nilikuwa nashika nafasi ya kwanza nay a Pili hadi namaliza STD VII.

Wakati wa utumishi wake mzee wangu alikuwa na utaratibu wa kwenda Likizo nyumbani Moshi kila mwisho wa mwaka na akawa anaenda nasi. Nakumbuka nilipokuwa STD V tulienda likizo na Babu yangu mzaa Baba akanipa zawadi ya kitabu kilichoitwa "Kitabu changu cha hadithi za Biblia". Kitabu hiki ni cha Mashahidi wa Yehova na kilikuwa kinaelelezea hadithi za kwenye Biblia na kilikuwa na picha zinazoonesha hadithi hiyo na wahusika (Bible charactors). Kabla ya Babu yangu kunipa zawadi hiyo, alininenea "kuwa Mjukuu wangu utasoma sana na utakuwa Mchungaji kisha akanitemea mate Mikononi na kunibariki kiuchumi na kielimu". Katika makuzi ya utotoni nililelewa na kukulia kanisani kanisa la K.K.K. T kwani wazee wangu walikuwa wazee wa kanisa katika kanisa lililokuwepo hapo kazini mwa mzee. Kitabu hiki kilizidi nijenga katika Imani, kumjua Mungu na kilinifanya nisome Biblia tangu Mwanzo hadi Ufunuo katika udogo wangu.

Kutokewa na Yesu.
Katika kipindi na umri huo nakumbuka niliota ndoto moja. Ndoto hiyo ilionesha kuwa Ilikuwa Jioni yapata saa 12 kwenda saa 1 jioni wakati jua kuzama, nikaona kivuli kikubwa cha mtu akitokea mawinguni kule jua lizamapo na kile kivuli kikaijaza dunia nzima. Mtu yule alitoka na kuja hadi nilipo lakini sikuweza ona sura yake tokana na mwangaza mkubwa uliokuwa unatoka usoni mwake.
NENO: ZEKARIA 14: 7 – Yesu na kurudi wakati wa jioni.
UFUNUO 1:13-14, 2:18, 4:2-3---- YESU na Sura yenye mng'aro.
Sikuwa nimeelewa ndoto hii inamaanisha nini tokana na udogo kwani nilikuwa STD IV lakini niliiweka moyoni mwangu na hadi sasa naikumbuka.

Majini Mahaba na Belzebul
Wakati wa kukua kwangu sehemu ambayo baba alikuwa anafanya kazi. Kuna sehemu kulikuwa na mti mkubwa wa Mkwaju, nilipokuwa natoka shuleni au kucheza na wenzangu na kupita hapo nilikuwa naokota pesa. Pia, kulikuwa na muembe mkubwa ile ya kizamani napo nilikuwa naokota pesa. Kila mara nilipo kuwa naokota Pesa na nilikuwa nampelekea mama yangu hadi ikafikia hatua mama akawa anahisi labda naiba pesa mahali kwani nilikuwa nampelekea tokana na malezi niliyolelewa. Baada ya kuendelea kukua nikaanza ota ndoto zisizo eleweka na zilizokuwa zinanichanganya na kuniumiza sana. Mara naota majitu yenye makucha marefu yakinipa pesa mara naota nipo chini ya zizi la mbuzi za mzee nafukua mavi ya mbuzi na kuokota hizo pesa. Sikuwa najua maana yake na nikawa napuuzia lakini hadi leo nazikumbuka baadhi ya ndoto hizo. Hapa ndipo palikuwa mwanzo wa kujiungamanisha na majini mahaba na Belzebul na nitaelezea Zaidi huko mbele kuhusu Haya majini mahaba na Belzebul

Nilifanikiwa kumaliza darasa la saba na hatimaye nilichaguliwa kwenda kidato cha kwanza.

Itaendelea...
 
Ukishamjua YESU KRISTO unaanza vita na ulimwengu wa roho, yani majini, mizimu, wachawi wanaanza kupigana nawe.

Hapo ndio ulitakiwa usirudi nyuma ilipaswa usimame na YESU/MUNGU.

Neno la Mungu linasema vita vyetu sio vya damu na nyama ni vita vya kiroho
 
Ukishamjua YESU KRISTO unaanza vita na ulimwengu wa roho, yani majini, mizimu, wachawi wanaanza kupigana nawe.

Hapo ndio ulitakiwa usirudi nyuma ilipaswa usimame na YESU/MUNGU.

Neno la Mungu linasema vita vyetu sio vya damu na nyama ni vita vya kiroho

Ucnisahau
 
Back
Top Bottom