Ushuhuda wa ndoa ya wazazi wangu, baba aliachishwa kazi ghafla miaka 14 iliyopita. Mama amekuwa ndio kila kitu

Ila wewe miaka 14 kuweza? Sio kwamba siku 2 tu ushaanza kumpelekesha Mzee wa watu?
Mimi sitaweza kwakweli, miaka 14 bila kitu cha kufanya seriously??.. Labda kama ni ugonjwa maybe kapalarize au ulemavu nitavulimia ila sio tu kukaa bila kufanya kitu na ana nguvu zake anakula tu na kulala
 
Habari wana JF
Leo nawapa ushuhuda wa maisha ya ndoa ya wazazi wangu...

Baba aliachishwa kazi ghafla miaka 14 iliyopita. Mama anafanya biashara ndogondogo amekuwa ndio kila kitu chakula, mavazi, ada za shule na mahitaji mengine...

Wakati baba anaendelea kufatilia kesi yake ya kuachishwa kazi bila sababu na fidia zake ambazo hakuweza kuzipata mpaka tunamzika mwaka jana RIP....

SOMO
Je, wanawake wa sasa hivi wanaweza kuishi na mwanaume asiye na kipato kwa miaka 14 bila hata kusikia ugomvi wa masuala ya kifedha...

Kila nikimuangalia mama huwa najiuliza, wapi naweza kupata aina hii ya wanawake ili niishi kwa amani nikijua kwamba nina jembe ndani. Hata siku nikikosa naweza kurudi nyumbani nikamwambia akanielewa...

Mahusiano siku hizi bila pesa hayaendi kabisaa....

Ndoa zimekuwa kama business partnership....
Kwahiyo katika hiyo miaka 14 alikuwa anafwatilia kesi tuu bila kujishughulisha na kitu kingine?? Mfano kusaidiana na bimkubwa hizo kazi ndogo ndogo au hata kamchongo kengine?? Miaka 14 yote???
 
Mimi sitaweza kwakweli, miaka 14 bila kitu cha kufanya seriously??.. Labda kama ni ugonjwa maybe kapalarize au ulemavu nitavulimia ila sio tu kukaa bila kufanya kitu na ana nguvu zake anakula tu na kulala
Sasa kibarua kimeota nyasi Mama uwe na uvumilivu siku moja atapata tu hata baada ya miaka 20, univumilie kesho nitapasua mawe
 
Kwakweli mimi hapana.. Nitamtafutia mtaji ilimradi tu apate hata biashara sio tu kukaa hivihivi
 
Kwa hio wewe ndio unatoa mtaji akiuliza umeutoa wapi na wewe huna kazi ya kueleweka zaidi unanijibu nini?
Ndomana napambana nijipate kabisa kiuchumi ndo niingie kwenye masuala ya mahusiano na mapenzi na mtoto wa mtu,, hope mpaka nitakapofunga ndoa nitakua niko somewhere hatakua na mashaka
 
Habari wana JF
Leo nawapa ushuhuda wa maisha ya ndoa ya wazazi wangu...

Baba aliachishwa kazi ghafla miaka 14 iliyopita. Mama anafanya biashara ndogondogo amekuwa ndio kila kitu chakula, mavazi, ada za shule na mahitaji mengine...

Wakati baba anaendelea kufatilia kesi yake ya kuachishwa kazi bila sababu na fidia zake ambazo hakuweza kuzipata mpaka tunamzika mwaka jana RIP....

SOMO
Je, wanawake wa sasa hivi wanaweza kuishi na mwanaume asiye na kipato kwa miaka 14 bila hata kusikia ugomvi wa masuala ya kifedha...

Kila nikimuangalia mama huwa najiuliza, wapi naweza kupata aina hii ya wanawake ili niishi kwa amani nikijua kwamba nina jembe ndani. Hata siku nikikosa naweza kurudi nyumbani nikamwambia akanielewa...

Mahusiano siku hizi bila pesa hayaendi kabisaa....

Ndoa zimekuwa kama business partnership....
Your story ni sawa na yangu. Japo mimi wote walianza saidiana kwa sababu before mama alikuwa mama wa nyumbani tu. RIP mzee, ulitupigania sana.
 
Ndomana napambana nijipate kabisa kiuchumi ndo niingie kwenye masuala ya mahusiano na mapenzi na mtoto wa mtu,, hope mpaka nitakapofunga ndoa nitakua niko somewhere hatakua na mashaka
Aaaha kwa hio mpaka uwe na akiba ya kutosha ndio unaingiamo huko ili kusudi likitokea la kutokea unafanya utatuzi wa haraka, duuh kumbe upo singo au umetoa mfano
 
Mwanamke akikupenda kweli hawez shindwa fanya chochote kwaajili yako. Kumbuka hao hao wanawake unaosema wanapenda pesa huwa wanaenda kuwahonga wanaume wanaowapenda
 
Hii ina kaukweli fulani hivi emu ondoa password hapo
 
  • Thanks
Reactions: _ly
Back
Top Bottom