Nakuwa muwazi. Nashukuru, nilisaidiwa kumpata wa kunioa na rafiki yake mama

Marytina

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
9,384
7,360
@Arusha,Mama mchagga (Mmaranguu), baba mngoni

Ndege mjanja hunaswa tundu bovu, baada ya kuchemka mwishowe nilisaidiwa kumpata wa kunioa 'Asante'
Mama aliwakataa wachumba zangu wawili, watatu alikuwa Mkibosho very handsome akisoma Uhandisi UDSM baba yake akiwa ni tajiri wa Hardware chains Arusha na Moshi. Mama alimkataa na akawaka kama mbogo na laana akatamka ‘Hata nife sitaki uolewe na mkibosho’

Kuna rafiki yake Mama akiitwa Mama Kavishe (Mchagga wa Rombo)akiwa Tour operator mdogo kipindi kile akanipigia simu, njoo mwanangu kuna zawadi nataka kukupa….Nilipofika akaniambia Marytina usitake kutuua mama zako kabla ya muda…”achana na huyo mkibosho” na tena naomba nikuchagulie mume….

Nikacheka…unichagulie, Ndio niruhusu nikuchagulie na hutajutia….na tunataka uolewe mapema kabla ya 23 years tupate mjukuu wa ndoa.Nakuchagulia mtu ambaye anaweza kuwa bora kwako na kwa familia. Nani huyo….nani huyo mama unataka niolewe naye..akanijibu LOTII, LOTII, LOTII…akaniambia waweza kwenda chukua funguo hamna dereva wa kukupeleka nyumban na hiyo CRUZA haiendi porini wiki ijayo nenda hata mjini (Nairobi) kajitafakari

Baada ya wiki nikarejesha gari na kukutana tena na Mama Kavishe…

Marytina: Mama alikuwa serious?

Mama Kavishe: Ndio na hata ningekuwa na binti wa kumzaa ningemwozesha LOTII,

Marytina :Lakini Mama mbona LOTII ni kama kaka yangu, na sikujua atajakuwa mpenzi wangu so mambo mengi nimemweka wazi tokea utoto? na Hajawahi kunitongoza?

Mama Kavishe : Koma na ukome…wewe Mngoni/Mchagga, LOTII Mmasai/Mmasai huo undugu uko wapi??? Hayo uliyomweka wazi ndio kinga yako kwenye huo uhusiano na tunajua anakupenda anakuheshimu ndio maana hawezi kukutongoza

Marytina: LOTII sasa mara ni mpishi, mara ni mbeba mizigo yupo yupo tu kwenye utalii bila profession sio tour guide, sio dereva, sio mpishi mwenye vyeti….kuna kipindi anakaa bila kazi miezi sita anakuwa kwao kijiweni ILBORU tutaishije mama? Ni form four tu hamna hata ndoto za kazi

Mama Kavishe: Kwa hiyo unampenda ila unakwama hapo….kwenye carrier & professionalism? We will help you to turn him around….step by step ila usimwambie hili. LOTII ana positive comments kwa kila aliyefanya nae kazi hata mimi nimefanya naye kazi kadhaa kwa uaminifu sana hivyo anaelekezeka

Marytina : Kwa hiyo ntamwanzaje wakati namheshimu, mbona kituko??? Na kama ana mtu tayari?

Mama Kavishe : Fanya uwezavyo kufanya ndani ya miezi mitatu nataka kuona ushahidi wa uwepo wa mahusiano …anzia kumpeleka DRIVING kama just rafiki na jirani…akijua nitampa CRUZA kama dereva, MKIFUNGA NDOA tutawapeleka UGANDA & KINSASHA, kisha SOUTH AMERICA, kwa kingereza , kifaransa na spaniola. Kisha German ….wewe nay eye mtakuwa Tour guides….the rest will be history ntajua mtakavyoendelea ila mkikwama tupo..

SASA HUYU LOTII NI NANI….

Utotoni nilipitia historia ngumu kidogo, tukiisha kama vitajiri miaka hiyo Arusha ILBORU, gafla baba, mjomba walitupwa korokoroni, Tukakimbilia Kenya (Mama na wadogo zangu wawili) baadae mama akakamatwa na kurejeshwa Tanzania kuunganishwa kwenye kesi .

Mama akaachiwa baada ya miaka mitatu, ila tayari dunia ilishaanza kunimeza kwan nililazimika kuwalea wadogo zangu mwenyewe (ingawa Mama alikuwa na hela nyingi benki) huku tukiendelea na Chuo na shule .Tulirejea TZ tukanunua nyumba njiro na mama alisema tusipende tembelea ILBORU.

Kuna siku nikaenda ILBORU….nikakutana na LOTII (mmasai, mvulana, jirani yetu, akisoma Lyamungo, akitumia muda mwingi tokea namfaham kushinda kwetu nyumbani ILBORU na nilimchukulia kama KAKA)…Akanikumbatia akalia akaniambia kwa nin tuliondoka bila kuaga hata kwa wazazi wake? Nilijaribu kumweleza akanielewa…

YAAN LEO MIMI NA LOTII NI MKE NA MUME NA WATOTO...TUKIZURURA KUSINI MWA JANGWA LOTE LA SAHARA TUTAKAVYO..asante mama KAVISHE,
 
Kuna kitu ni very serious kuhusu watu wa kibosho hasa kuoa na kuolewa, sana sana kuolewa.

Nimewahi kuwa nae binti mkibosho na wazazi wangu pamoja na watu wa karibu wakakataa kabisa kuingia kwny ndoa na huyo mkibosho.

Baada ya siku nyiingi mbele ikabidi nimshukuru Mungu kwa kutoingia kwenye ndoa na yule mkibosho.

Nilichogundua ni kwamba, watu wako wa karibu wale wanaokujua hasa wazazi, ndugu n.k sana sana watu wazima wenye ndoa zao na maisha yao, wakikwambia kitu huwa kwa 90% wapo sahihi.

Mungu atusaidie kwenye maamuzi ya kuoa wanaume na kwa wanawake pia.
 
Labda tumegee siri tusiyoijuwa kuhusu Wakibosho.
 
Kuna fumbo kubwa pale wazazi wetu wa kwanza Adam na Hawa walipokosea kwa tamaa.

Mpaka leo hii tunateseka ktk maisha kutokana na tamaa, mambo mazuri yalojificha Mungu kuna namna ameyaweka ili umtafute ujue.

Shetani ili kutupoteza huwa analeta mazingira ya tamaa, ataleta watu, mali n.k ili utamani kisha akupige pingu.
 
Kuna kitu ni very serious kuhusu watu wa kibosho hasa kuoa na kuolewa, sana sana kuolewa.

Nimewahi kuwa nae binti mkibosho na wazazi wangu pamoja na watu wa karibu wakakataa kabisa kuingia kwny ndoa na huyo mkibosho.

Baada ya siku nyiingi mbele ikabidi nimshukuru Mungu kwa kutoingia kwenye ndoa na yule mkibosho.

Nilichogundua ni kwamba, watu wako wa karibu wale wanaokujua hasa wazazi, ndugu n.k sana sana watu wazima wenye ndoa zao na maisha yao, wakikwambia kitu huwa kwa 90% wapo sahihi.

Mungu atusaidie kwenye maamuzi ya kuoa wanaume na kwa wanawake pia.
wakibosho wana nini kwani mkuu
 
Labda tumegee siri tusiyoijuwa kuhusu Wakibosho.
Niliambiwa kuwa, huko wanawake wana nguvu sana ndani ya ndoa kuliko wanaume kitu ambacho hakitakiki kabisa ndani ya ndoa.

Kutokana na mwanaume kuwa chini, ambavyo sio nature, mwanaume atapita ktk mateso ya akili na nafsi, hapo ndipo kicho kinapokujia.

Pili, niliambiwa wanawake wa huko wana ubabe na kutaka uhuru zaidi ktk maisha yao, mkifika hatua fulani ya mafanikio, sio rahisi mwanamke akawa na ww moyoni mwake. Hapo atatamani uondoke duniani ili awe huru zaidi.

Tatu, ni watu wanaojali kujenga makwao na familia za kwao zaidi kuliko kitu kingine.

Kwahiyo mkuu niliambiwa hayo ila mimi kama mimi Allen, nathibitisha haya baada ya kukaa nae ktk mahusiano kwa almost 2 years.

1. UJEURI.
2. UKATILI.
3. HASIRA NA VISASI.
4. TAMAA ZA MALI, HAKUWAHI KURIDHIKA HATA UMHUDUMIE VIPI.
5. KUJISIKIA, SIFA N.K
 
Niliwahi kuambiwa 'Allen huko kibosho wenzio tunapiga tu na kutembea, huko hatuoi, ukiweza mzalishe kisha lea ila usithubutu kuoa'.

Ilinipita miezi isiyopungua 10 kuthibisha hii kauli ya wadau. Nikazama na JF, kuna thread jamaa alianzisha kuhusu mwanamke wa kibosho, wadau JF walitiririka sana, yote yalosimwa mule ndani yalikuwa yanaringana kabisa na alowahi kuwa mpenzi wangu.

Katika ile thread jamaa naenikabidi azame kumfatilia mpenzi wake, hatimae akaghairi kumuoa pia kutokana na tabia zao.

Sipo hapa kuponda makabila ya watu ila wanaume tujitafakari saaana kabla ya kuingia ndani ya ndoa.
 
Hii thread kuhusu watu wa kibosho ilifungua saaaana akili.

Niliambiwa kuwa, huko wanawake wana nguvu sana ndani ya ndoa kuliko wanaume kitu ambacho hakitakiki kabisa ndani ya ndoa.

Kutokana na mwanaume kuwa chini, ambavyo sio nature, mwanaume atapita ktk mateso ya akili na nafsi, hapo ndipo kicho kinapokujia.

Pili, niliambiwa wanawake wa huko wana ubabe na kutaka uhuru zaidi ktk maisha yao, mkifika hatua fulani ya mafanikio, sio rahisi mwanamke akawa na ww moyoni mwake. Hapo atatamani uondoke duniani ili awe huru zaidi.

Tatu, ni watu wanaojali kujenga makwao na familia za kwao zaidi kuliko kitu kingine.

Kwahiyo mkuu niliambiwa hayo ila mimi kama mimi Allen, nathibitisha haya baada ya kukaa nae ktk mahusiano kwa almost 2 years.

1. UJEURI.
2. UKATILI.
3. HASIRA NA VISASI.
4. TAMAA ZA MALI, HAKUWAHI KURIDHIKA HATA UMHUDUMIE VIPI.
5. KUJISIKIA, SIFA N.K
Mimi huwa siamini sana kanuni ya one size fit all.

Unachokiandika wewe nimewahi kuona Wamachame ndio wanatuhumiwa hayo, lakini katika Wamachame ninaowafahamu sijaona hiki.

Mimi nadhani kikubwa ni mwanaume mwenyewe na umekwenda kuoa familia gani?

Kwa sababu hili swala ni mtambuka hata wanawake wanyantuzu wanashutumiwa kwa ushirikina, wahaya na limbwata la Shuntama, Warangi, wapare, wanyiramba hawajui kukataa.

Sasa hapo ukiingiza jamii nzima kwa maoni yangu inakuwa siyo sahihi.
 
Mkuu nakuheshimu sana, nakuona kule Jukwaa la Sports, nakuona ni Mwananchi mwenzangu.

Mimi nilikuwa na mtazamo kama wako, niliambiwa hayo maneno kuhusu hao watu ila nkapuuzia, miezi kadhaa mbele niliona kila rangi ambayo before sikuiona.

Niliwaambia wale watu kuwa hakuna kabila lililokamilika, kila kabila kuna mapungufu yake, mimi nimempenda na mimi sioni hayo mapungufu mnayoeleza.

Mkuu Mkuu Mkuu, takriban miezi 10 mbele au 11 nikajua Allen nilikuwa nimeshajichimbia kaburi, ilibaki niingie mwenyewe tu kisha nifukiwe.
 
Hongera kama umeweza kufanya utafiti kabla ya kuingia kichwakichwa.

Ndoa nyingi zimegeuka Jehenamu kwa sababu waowaji hawakujipa nafasi ya uchambuzi yakinifu.
 
Hongera kama umeweza kufanya utafiti kabla ya kuingia kichwakichwa.

Ndoa nyingi zimegeuka Jehenamu kwa sababu waowaji hawakujipa nafasi ya uchambuzi yakinifu.
Nakubaliana na wewe 100%, baada ya mambo yangu kuanza kwenda kombo, nikaanza kuzama zaidi kutafuta ukweli juu ya hawa watu, mpaka huku JF nikazama ndo nikagundua mengi zaidi zaidi.

Nilimpenda sana mkuu, sikuwahi kuwa serious ktk mahusiano kama ambavyo nilikuwa na yule binti, hakuna kitu ambacho alikosa ila ndo hivyo mkuu.
 
Back
Top Bottom