Ngoja nikushambulie kidogo....
Ogopa sana kuhisi huko uliko ndio sahihi kuliko pengine....
Hata mimi niwewahi kupata manufaa makubwa baada Tu ya kutoa sehemu ya 10% ya mapato yangu....
Ngoja nikupe uhalisia...
Mwezi wa 8 mwaka jana mmoja wa marafiki zangu alikuja kunitembelea ofisini na hivyo kufanya uhalifu wa kuiba fedha (mapato) ya taasisi ninayoifanyia kazi.... Hali iliyonipekea kuwa na changamoto ya kukosa usingizi kwasababu ya fedha iliyoibiwa ijapokuwa uongozi wa Taasisi uliamua kuisamehe ile fedha baada ya mimi kumtajia muhisiwa ambaye wao wanamfahamu vyema kutokana na matukio yaliyowahi kutokea hapo nyuma kabla ya Mimi kuwa muajiriwa ndani ya hiyo taasisi...
So kuanzia August mpaka December sikuwa vizuri kifedha kwasababu nilijikuta naingia kwenye madeni yasiyoeleweka.... Nakumbuka yalifikia kama laki 756,000 sasa December 20 nilikuwa kwenye lindi la mawazo hivyo nikawa nawaza naanzaje 2022 nikiwa na madeni?
Ila neno ninalolitumia kila siku ninapokuwa kwenye changamoto ni MUNGU ANAJUA NI KIPI UNASTAHILI, MUAMINI ATATENDA.... Jioni niko kwenye kibarua ikapigwa simu nahitajika kwenye kikao cha siku 3 nje ya mkoa.... Lakini changamoto sina hata Mia mbovu.... Kawaida ofisi inafungwa saa kumi na mbili Ila Mimi nikajikuta nazidisha mpaka saa moja na nusu still niko kibaruani na huku nikiwa nawaza ni wapi nitaenda kupiga sound nipate atleast laki 2.5?
Mungu si athumani alikuja MTU saa mbili kasoro usiku akaniuliza kama naweza mpatia huduma hivyo nilimpa na akaongeza angependa watoto wake kama watano hivi wafanyiwe procedure ndani ya week hiyo nikamwambia inawezekana na akaomba aniachie advance ya laki 1.2 hivi so halafu akaondoka ... Naapa mbele ya Mungu nililia na nikajiuliza hivi inawezekana mimi ni mtoto wa mwisho wa Mungu mbona ananijali hivyo?
In short, ukienda kwenye seminar usisahau na ona umuhimu wa kuweka TGS kubwa




utanishukuru
Paap baada ya seminar tukaingiziwa mpunga mrefu nilioweza kukamilisha madeni yote na kuwapatia fedha ya Christmas na mwaka mpya ndugu zangu....
Ninachotaka kusema hasa kwetu sisi wakatoliki tunao Hama Hama bila sababu, tusali kwa kukiri kweli na tuamini kweli tuache huu mchezo wa kusali kwa mazoea....
Next time, nitajatoa ushuhuda wa Ekarist Takatifu uliowahi kunitokea nikiwa mtumikiaji (ministrant) Parokia moja iliyopo Jimbo kuu la Dar es salaam
Ushuhuda mwingine, mbele ya Groto la Bikirira Maria 2019
Mwingine 2020
Na huu niliouelezea ni December 20, 2021
Amini katika unachokiamini usikubali kuyumba...