mpwa
Elli nilivyomaliza form 6 niliomba UD tukafanya mtihani wa chuo nika'apply na diploma ya ualimu matokeo ya diploma yalitoka mapema kabla ya yale ya chuo nimechaguliwa TTC Korogwe kwa masomo ya Geography na Mathematics (GM),
wiki iliyofuata yakatoka ya chuo UDSM nimechaguliwa Architecture miaka mitano, kwa wakati ule wa mheshimiwa sana mkapa walimu walikuwa ndo wenye hela vijijini nilijishauri sana kusoma ualimu lakini mmmh!, bora si kwenda ualimu.
Wakuu
Elli na
zumbemkuu.
Nawauzieni siri! Kazi nzuri niya mwenzako, na jitihada zako ndio zitakutoa.
Uzuri wote
Elli na
zumbemkuu) kwa kuwa mnatokea Lushoto mtakuwa mna mfahamu vizuri Mwalimu Soka, mwalimu Soka alikuwa anakaa Chakechake akifundisha Kitopeni mimi nikiwa bwana mdogo (Chabebi) nikisoma Hazina (Lushoto Primary kwa sasa). Nilisoma tuition kwake, alikuwa anachacharika kwenye kila aina ya kitu kinachoita kuingiza pesa! Leo Mwl Soka yuko kwenye mitumba kesho yuko kwenye Mbao, leo amefungua Glossary anauza bia, mara kesho amekuwa wakala wa bia wilaya ya Lushoto, mara anafuga yale madubwana ambayo nikiyaona lazima nipige Astakafuli! Mara anakusanya mahindi na kuuza. Yaani alikuwa na jitihada na vurugu za kutafuta! Alithubutu!
Leo mwalimu Soka ni miongoni mwa matajiri wakubwa pale Lushoto! Kwa taarifa yenu nilikutana naye miaka kama 3 iliyopita bado alikuwa anapigisha chaki kama kawaida! Kumbukeni, hakuwa akifundisha sekondari na wala hakuwa na elimu kubwa ya kiwango cha shahada kama chenu
Elli na
zumbemkuu).
Mwingine yuko Handeni maarufu sana kwa jina la TEACHER, nilikutana naye Mkuzi akitokea Kwemakame nilikuwa nasubiria gari hadi Lushoto mjini kisha nikamate zangu Coaster hadi Mkoa (Tanga), nikapiga mkono gari yake akasimama. Akuliza "Ndio kaka nikusaidie nini ndugu yangu"? Nikamuambia "Samahani Bro, naenda Lushoto naomba unisaidie lift nimesubiria gari muda mrefu hapa naona haziji" akaniambia "Usijali panda twende ndugu yangu". Ndani ya gari (Pajero short chases) alikuwa yeye na jamaa mwingine lakini nyuma kulikuwa na mifuko kama 4 ya unga kilo 20.
Nilikuwa kimya kwenye gari kwa muda kidogo nikiwaza jinsi mama alivyo nihadisia kabla sijaondoka kuhusu kuhusu kumlipia karo mtoto wa dada yangu mmoja ambaye baba yake aliapa kuto kumsaidia, na alikuwa kafaulu shule ya UKATA (kata).
Ghafla jamaa akaniiuliza, huku ndio kwenu? Nikamjibu ndio, unaishi huku? Nikamuambia hapana niko Tanga, oh! Unakwenda Tanga?... Mimi naenda Handeni unaonaje nikikuacha Korogwe?! Nikamuambia haitakuwa vibaya.
Akaiambia itabidi uvumilie maana itakuwa na mazungumzo na watu fulani Lushoto mjini, Soni, na Mombo.
Tulipo fika Magamba akanunua Matunda ghafla ikaja Fuso moja akaitwa na jamaa mmoja "Teacher, teacher" kumbe yule bwana ni mwalimu. Baadae nikawa interested kuumuliza.
Kumbe Bro wewe ni Mwalimu?!
" Mimi ni mwalimu kaka mwaka takribani wa kumi na tisa huu, niko Handeni" Nikaendelea kumdadisi, "mbali na ualimu najishughulisha sana na kilimo na biashara, kwa sasa nalima sana nina hekari kama 1500 na nina mashine za kusaga".
Kumbe jamaa alikuwa anatokea Kwemakame na Mlola kutafuta wateja wa jumlajumla awe ana wauzia unga wa sembe, unao sagwa na mashine zake na offcourse unao tokana na mahindi anayo vuna mwenyewe.
Elli na
zumbemkuu, siku moja niko Korogwe nikamuona tena Teacher tukasalimiana. Kuna jamaa akaniambia "Oyaa unajuana na huyo fogo?!... Jamaa ana vyuma (hela) hapo Handeni huwa anaikopesha mpaka Halmashauri" Nikaona jamaa ananipiga fix tu! Nikajiuliza akopeshe Halmashauri?!
Ukweli ni kwamba jamaa ana vyuma vya kufa mtu!
Kwa maelezo na mifano hiyo michache hapo juu! Nimejifunza kuwa juhudi ndio zinaweza kukutoa! Kuwa na kazi nzuri sio kipimo pekee cha kukutoa kimaisha!
Nani alikuwa na vyuma kama Salimu Matagi?! Nani walikuwa na vyuma kama kina Kusaga?!
Jamaa yangu mmoja, ni mwalimu, ana hekari 15 za michungwa Muheza, kwa wastani kila mwaka anakunja Milioni 10. Life goes on!
Wakati mwingine hata House gal anaweza kutoka kimaisha kuliko baba mwenye nyumba, what matters ni mindset. Hahahaha.