Mpwa wangu nipe list ya walimu wenye mafanikio na ambao wako bado committed na kazi zao....mimi ninachojua na ambacho nina uhakika nacho tena kwa mifano...walime wengi waliofanikiwa ( sio wote nimesema wengi) wao wanafanya biashara na ualimu unabakia kivuli tu...je tufanye hivyo pia? Wakati nasoma Lushoto kulikua na Mwalimu wa shule ya Msingi alikua vizuri sana ila hakua anafundisha kwa siku nzima na wakati mwingine asifike hata shule....alikua ni dealer mzuri sana wa Mbao na Dealer wa Pombe pia....vipindi vyake alikua akiwauzia walimu wengine.....QUOTE]
Mkuu Elli wanachoshindwa kuelewa watu kama hao ni rahisi sana, ukiona mwalimu anajishughulisha na vitu vingine vya kujiongezea kipato fahamu hapo ufanisi darasani sifuri kama sio "F". Ualimu sio kama Udaktari, Uhasibu, Uinjinia, Ufundi mwingine wowote ule ambapo ukitoka ofisini tu kila kitu umekiacha ofisini, changamoto na mengineyo utayakuta kesho tena ukirudi ofisini, Ualimu haupo hivyo ndugu zangu, Ualimu ni popote ukiwa shuleni/darasani unafundisha, ukimaliza kipindi ndiyo muda wa kuandaa andalio la somo au kipindi kingine, kama haitoshi mwalimu huyo huyo anapokuwa nyumbani ndiyo muda mwafaka wa kuandaa somo la kesho yake pamoja na andalio la somo.
Sasa unaposema mwalimu avumilie kuishi kwenye mazingira magumu yasiyokuwa hata na umeme unategemea hilo somo litaandaliwa saa ngapi eti mtu anajaribu kulinganisha Mwalimu na Mtumishi mwingine, hilo ni kosa. Mwalimu anaingia darasani pasipo kujiandaa vya kutosha kutokana na mazingira duni anayoishi, unategemea nini hapo kama sio wale 60%. Walimu waliopo makazini wamevunjika mioyo, jamii inawadhararu hata makonda tunawasikia mabararani wakikashifu magari fulani kuwa haya si ya walimu, serikali nayo ndiyo kabisa.
Mwalimu wa leo aliyejitoa ni yule wa siku nyingi ambaye hana namna tena yupo kwa sababu ndiyo kazi inayompa kuishi yeye na familia yake lakini wale ambao bado umri unaruhusu wengi wao wapo kwenye Ualimu huku wakisubiri target zao nyingine zitiki, sasa unafikiri atakuwa na muda wa ziada wa kumsaidia mtoto wa mtu!
Elimu inashuka na sababu zipo zinaonekana lakini wenye maaamuzi wanajifanya kama hawaoni.
Naheshimu sana walimu kwa maana bila wao mimi leo hii nisingeweza kutanua jijini, nauelewa Ualimu japo si sana kwa kuwa hata mimi baba yangu alikuwa Mwalimu maisha na tuliyokuwa tunaishi najua mimi, alivyonisomesha kwa mbinde mpaka nafika Elimu ya Chuo Kikuu najua mimi.