Ushuhuda: Nilikimbia Ualimu Kuepuka Matatizo

Ushuhuda: Nilikimbia Ualimu Kuepuka Matatizo

Mwalimu Elli HUKUSTAHILI KUWA MWALIMU NIPE MAANA YA NENO "KWENE"Kiukweli wewe ni mwl wa gred A Uliyepata 4 ya 28 tena kwa KUBAHATISHA.
 
Wakuu Elli na zumbemkuu.

Nawauzieni siri! Kazi nzuri niya mwenzako, na jitihada zako ndio zitakutoa.

Uzuri wote Elli na zumbemkuu) kwa kuwa mnatokea Lushoto mtakuwa mna mfahamu vizuri Mwalimu Soka, mwalimu Soka alikuwa anakaa Chakechake akifundisha Kitopeni mimi nikiwa bwana mdogo (Chabebi) nikisoma Hazina (Lushoto Primary kwa sasa). Nilisoma tuition kwake, alikuwa anachacharika kwenye kila aina ya kitu kinachoita kuingiza pesa! Leo Mwl Soka yuko kwenye mitumba kesho yuko kwenye Mbao, leo amefungua Glossary anauza bia, mara kesho amekuwa wakala wa bia wilaya ya Lushoto, mara anafuga yale madubwana ambayo nikiyaona lazima nipige Astakafuli! Mara anakusanya mahindi na kuuza. Yaani alikuwa na jitihada na vurugu za kutafuta! Alithubutu!

Leo mwalimu Soka ni miongoni mwa matajiri wakubwa pale Lushoto! Kwa taarifa yenu nilikutana naye miaka kama 3 iliyopita bado alikuwa anapigisha chaki kama kawaida! Kumbukeni, hakuwa akifundisha sekondari na wala hakuwa na elimu kubwa ya kiwango cha shahada kama chenu Elli na zumbemkuu).

Mwingine yuko Handeni maarufu sana kwa jina la TEACHER, nilikutana naye Mkuzi akitokea Kwemakame nilikuwa nasubiria gari hadi Lushoto mjini kisha nikamate zangu Coaster hadi Mkoa (Tanga), nikapiga mkono gari yake akasimama. Akuliza "Ndio kaka nikusaidie nini ndugu yangu"? Nikamuambia "Samahani Bro, naenda Lushoto naomba unisaidie lift nimesubiria gari muda mrefu hapa naona haziji" akaniambia "Usijali panda twende ndugu yangu". Ndani ya gari (Pajero short chases) alikuwa yeye na jamaa mwingine lakini nyuma kulikuwa na mifuko kama 4 ya unga kilo 20.

Nilikuwa kimya kwenye gari kwa muda kidogo nikiwaza jinsi mama alivyo nihadisia kabla sijaondoka kuhusu kuhusu kumlipia karo mtoto wa dada yangu mmoja ambaye baba yake aliapa kuto kumsaidia, na alikuwa kafaulu shule ya UKATA (kata).
Ghafla jamaa akaniiuliza, huku ndio kwenu? Nikamjibu ndio, unaishi huku? Nikamuambia hapana niko Tanga, oh! Unakwenda Tanga?... Mimi naenda Handeni unaonaje nikikuacha Korogwe?! Nikamuambia haitakuwa vibaya.

Akaiambia itabidi uvumilie maana itakuwa na mazungumzo na watu fulani Lushoto mjini, Soni, na Mombo.

Tulipo fika Magamba akanunua Matunda ghafla ikaja Fuso moja akaitwa na jamaa mmoja "Teacher, teacher" kumbe yule bwana ni mwalimu. Baadae nikawa interested kuumuliza.

Kumbe Bro wewe ni Mwalimu?!

" Mimi ni mwalimu kaka mwaka takribani wa kumi na tisa huu, niko Handeni" Nikaendelea kumdadisi, "mbali na ualimu najishughulisha sana na kilimo na biashara, kwa sasa nalima sana nina hekari kama 1500 na nina mashine za kusaga".

Kumbe jamaa alikuwa anatokea Kwemakame na Mlola kutafuta wateja wa jumlajumla awe ana wauzia unga wa sembe, unao sagwa na mashine zake na offcourse unao tokana na mahindi anayo vuna mwenyewe.

Elli na zumbemkuu, siku moja niko Korogwe nikamuona tena Teacher tukasalimiana. Kuna jamaa akaniambia "Oyaa unajuana na huyo fogo?!... Jamaa ana vyuma (hela) hapo Handeni huwa anaikopesha mpaka Halmashauri" Nikaona jamaa ananipiga fix tu! Nikajiuliza akopeshe Halmashauri?!

Ukweli ni kwamba jamaa ana vyuma vya kufa mtu!

Kwa maelezo na mifano hiyo michache hapo juu! Nimejifunza kuwa juhudi ndio zinaweza kukutoa! Kuwa na kazi nzuri sio kipimo pekee cha kukutoa kimaisha!

Nani alikuwa na vyuma kama Salimu Matagi?! Nani walikuwa na vyuma kama kina Kusaga?!

Jamaa yangu mmoja, ni mwalimu, ana hekari 15 za michungwa Muheza, kwa wastani kila mwaka anakunja Milioni 10. Life goes on!

Wakati mwingine hata House gal anaweza kutoka kimaisha kuliko baba mwenye nyumba, what matters ni mindset. Hahahaha.

kama unafuata sheria za kufundisha huwezi toka kama unavyotaka tuamini
 
Last edited by a moderator:
Ni kweli kabisa Mpwa wangu unachosema, sasa kama umeshanihukumu hata nikikupa manaa yake itasaidia kitu?
Mwalimu Elli HUKUSTAHILI KUWA MWALIMU NIPE MAANA YA NENO "KWENE"Kiukweli wewe ni mwl wa gred A Uliyepata 4 ya 28 tena kwa KUBAHATISHA.
 
Hahahahah mpwangu Elli upo wapi siku hizi?
 
Last edited by a moderator:
Mpwa niko mtaani ni mjasiliamali tu ila sikwepi kodi

Mbona umejisalimisha haraka kwamba hukwepi kodi.?....nina wasiwasi utakuwa mmoja wa wenye contena....lol
 
Hahahahah sawa mpwa wacha si tukomae na ma TGS tuuu

Ooogghhh niliogopa maana sikua naelewa hata hizo TGS ila nilianza na salary ya laki mbili na kidogo, na ka Bachelor kangu!
 
Mkuu Elli umeitafunia Tume ya Pinda kila kitu bado kumeza tu, wakitaka wameze wasipotaka wafanye kama hawaoni.

Ulichofanya wewe hapo mwishoni, ndicho walimu wengi walichofanya na wanachoendelea kufanya sasa hivi kimya kimya. Asiyeamini aende vyuo vya elimu ya juu ataone ni wanavyuo wangapi wenye fani za Ualimu wanachukua fani nyinginezo kama Marketing, BBA, IT/Comp. Eng./Science, Law, Human Resource/Industrial Relation, Uhasibu (CPA) n.k.
Hata kwenye nyadhifa za juu za uongozi nchi hii wamejaa walimu, bungeni wamejaa walimu. Jiulize kwanini wamekimbia fani zao.

Walimu wamechoka kudhalilishwa jamani tena unakuta anadhalilishwa na kajitu kenye cheti tu maskini kalichopo kaunta labda ya Halmashauri, wizarani, benki nk. wakati mwalimu kamaElli ana Bachelor yake.

Naelewa Serikali imelala katika kujali walimu lakini itakapofungua macho itakuja kuta ualimu ni sehemu ya vijana wetu kupitia kwenda kwenye mafanikio tu.

Ukweli ndo huo ualimu ni uchochoro tu wa kupita kwenda kwenye mafanikio kwa kijana wa kimaskini wa kTz
 
Bac siendi kusoma degree ya ualimu
 
Bora tuandae taifa la vibaka na wabakaji kuliko kuandaa taifa nyonge lenye watu waoga na wanafiki kama taifa letu. Jana nilimsikiliza Rais aliyetokana na Chama Cha Magamba (inasemwa eti hata mimi ni Rais wangu...) lakini kusema ukweli sikumuelewa. Alitumia muda mwingi kuudanganya Umma eti serikali yake haitathubutu kuwalipa watumishi wa Umma, wapatao laki tano hivi, kwa kutumia mapato ya nchi zaidi ya asilimia 80. Lakini alisahau kuwaambia ukweli wa mafisadi wachache tu nchi hii wanaomiliki ukwasi kuliko mali zote za serikali. Kusema kwamba serikali yake haitawalipa walimu ni sawa na kusema, liwalo na liwe! Si anajua watoto, wajukuu, wake, wakwamwana, mashemeji, vipusa...... wote wanasoma nje ya nchi? Na wale wanaosoma nchini sana sana watakuwa wanasoma Feza Schools ambako karo yake ni shilingi milioni saba kwa mwaka kwa mtoto wa chekechea. Kwa hiyo walimu wafundishe wasifundishe hilo ni shauri lenu maskini wakubwa!!! Hayo ndiyo niliyoyasoma akilini mwa mkubwa yule aliyekuwa anauma na kupuliza pale mbele ya wahariri wa vyombo vya habari!

kuna kauli moja aliitoa kuhusu shutuma kwa wanae hasa yule mkubwa, nilishangaa Sana.
 
Ooogghhh niliogopa maana sikua naelewa hata hizo TGS ila nilianza na salary ya laki mbili na kidogo, na ka Bachelor kangu!
kuna mwalimu ame proposal hapa kwa post hii bado nafikiria
 
Back
Top Bottom