Ushuhuda: Nilikimbia Ualimu Kuepuka Matatizo

Tumekusanyika wote, tumependeza kweli, ni kozi mbalimbali na tumetengwa vivyo hivyo!! Mimi nahitimu kozi ya Elimu ya Watu wazima (Bachelor of Education in Adult Education) ni furaha kweli. Ila kuna kitu kinaniumiza sana kila nikikumbuka shule niliyopangiwa.

Kweli hii si shule bali ni majengo tu, hayana madirisha mazuri, sakafu chafu, imetoboka toboka! Nashindwa kufundisha kutoka na vumbi lile, ubao wa kufundishia haueleweki, ofisini sina hata rula, inabidi nijinunulie kalamu! Lakini mbaya zaidi ni hawa wafuatao; wanafunzi wawili wenye ulemavu wa viungo, inabidi wakae chini pale mbele maana hawawezi kukaa kwene madawati na pia baskeli zao hazipiti kwene milango ya madarasa. La pili, wanafunzi wangu wanaonekana kukata tamaa ya maisha kabisa na kila ninavyojaribu kuwaelimisha hawaonekani kabisa kunielewa. Wanauliza maswali magumu kuliko uwezo wa kuyajibu, hawana maabara hata moja, kuna gunia moja na box ambalo tumehifadhia mifano ya test tube, spatula na n.k

Walimu wenzangu nao wanaonekana wamefika mwisho wa maisha yao, ni walevi wa kutupwa (si walaumu) na nguo zao zinaonyesha fadhaiko kubwa na kukata tamaa kwa hali ya juu, ni kilio kikubwa. Niko kwene nyumba ya kupanga, naonekana kama ndio mungu wao, mwenyewe nimepigika!

Siku moja niakenda Halmashauri kufuatilia madai yangu, nilichokikuta ilikua ni pigo jingine, kauli za wahasibu wale zilinikatisha tamaa sana sana, ni kauli zilizojaa jeuri na kiburi, mbaya zaidi namuona kijana mmoja ambae tulimaliza mwaka mmoja kwa kozi tofauti (Accounts) ni mmoja wa wahasibu/cashier wa pale, yeye anapendeza jamani si haba hakuna ulinganisho wa mimi na yeye kwa namna yoyote ile. Naelekea kwene ofisi za TSD huko nako nakuta kituko majibu ya hovyo sana, roho inauma sana.

Ninaporudi jioni nimechoka sana maana hata basi la kurudia kwangu nililikosa na hivyo kupanda Landrover, nimejaa vumbi sana, nimechoka na kesho natakiwa tena niwepo darasani nifundishe wanafunzi wangu!!! Usiku ule unakuwa usiku wa maumivu makali sana kwangu, nikijiuliza kuwa kwanini nilifanya chaguo baya? Maana nilifaulu kwa kiwango cha Division One point Seven kwa form six.

Asubuhi naamua kuongea na wanafunzi wangu badala ya kufundisha tu kila siku, tunabadilishana mawazo, maana si mwalimu wala si wanafunzi wanaoneka wana ari ya kusoma tena!!!!! Nawauliza, ni wapi alipo Asha Amiri? wanacheka na mmoja anasimama na kuongea kwa kejeli, "ameshaolewa, yaani mwalimu huna habari?"

Ni jioni sasa, nipo nje pale nyumbani, wanakijiji wanaendelea na shughuli zao, huyu anachota maji hawa wanarudi machungani, nina kiredio kidogo nasikiliza nisichokielewa! Maana hakika mawazo yangu yako mbali sana, ile degree haina maana tena, sina wa kumfundish maarifa yale! Naonekana kituko pale kijijini kwa kutaka kuwafundisha watoto wale!!! Ghafla, napata ujasiri wa ajabu, yes ujasiri wa ajabu sana. NIMEAMUA KUACHA KAZI. Kesho ni ijumaa kwahio nitaomba neinde mjini mara moja lakini hapo ndipo mwisho wa kukaa hapa.

Narudi mjini na kuamua kaunza maisha ya tofauti sana na kujaribu kuisahau ndoto ile kwamba ningekuwa Mwalimu mzuri, nimeachana na vituko vya kukatwa pesa ya MWENGE kwa ajili ya kufungua miradi ya watu binafsi, nimeachana na maumivu yale ya kudharauliwa na watumishi wenzangu walioko halmashauri, sijawahi pia kukaa nikafahamu mshahara wangu ni shilingi ngapi hasa, maana kila siku unabadilika kwene payslip.

Walimu wana haki sawa na watumishi wengine, tuwapende, tuwajali na tuwatunze!!!

Mwalimu Elli

Pole sana. Ulichukua uamuzi wa maumivu. Sikulaumu kwa lolote. Kila mmoja atabeba mzigo wake. Sawa nami nina watoto wanahitaji kufundishwa, lakini lazima na mwalimu ale, avae, alale pazuri etc. kama havipo afanyeje! Hao wanasiasa watoto wao hakuna anayekwenda ualimu. UAMUZI SAHIHI
 
Asante Mpwa, niliumia sana mwanzoni niliteseka na kutengwa na baadhi ya wana familia kuwa nimeacha kazi, lakini ninavyoongea hivi leo, nashukuru MUNGU ninaweza kuwasaidia pia, maana kwa salary ya ualimu na mimi ningeishia kuomba omba!!!

Jamani hii kazi ni ya kujitolea pia unasaidia wa Tz wenzako na unapata swawabu.Ukiacha kaz unaandaa taifa la wajinga,makahaba na vibaka ambao haohao watakukaba wewe au nduguyo ata kwetu TANGA kuna shida tele za elimu ndio mana vijana wanakuwa wanganga

Bora tuandae taifa la vibaka na wabakaji kuliko kuandaa taifa nyonge lenye watu waoga na wanafiki kama taifa letu. Jana nilimsikiliza Rais aliyetokana na Chama Cha Magamba (inasemwa eti hata mimi ni Rais wangu...) lakini kusema ukweli sikumuelewa. Alitumia muda mwingi kuudanganya Umma eti serikali yake haitathubutu kuwalipa watumishi wa Umma, wapatao laki tano hivi, kwa kutumia mapato ya nchi zaidi ya asilimia 80. Lakini alisahau kuwaambia ukweli wa mafisadi wachache tu nchi hii wanaomiliki ukwasi kuliko mali zote za serikali. Kusema kwamba serikali yake haitawalipa walimu ni sawa na kusema, liwalo na liwe! Si anajua watoto, wajukuu, wake, wakwamwana, mashemeji, vipusa...... wote wanasoma nje ya nchi? Na wale wanaosoma nchini sana sana watakuwa wanasoma Feza Schools ambako karo yake ni shilingi milioni saba kwa mwaka kwa mtoto wa chekechea. Kwa hiyo walimu wafundishe wasifundishe hilo ni shauri lenu maskini wakubwa!!! Hayo ndiyo niliyoyasoma akilini mwa mkubwa yule aliyekuwa anauma na kupuliza pale mbele ya wahariri wa vyombo vya habari!
 
Mpwa umesema ukweli kabisa

Siyo siri inasikitisha, ninao wadogo zangu (dada zangu wawili) ni walimu nikiangalia maisha yao yalivyo najiuliza, "hivi kama isigekuwa kazi za waume zao, hawa wadogo zangu wangekuwa na hali gani?", Inasikitisha siyo siri!!!!!
 
sasa imagine inakluaje kwa mwanaume? hali ni mbaya sana halafu umeoa labda mwanamke hana kazi
Siyo siri inasikitisha, ninao wadogo zangu (dada zangu wawili) ni walimu nikiangalia maisha yao yalivyo najiuliza, "hivi kama isigekuwa kazi za waume zao, hawa wadogo zangu wangekuwa na hali gani?", Inasikitisha siyo siri!!!!!
 
Tumekusanyika wote, tumependeza kweli, ni kozi mbalimbali na tumetengwa vivyo hivyo!! Mimi nahitimu kozi ya Elimu ya Watu wazima (Bachelor of Education in Adult Education) ni furaha kweli. Ila kuna kitu kinaniumiza sana kila nikikumbuka shule niliyopangiwa.

Kweli hii si shule bali ni majengo tu, hayana madirisha mazuri, sakafu chafu, imetoboka toboka! Nashindwa kufundisha kutoka na vumbi lile, ubao wa kufundishia haueleweki, ofisini sina hata rula, inabidi nijinunulie kalamu! Lakini mbaya zaidi ni hawa wafuatao; wanafunzi wawili wenye ulemavu wa viungo, inabidi wakae chini pale mbele maana hawawezi kukaa kwene madawati na pia baskeli zao hazipiti kwene milango ya madarasa. La pili, wanafunzi wangu wanaonekana kukata tamaa ya maisha kabisa na kila ninavyojaribu kuwaelimisha hawaonekani kabisa kunielewa. Wanauliza maswali magumu kuliko uwezo wa kuyajibu, hawana maabara hata moja, kuna gunia moja na box ambalo tumehifadhia mifano ya test tube, spatula na n.k

Walimu wenzangu nao wanaonekana wamefika mwisho wa maisha yao, ni walevi wa kutupwa (si walaumu) na nguo zao zinaonyesha fadhaiko kubwa na kukata tamaa kwa hali ya juu, ni kilio kikubwa. Niko kwene nyumba ya kupanga, naonekana kama ndio mungu wao, mwenyewe nimepigika!

Siku moja niakenda Halmashauri kufuatilia madai yangu, nilichokikuta ilikua ni pigo jingine, kauli za wahasibu wale zilinikatisha tamaa sana sana, ni kauli zilizojaa jeuri na kiburi, mbaya zaidi namuona kijana mmoja ambae tulimaliza mwaka mmoja kwa kozi tofauti (Accounts) ni mmoja wa wahasibu/cashier wa pale, yeye anapendeza jamani si haba hakuna ulinganisho wa mimi na yeye kwa namna yoyote ile. Naelekea kwene ofisi za TSD huko nako nakuta kituko majibu ya hovyo sana, roho inauma sana.

Ninaporudi jioni nimechoka sana maana hata basi la kurudia kwangu nililikosa na hivyo kupanda Landrover, nimejaa vumbi sana, nimechoka na kesho natakiwa tena niwepo darasani nifundishe wanafunzi wangu!!! Usiku ule unakuwa usiku wa maumivu makali sana kwangu, nikijiuliza kuwa kwanini nilifanya chaguo baya? Maana nilifaulu kwa kiwango cha Division One point Seven kwa form six.

Asubuhi naamua kuongea na wanafunzi wangu badala ya kufundisha tu kila siku, tunabadilishana mawazo, maana si mwalimu wala si wanafunzi wanaoneka wana ari ya kusoma tena!!!!! Nawauliza, ni wapi alipo Asha Amiri? wanacheka na mmoja anasimama na kuongea kwa kejeli, "ameshaolewa, yaani mwalimu huna habari?"

Ni jioni sasa, nipo nje pale nyumbani, wanakijiji wanaendelea na shughuli zao, huyu anachota maji hawa wanarudi machungani, nina kiredio kidogo nasikiliza nisichokielewa! Maana hakika mawazo yangu yako mbali sana, ile degree haina maana tena, sina wa kumfundish maarifa yale! Naonekana kituko pale kijijini kwa kutaka kuwafundisha watoto wale!!! Ghafla, napata ujasiri wa ajabu, yes ujasiri wa ajabu sana. NIMEAMUA KUACHA KAZI. Kesho ni ijumaa kwahio nitaomba neinde mjini mara moja lakini hapo ndipo mwisho wa kukaa hapa.

Narudi mjini na kuamua kaunza maisha ya tofauti sana na kujaribu kuisahau ndoto ile kwamba ningekuwa Mwalimu mzuri, nimeachana na vituko vya kukatwa pesa ya MWENGE kwa ajili ya kufungua miradi ya watu binafsi, nimeachana na maumivu yale ya kudharauliwa na watumishi wenzangu walioko halmashauri, sijawahi pia kukaa nikafahamu mshahara wangu ni shilingi ngapi hasa, maana kila siku unabadilika kwene payslip.

Walimu wana haki sawa na watumishi wengine, tuwapende, tuwajali na tuwatunze!!!

Mwalimu Elli
bro pole sana!! teachin ni kazi ngum hasa kwa hili linchi letu!! mi binafsi ningekushaur kama una weza ni bora uchek mishe nyingine kama biashara au kama unaweza rudi chuo ukachukua master au degree ya kitu kingine!!! pole sana na hayo ndo maisha ya hapa bongoland!
 
Mpwa nilishakimbia huko muda tu hebu soma mistari ya mwisho hapo
bro pole sana!! teachin ni kazi ngum hasa kwa hili linchi letu!! mi binafsi ningekushaur kama una weza ni bora uchek mishe nyingine kama biashara au kama unaweza rudi chuo ukachukua master au degree ya kitu kingine!!! pole sana na hayo ndo maisha ya hapa bongoland!
 
Hongera kwa kufanya maamuzi sahihi, ungezeeka kabla ya umri wako
 
asante kwa pongezi ila there is so much to be done urgently otherwise, hilo kundi linalipoanda huko chini litakua hatari sana kwa usalama wa Taifa
Hongera kwa kufanya maamuzi sahihi, ungezeeka kabla ya umri wako
 
kaka poa, ulichoamua ni sahihi lakini ni wachache wenye maono kama yako, na wengi ni waoga wa kufanya maamuzi magumu..
 
Asante Mpwa, niliumia sana mwanzoni niliteseka na kutengwa na baadhi ya wana familia kuwa nimeacha kazi, lakini ninavyoongea hivi leo, nashukuru MUNGU ninaweza kuwasaidia pia, maana kwa salary ya ualimu na mimi ningeishia kuomba omba!!!

Hapo ndio shida ilipo...
Familia hazituelewi na kuonekana unachagua kazi
Anaejua ugumu au uzuri wa kazi ni alieifanya sio anaekutegemea.
Hongera kwa uamuzi wa kijasiri
 
yea yeah uko sahihi kabisa
 
Mpwa wangu MANI, Paloma zumbemkuu saudari na wengineo wengi....hivi ndivyo Mpwa wenu alivyoukimbia ualimu kwa uamuzi wa maumivu....mgumu kuliko, bado naupenda sana ualimu lakini si ktaika mazingira ya kujitesa.....

Pole sana mpwaa.
Kwa sasa unajishughulisha na nini? Au bado unaendelea na ualimu?
 
Hahahahaha animefungua kijiwe changu cha Gahawa pale kwa Mtogole Mpwa una visa wewe...mengine tutaongea nje ya jukwaaa bhana naogopa mtakuja kunikopa
 
Pole sana mpwaa.
Kwa sasa unajishughulisha na nini? Au bado unaendelea na ualimu?

Mpwa Elli anasema hataki kufundisha watoto ambao hawako tayari kusoma kutokana na sababu kadhaa wa kadhaa haswa vitendea kazi !
 
Last edited by a moderator:
Mpwa huo ndio ukweli bhana, yaani unawaonea huruma maana inafikia kipindi wewe Mwalimu unapata taaabu kubwa kweli kuelezea jambo na watoto wenyewe hawajala kitu wanaumwa njaaa, shule haitoi hata maji ilifikia kipindi hata vyoo vya shule havitumiki tena (serious)
Mpwa Elli anasema hataki kufundisha watoto ambao hawako tayari kusoma kutokana na sababu kadhaa wa kadhaa haswa vitendea kazi !
 
Masaibu ya walimu na hatima ya elimu ya Tanzania

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom