Ushuhuda na pongezi kwa mifumo ya TAUSI na e-ARDHI

Lyetu

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2018
Posts
1,333
Reaction score
3,541
Habari za wakati huu wapendwa katika Bwana,

Nichukue nafasi hii kutoa pongezi kwa hii mifumo miwili ambayo imerahisisha sana ununuzi wa Ardhi na kuwasilisha maombi ya Hati bila usumbufu.

Nilinunua kiwanja TAUSI portal ambapo taratibu zake ni rahisi na rafiki sana, na baada ya kumaliza kulipia malipo ya kiwanja niliomba HATI kupitia mfumo wa e-ardhi ambao pia ni rafiki sana kwa gharama ya Tsh 54,000. Ndani ya mwezi mmoja tayari nimepata HATI.

Nilinunua kwa kujaribu tu nikiwa tayari kupoteza hiyo pesa, ila sasa nikutoe hofu, yeyote uliyekuwa unawasiwasi na hii mifumo, inafanya kazi vizuri sana.
 
hongera sana.
Nisaidie please. Nina kiwanja changu cha siku nyingi. Hakijapimwa ie survey plan haipo. naweza kutumia mfumo huu kupata hati?
 
1756306771609.png

Hii ni orodha ya baadhi ya huduma zinazotolewa, nadhani unaweza kuomba kupimiwa kiwanja chako kisha ukaendelea na maombi ya Hati
 
Habari za wakati huu wapendwa katika Bwana,

Nichukue nafasi hii kutoa pongezi kwa hii mifumo miwili ambayo imerahisisha sana ununuzi wa Ardhi na kuwasilisha maombi ya Hati bila usumbufu.

Nilinunua kiwanja TAUSI portal ambapo taratibu zake ni rahisi na rafiki sana, na baada ya kumaliza kulipia malipo ya kiwanja niliomba HATI kupitia mfumo wa e-ardhi ambao pia ni rafiki sana kwa gharama ya Tsh 54,000. Ndani ya mwezi mmoja tayari nimepata HATI.

Nilinunua kwa kujaribu tu nikiwa tayari kupoteza hiyo pesa, ila sasa nikutoe hofu, yeyote uliyekuwa unawasiwasi na hii mifumo, inafanya kazi vizuri sana.
Nisaidie procedures za kupata hata, nilishalipia kiwanja kupitia mfumo wa tausi. Akaunti ya e ardhi ninayo.
 
Tatizo hawaweki bei ya viwanja, siku ya kuuza viwanja nayo haijulikani..

Marekebisho yanahitajika sana kwenye mfumo..
 
Kwenye account yako ya e-ardhi bonyeza sehemu iliyoandikwa Anzisha ombi

Kisha chagua Maombi ya Hatimiliki, kisha chagua Endelea

Baada ya hapo utajaza taarifa kama Mkoa ulikonunua kiwanja, wilaya, Halmashauri, kisha bonyeza WASILISHA

Baada ya hapo utajaza taarifa za wahusika (taarifa zako muombaji) kwa kubonyeza Weka wahusika.

Baada hapo utaombwa kujaza taarifa za kiwanja

Utaombwa nyaraka, hapa utaweka nakala ya kitambulisho kwenye kipengele cha Proof of Citizenship, Utaweka invoice ya kiwanja kutoka Tausi kwenye kipengele cha Sales Agreement, utaweka invoice ya kiwanja kwenye kipengele cha neighbors Consent, utaweka risiti za malipo kutoka Tausi kwenye kipengele cha Proof of payment.

Kama taarifa ulizojaza zitakuwa sahihi utapewa control number ya kulipia gharama za ombi Tsh 5000, kisha utapewa control number ya gharama za kuandaa Hati.

Ukishalipia utakuwa unatrack kwenye mfumo ombi lako limefika hatua gani, na ni ofisi gani inashughulikia hiyo hatua, ni Halmashauri au ofisi ya ardhi ya mkoa.

Ombi likikamilika, litakuwa na status ya Completed na utapata sms ya kwenda kuchukua Hati yako kwa kamishna wa ardhi mkoa husika.
 
Tatizo hawaweki bei ya viwanja, siku ya kuuza viwanja nayo haijulikani..

Marekebisho yanahitajika sana kwenye mfumo..
Mkuu viwanja vilivyopo kwenye mfumo wa tausi vyote vina bei na viko tayari kwa kuuzwa . Ni wewe tu
 
Tatizo hawaweki bei ya viwanja, siku ya kuuza viwanja nayo haijulikani..

Marekebisho yanahitajika sana kwenye mfumo..
Viwanja vyote vina bei, kama umeingia kwa kutumia simu rotate simu yako, kisha bonyeza kiwanja chochote.

Kwa kufanya hivyo utapata taarifa kama ukubwa wa kiwanja, bei, matumizi ya kiwanja na gharama za kiwanja husika.

NB, Viwanja vyenye rangi nyekundu vimeshanunuliwa na vyenye rangi ya kijana havijanunuliwa.
 
mtzedi , OK mkuu ngoja nijaribu.. Maana nimeona location ya wivanja Nimeipenda sana.
 
Kwa msada zaidi kuview eneo ambako vipo viwanja kama hupajui/ hujawahi kufika, tumia google map au google earth.

Viwanja vya TAUSI vipo kwenye ramani ila sio satellite view, so wewe unaweza kutafuta hiyo location kwenye Google earth/ Google map kupaangalia vizuri kwa satellite view. Labda Kuna mabonde ya maji au miinuko, kupima umbali labda kutoka katikati ya mji, kama kuna huduma za kijamii kama hospital n.k
 
Nimeona mkuu, but hiyo sehemu naona ni kwa ajili ya ujenzi wa viwanda tu.

Ivi unaweza kununua Sasa hivi Alafu baada ya mda Fulani nakipiga bei kwa mtu mwingine??
 
Habari za wakati huu wapendwa katika Bwana,

Nichukue nafasi hii kutoa pongezi kwa hii mifumo miwili ambayo imerahisisha sana ununuzi wa Ardhi na kuwasilisha maombi ya Hati bila usumbufu.

Nilinunua kiwanja TAUSI portal ambapo taratibu zake ni rahisi na rafiki sana, na baada ya kumaliza kulipia malipo ya kiwanja niliomba HATI kupitia mfumo wa e-ardhi ambao pia ni rafiki sana kwa gharama ya Tsh 54,000. Ndani ya mwezi mmoja tayari nimepata HATI.

Nilinunua kwa kujaribu tu nikiwa tayari kupoteza hiyo pesa, ila sasa nikutoe hofu, yeyote uliyekuwa unawasiwasi na hii mifumo, inafanya kazi vizuri sana.
Thibiitisha ukweli wa na uhalisia wa taarifa yako!Kama ni hivyo mbona hautumiki kuepuka kero za hii mambo za kufuatilia hati za ardhi ama kufanya manunuzi?
 
Nimeona mkuu, but hiyo sehemu naona ni kwa ajili ya ujenzi wa viwanda tu.

Ivi unaweza kununua Sasa hivi Alafu baada ya mda Fulani nakipiga bei kwa mtu mwingine??
Nadhani inawezekana mkuu, sijaona masharti yoyote yanayonizuia kununua kiwanja kwajili ya matumizi ya viwanda
 
Thibiitisha ukweli wa na uhalisia wa taarifa yako!Kama ni hivyo mbona hautumiki kuepuka kero za hii mambo za kufuatilia hati za ardhi ama kufanya manunuzi?
Ni mfumo mpya, so unadeal na maombi mapya.na haya maombi yanapita kwa idara tofauti tofauti ili kuondoa ujanja ujanja wa maafisa.

Mfano onapoanzisha ombi linaanzia halmashauri, pale afisa ardhi analifanyia kazi anatuma kwa mkubwa wake nae anapitia nyaraka kisha analituma ofisi ya kamishna.

Ofisi ya kamishna wanapitia ombi kwa kukagua nyaraka na kumtumia Kamishna, nae anakagua nyaraka anatoa approval na kulituma kwa msajili wa Hati, msajili nae atapitia nyaraka kisha atatuma kwa mtu wa mwisho anaeprint Hati, huyu nae atakagua nyaraka kabla hajaprint na kukabidhi Hati.

so ukiangalia ni zoezi ambalo linajumuisha watu wengi si rahisi kutengeneza hati mbili kwa mtu mmoja kama ilivyokuwa hapo awali au kulete janja janja.
1756310947968.png

Hili ni ombi langu, ukiangalia hapo juu kwenye Jaza na wasilisha maombi lina mwezi mmoja tu, na status inasoma COMPLETED na muda uliotumika kwa kila Hatua ya ombi
1756311070933.png
 
View attachment 3455230

Hili ni ombi langu, ukiangalia hapo juu kwenye Jaza na wasilisha maombi lina mwezi mmoja tu, na status inasoma COMPLETED na muda uliotumika kwa kila Hatua ya ombi
View attachment 3455231
Nitajaribu kuona ufanisi wake.
 
Back
Top Bottom