USHUHUDA: Kuku wa kienyeji (Pure) - Biashara kichaa isiyo na tija

We mdada na wewe unaweza kufuga!!!? Mimi nadhani wewe ni wale wanaovaa viatu virefu na jeans huku wakiwa na kucha za kubandikiza. Karibu kwenye ujasiriamali.
Looh hisia zako zinakudanganya jamani.... Santeee ntakaribia muda si mrefu
 
kuku wa kienyeji wanalipa ikiwa utapata chakula cha kutosha kutengeza viini ili viwe vinawapa hali ya kuihitaji kutaga, kuku hawa inabidi kwanza uwachanganye na kuku wa kienyeji wa malawi, alafu akianza kutaga, jaribu kuhesabu mayai mara nyingi hutaga kumi na mbili hadi 14, chunga sauti yake akianza sauti ya kulalia, ukimukuta unamchukua unamwogesha na sabuni ya homo siku mbili , anapoteza ile joto iliyotayarishwa kwa ajiri ya mayai, baada ya siku tatu huanza utaga tena.
 
Kumekuwa na upotoshaji kwa baadhi wa watu wanaojiita wataalamu wa ujasiriamali, hasa wanaofanya shughuli za ufugaji kwa maandiko ya whatsapp bila kuwa na hata kuku mmoja bandani.

Nimesukumwa kuandika bandiko hili hapa kutokana na jumbe mbali mbali za uufugaji wa kimtandao unaoshawishi vijana kuwa watatajirika mapema kwa shughuli za ufugaji kwa kuanza na kuku wa kienyeji kumi na moja na kuweza kupata Zaidi ya kuku miatatu ndani ya kipindi cha mwaka mmoja wa uzalishaji. Hoja yao inaweza kuwa sahihi, ila ningependa kusisitiza mafanikio katika ufugaji hayapo katika idadi ya kuku unayomiki, bali ni namna ulivyoweza kumanage biashara ya ufugaji.

Hoja yangu leo hapa ni kwamba, Biashara ya kuku wa kienyeji hailipi na nikupoteza muda wako. Na nitatetea hoja yangu kwa mifano hai na uzoefu wangu katika ufugaji.

Biashara ya Mayai. (idadi isiyo na tija kibiashara)

Kwa asili ya kuku wa kienyeji,huwa wanatabia ya utagaji wa mayai 7-10 na mara nyingi ni siku kwa siku 10 mfululizo, utamiaji -siku 21, na uleaji wa vifaranga - siku 50-60. Hii inampelekea kwa kuku mmoja kuweza kutaga wastani wa mayai 35-50 kwa mwaka kwani anapoteza muda mwingi kwa shughuli za utamiaji na malezi ya vifaranga badala ya kutaga. Idadi hii ya mayai haina tija kibiashara kwani kuku mmoja anaweza kukuzalishia tray 1 mpka mbili kasoro pekee kwa mwaka ambayo kwa bei ya soko si Zaidi ya shilingi za kitanzania 20,000 tu kwa mwaka.

Changamoto kwenye soko la mayai ya kienyeji. (Uhifadhi wa mayai)

Mayai ya kienyeji ni kati ya bidhaa ngumu Zaidi kuhifadhika. Ikumbukwe kuwa tofauti na mayai ya kisasa, mayai ya kienyeji huwa yamerutubishwa na majogoo. Hivyo kuharibika ndani ya muda ya week moja au pungufu kama hayatatuzwa katika mazingira salama kwaajili ya utunzaji. Kipindi cha joto kali, mayai haya huanza kujitenenezea kifaranga au mishipa ya damu ambayo baada ya muda mfupi hugeuka viza na kutofaa kwa matumizi tena.

Kwa uzoefu wangu binafsi, nilianza kusambaza mayai ya kienyeji kwenye supermarkets miaka mitatu iliyopita. Nilipata changamoto kubwa sana ya kubadilisha mayai mara kwa mara kwani mteja akichukua yai viza ni kumpoteza kabisa. Hii ni changamoto ya kwanza ambayo mpaka sasa bado inasumbua wafugaji wengi.

Bei juu kwa mayai ya kienyeji

Gharama za mayai husika, bei ya mayai ya kienyeji iko juu ukilinganisha na gharama za mayai ya kuku wa kisasa. Soko kubwa la mayai ni pamoja na vibanda vya chips, migahawa na hoteli. hawa wanauhitaji mkubwa sana wa mayai na soko liko juu muda wote wa mwaka.

Soko la mayai ya kienyeji lipo Zaidi kwenye households(soko la familia) hasa kwa vigezo vya kuzingatia afya zaidi. Soko hili la familia sio kubwa, ni soko dogo na mara nyingi hutumia tray moja kwa kipindi cha wiki mbili au Zaidi. Kwa mzalishaji mkubwa wa mayai ya kienyeji ni lazma awe na soko la familia pana Zaidi kuweza kupata faida ndogo, nasema faida ndogo maana ili kuzalisha mayai tray kumi (mayai 300) kwa siku, utahitaji Zaidi ya matetea 700 mpaka 1000 ya kienyeji pure. idadi ambayo ni kubwa kuliko idadi ya mayai yanayopatikana.

Biashara ya Nyama

Na declare interest, mimi pia ni msambazaji wa nyama ya kuku wa kienyeji, hivyo naongea kwa uzoefu, na niko tayari kukosolewa. Pamoja na kufugwa katika misingi ya kijani (organic rearing), iyo pekee haitoshi kumpa thamani inayostahili huyu kuku sokoni.

Thamani ya kuku sokoni ni uzito alio nao, organic component ni jambo la ziada lililo muhimu pia. tunavyo jadili bei ya soko ya kuku huyu ni lazma tumliganishe na gharama za bidhaa pinzani zilizoko sokoni. Haitawezekana kumuuza kuku mwenye kilo moja au pungufu kwa bei ambayo tunashawishiana humu ya 15,000-20,000 wakati bidhaa pinzani (nyama nyeupe) kama samaki sato toka mwanza wanauzwakwa 7,500 kwa kilo, au kitimoto, nyama ya ngombe ambazo nazo kilo ni 7,500-8,000.

Hivyo basi, hoja yangu hapa ni uzito wa kuku husika. Ukiachana na jamii chache za kuku wa kienyeji (kuchi etc) wenye uzito mzuri, majority ya kuku pure wa asili/kienyeji kwa majogoo huwa na pungufu ya kilo moja na nusu. Kumbuka uzito wa kuku hawa sio kwasababu ya malisho duni, laah hasha, bali ni kutokana na vinasaba (genes) vyao kuwafanya kuwa na maumbo madogo madogo. kwa kuku wa aina hii, sitegemei mfugaji kama atafanikiwa kuwapeleka sokoni na kuweza kupata bei nzuri toka kwa mlaji wa mwisho.

Nini kifanyike?

Ili ufugaji uwe wenye tija kibiashara ufanyike, ni lazma wafugaji tuamke na kuachana na ufugaji wa kuku hawa asilia kwani hawana tija. Nikisema hivi simaanishi watu waache kufuga, hapana, ila wafuge aina /breeds za kuku zenye tija kibiashara. Kuku pekee unaoweza kuwafuga kwa mbinu za kienyeji na bado wakakuletea mfugaji faida nzuri kibiashara, ni kuku aina ya chotara (cross breeds). Hii ni aina ya kuku wenye sifa zote za ukienyeji kwa misingi ya mbinu zao za kuwafuga pamoja na namna walivyo nauwezo wa kuhimili mazingira hasa ya vijijini.

Kuna aina mbalimbali ya kuku hawa ikiwamo Black/ white australorps, kroiller, Rhodes island red, red hamshire, Sussex etc. Hawa ni kuku ambao wanaserve purpose zote za mayai na za nyama. Mfano kuku aina ya black/white australorps wao wanauwezo wa kutaga mpaka mayai 250 kwa mwaka, tofauti na wa kienyeji, mayai ya kuku hawa huwa makubwa na yenye kasha jeupe na kiini cha njano kama utawafuga kwenye mazingira na mbinu asilia (za kienyeji).

Ukilinganisha uwezo wa utagaji wa kuku hawa utagundua utagaji wao ni Zaidi ya asilimia 500% ukilinganisha na ule wa kienyeji pure. Idadi hii ya mayai toka kwa kuku mmoja kwa mwaka, anaweza kumwezesha mfugaji kuzalisha mayai kwa wingi na kushusha Zaidi bei ya mazao yake (mayai) kuwa chini kuweza kuliteka soko kwa urahisi Zaidi. Kumbuka, bei ya juu ya mayai ya kienyeji ni kwaajili ya kulipia gharama kubwa za utunzaji wa kuku huyu ilihali utagaji wake ni hafifu.

Pili, kuku hawa wana nyama nyingi Zaidi kuliko hawa wa kienyeji kwa majogoo hufikia mpaka uzito wa kilo 3-3.5. huku matetea hufikia kilo 2-2.5 na huwa na nyama nzuri, iliyokomaa vyema na yenye ladha. kwa uzito huu kwa majogoo, kuku hawa uuzwa kwa bei ya 20,000 - 25,000 wakiwa hai. bei ambayoni kwa mujibu wa bei ya soko kwa makadirio ya shilingi 8,000 kwa kilo kwa nyama nyeupe.

Mapungufu

Pamoja na ubora wa kuku hawa katika ufugaji wa kibiashara, kuku hawa pia wanachangamoto mbali mbali ikiwemo kutokuwa na uwezo wa kutamia. Pamoja na hii kuwa changamoto pia ni fursa kwani kwa yeye kutotamia kunamwongezea nafasi ya yeye kuendelea kutaga mara nyingi Zaidi bila kupumzika. Hivyo changamoto hii ni faida kwa mfugaji anaelenga kufuga kwa tija. Kwa vile mayai haya huwa yamerutubishwa na majogoo, nirahisi kwa mfugaji kuongeza idadi ya kuku kwa kupitia kutotolesha kwa mshine za kuangulia vifaranga au kumpa kuku mwingine ayatamie kwa niaba.


Neno la kufungia:


“ I think I touched a raw nerve when I said farming is NOT cool! I believe farming takes a lot of HARD work and dedication. Lets not lie to the youth that they'll become instant millionaires when they get into farming. It becomes "cool" once you master the trade......” caleb

Ufugaji unalipa ukiweza kuibudu biashara ya ufugaji,


Kwa ushauri Zaidi kuhusu shughuli za ufugaji, tuwasiliane kwa namba 0755815174. pia pata fursa kusoma ya Makala mbali na utaalamu kutoka kwenye mtandao wetu www.backyard.co.tz

Nimejaribu kuattach picha za baadhi ya kuku bora wanaofaakufugwa kienyeji na wakaleta tija kibiashara hapa chini. Neno langu si sharia, nakaribisha Michango

View attachment 385750
View attachment 385751
View attachment 385752
View attachment 385753
View attachment 385754
Umenitoa matongo-tongo katika hii industry. Nitakutafuta
 
Nimesoma makala yako kwa undani but mengine si kweli.n imegundua pia unavutia biashara yako pia!
Kwa mfano mm nilianza na kuku 3,majike 2 na dume 1 wa kienyeji.ilikua mwisho wa mwezi wa 12 mwaka jana 2015. But mpaka mwez wa sita mwaka huu nilikuwa nimepata kuku zaid ya 60. Kuku wangu wanataga wastan wa mayai 15-18. Na kila baada ya miezi miwili ni lazima watoto.ninachokifanya vifaranga nilikua nabitunza mwenyewe toka siku ya kwanza kutotolewa .
Kuku wangu wanataga kila baada ya wiki 2 baada ya kutotoa.
Tena nimegundua njia nzuri ya kuku wa kienyeji kutotoa vifaranga kuanzia 20-24. Kwa wakati mmoja na kwa kuku mmoja.
Kuku wa kienyeji wanalipa kama itaamua kukomaa na kufuata maelekezo.
Ufugaji wa kuku wa kienyeji una changamoto zake japo zinaweza tatulika pia.
Mkuu shukrani kwa maelezo mazuri, yanatia Moyo kwa ambao tunataka kuanzisha miradi ya kuku wa Kienyeji. Tunaweza kujifunza mengi kupitia watu kama nyie wenye uzoefu kama wewe na Ginner
 
Kuku wangu mmoja ameanza tena kulalia mayai tena nimempa mayai 23 nategemea atotoe yote. Nitawatumia picha ya namna ya kumwekea mayai kwa beseni la kunawia.
Picha ya kuku alolalia mayai 23.
 

Attachments

  • 1473772610003.jpg
    1473772610003.jpg
    34.6 KB · Views: 315
  • 1473772630265.jpg
    1473772630265.jpg
    50.7 KB · Views: 337
  • 1473772670693.jpg
    1473772670693.jpg
    56.4 KB · Views: 308
Nashukuru kwa kukubali kupokea challenge,
kwa ufupi andiko lako limejaa upotoshaji mkubwa na linalenga kuwakatisha tamaa, wajasiriamali wadogo wadogo ambao wanapendelea kufuga kuku wa kienyeji.
Pia nimegundua mambo makubwa mawili,
1. Bila shaka utakuwa unauza hiyo aina ya kuku amabayo unadai kuwa ni wazuri.
2. Bado hujajua mbinu mbali mbali za ufugaji wenye tija.

Hebu tazama hapa, ulichoandika.

Kwa asili ya kuku wa kienyeji,huwa wanatabia ya utagaji wa mayai 7-10 na mara nyingi ni siku kwa siku 10 mfululizo, utamiaji -siku 21, na uleaji wa vifaranga - siku 50-60. Hii inampelekea kwa kuku mmoja kuweza kutaga wastani wa mayai 35-50 kwa mwaka kwani anapoteza muda mwingi kwa shughuli za utamiaji na malezi ya vifaranga badala ya kutaga. Idadi hii ya mayai haina tija kibiashara kwani kuku mmoja anaweza kukuzalishia tray 1 mpka mbili kasoro pekee kwa mwaka ambayo kwa bei ya soko si Zaidi ya shilingi za kitanzania 20,000 tu kwa mwaka.

kuku wa kienyeji wanataga mayai 15 hadi 20 na sio kwa siku za mfululizo kuna siku nyingine huwa hatagi na hii inatokana na kutokushiba vizuri, nakubali kuhusu muda wa kulea kuwa ni siku 50 hadi 60. unachotakiwa kufanya siku tatu baada ya kuku kutotoa vifaranga, mnyang'anye vifaranga na uviweke mbali nae huko vipatie chakula cha kukuzia stater, maji ya kunywa changanya na glucose, pia weka na chanzo cha joto kama ile mtungi wenye mkaa wa moto ndani yake.
ukifanya hivyo itamchukua kuku huyo uliemnyang'anya vifaranga wiki mbili na kuanza tena utagaji.
kwa mwaka atatoa kati ya mayai 100 hadi 160 kwa uhakika.

Tizama na hapa.

'Mayai ya kienyeji ni kati ya bidhaa ngumu Zaidi kuhifadhika. Ikumbukwe kuwa tofauti na mayai ya kisasa, mayai ya kienyeji huwa yamerutubishwa na majogoo. Hivyo kuharibika ndani ya muda ya week moja au pungufu kama hayatatuzwa katika mazingira salama kwaajili ya utunzaji. Kipindi cha joto kali, mayai haya huanza kujitenenezea kifaranga au mishipa ya damu ambayo baada ya muda mfupi hugeuka viza na kutofaa kwa matumizi tena.

uhifadhi wa mayai ya kienyeji sio mgumu, yanakaa bila ya kuharibika kwa muda wa mwezi mmoja, unachotakiwa kufanya, hifadhi mayai yako ktk trey ya mayai, pia chunguza kama yai lina ufa hilo usilihifadhi litumie kwa kula mwenyewe na familia, pia weka mayai yako sehemu ya wazi ambayo ina mwangaza wa kutosha, kuyaweka mayai sehemu isiyo na mwangaza kutapelekea mayai kuanza kutunga kifaranga ndani yake (hiyo ni kwa mayai ya kuuza kwa matumizi ya lishe)
kama unahifadhi yai la kutotolesha hilo halitakiwi lizidi siku 14 uwe tayari ushampa kuku kwa ajili ya kuatamia.
kwa faida yako na wengine si lazima kuku wa kienyeji apandwe na jogoo ndio atage, umri wake wa kutaga ukifika tu ataanza kutaga, ambao ni miezi sita hadi saba.

Pia bei ya kuku wa kienyeji zaidi kutokana na ladha yake na wala sio kilo zake.

Mwisho.

Ningefarijika sana kama unge declare interest kuwa wewe ni mfanya biashara wa hao kuku uliowapigia debe, hata ukaweka na picha zao na namba yako, kuliko kuwakatisha tamaa wafugaji waliojikita ktk ufugaji mdogo mdogo wa kuku wa kienyeji.
Pia nawatia moyo wafugaji wote wasikatishwe tamaa na maandiko kama hayo bali yawe chachu ya wao kujua zaidi mbinu mbali mbali za kupata kuku wengi ndani ya muda mfupi na wasichoke kujifunza.

kama utanataka kujua chochote kuhusu kuku wa kienyeji njoo in box nitakusaidia bila ya malipo yoyote, mimi sio mfanya biashara, nami nakaribisha kukosolewa.







Nitakutafuta ndg nimekuelewa. Huyo jamaa kachemka lkn nae niuelewa wake..
 
Mkuu shukrani kwa maelezo mazuri, yanatia Moyo kwa ambao tunataka kuanzisha miradi ya kuku wa Kienyeji. Tunaweza kujifunza mengi kupitia watu kama nyie wenye uzoefu kama wewe na Ginner
Asante kwa mchango wako mkuu.kiukweli kama unataka kua mfugaji usiogope wala kusikia maneno yenye kukatisha tamaa.mm nilipata maelezo mengi na maandiko mengi tena humu jf hasa jamaa mmoja aitwae Gazeti ana uzi wake humu.nilisoma makala yote bila kuacha hata coment moja.nikaanza kufuga.kiukweli mwanzo nilipata changamoto saana nakumbuka mara ya kwanza nilianza na kuku wawili baada ya kama miezi minne nikawa na kuku zaid ya 40. Kilichotokea ni malaika wako ndo wanajua maana wooooote walikufa baada ya kupata ugonjwa.nilikula kuku mpaka wakanikina moja leo mm hua Sili firigisi maana zilinikifu kabisaaa!mama yoyo akapata hasira akaniambia hakuna kufuga tena mpka tuhamie kwetu coz nilikua nimepanga! Nami ckua na ubishi maana yy ndo mhudumiaj mkuu hapa hom.nikawa nasoma makala mblmbl kujiongezea maujuzi.nikshamia hom kwangu nikaanza na kuku wawili tena baada ya miezi 4 nikapata kama 60 pamoja na makinda nao pia nikapata mtikisiko wakapata ugonjwa nikabak na mmoj nikaanza tena. Sasa nimeanza kutulia maana nimejifunZa mengi.hakuna kukata tamaa.
 
Mkuu kipekee nimejifunza mengi kupitia hii makala yako, na kama ntakua na plani ya kufuga kuku ni dhahiri ntakutafuta nipate mwongozo na matirio zaidi
 
Ginner
Mimi ni mfugaji wa kuku wa kienyeji pure. Nimeanza miaka mi3 iliyo pita na nimepata faida sana hata kuku wa kizungu sitamani
1 wana soko hasa katika mahoteli makubwa
2 kuku wa kienyeji anafundishika tabia. Na ukitaka faida usisubiri kuku akulele vifaranga
3 kuku wa kienyeji ni wavumilivu na hawahitaji mlolongo saana wa chakula ( kila siku madini n.k)

Mimi naweza nikakukosoa saaaana na kukuomba uombe radhi kwa wana jamvi
Kiwango cha kuku nilicho nacho. Kila mwezi lazima nipate zaidi ya 90( trey 3 hizo). Soko langu liko kwenye mahoteli na mayai yanakaa wiki 2 hadi kuharibika na kuharibika kwakwe si kwamba ushindwe kula.
Safi Sana Mkuu, Tunashukuru kwa kututia moyo, Miaka mi3 inatosha kabisa kukupa ujuzi na uzoefu kuhusu huu mradi, Ni dhahiri tutajifunza mengi
 
12
Utengenezaji wa vyakula vya Kuku
Namba moja hadi nne katika jedwali hili ni michanganyiko wa vyakula aina 4 tofauti
kwa ajili ya kuku wenye umri uliotajwa hapa juu. Ukihitaji kuandaa chakula cha kuku
hao, chagua mchanganyiko mmoja (kwa safu wima) wenye malighafi zinazopatikana
kwenye eneo lako kwa urahisi na utakazozimudu kifedha.
UTAYARISHAJI CHAKULA CHA KUKU WANAOTAGA (MIEZI 5 HADI MIEZI
18) PAMOJA NA KUKU WAZAZI
Aina ya vyakula
Kiasi (kilo)
Chenga za Mahindi
31.5kg
Mtama
15.0kg
Pumba ya mahindi
13.0kg
Mashudu ya Alizeti
20.0kg
Dagaa
12.0kg
Chokaa
3.0kg
Premix
0.25gm
Chumvi
5.0gm
Jumla
100kg
-------------------------------------------------------------------------------

Aina ya vyakula
Kiasi (kilo)
Dagaa kilo
12.0kg
Chenga za mahindi
30.0kg
Mtama
6.75kg
Mashudu
20.0kg
Pumba ya mahindi
23.0kg
Chumvi
0.25gm
Chokaa
3.0kg
Mifupa
5.0kg
Jumla
100kg
AU
Vyakula hivi vyote vinafaa kwa kuku watagaji na kuku wazazi. Tofauti kwenye kuku
wazazi ni kuwa wanalishwa kiasi pungufu ili wasinenepe na kushindwa uzalishaji.
Mwongozo uliotolewa, hapa juu ni kwa ajili ya kuandaa kilo 100 za chakula cha kuku,
endapo unataka kutengeneza kilo 500 itabidi kila kilichopo kwenye mchanganyiko
kizidishwe, mara tano ndipo kupata hizo kilo 500....HAKIKA KINAFANYA KAZI JARIBU HIYO 4MLA END INGATIA HAWAUMWI UTAPATA MATOKEO

Dah! Safi Sana Mkuu, Kuku wangu wako mbioni kuanza kutaga, Naamin huu muongozo utanisaidia sana. Kiukweli mwanzoni wakiwa na miezi mi3 walikuwa wanakufa sana, karibia 30 hivi. ila sasa nashukuru mungu wamekuwa wakubwa vifo zimekoma na walibakia kama 100 hivi.

Mkuu kwa Kilo 100 baada ya kuzichanganya zinatosha kulisha kuku wangapi na kwa muda gani? Na je chokaa ni chokaa tuu hata hii inayotumika kwenye Ujenzi inafaa. Nauliza kaama huwa nasikia kuna chokaa maalumu kwa ajili ya kuku, Kwa kipindi chote hicho tumekuwa tukiwapa chakula kilichoandaliwa tayari
 
Kuna jamaa yangu mmoja alinielekeza namna nzuri ya kuku kutotoa mayai yote bila kuacha. Ni kwamba aliniambia ninunue vile vibeseni vidogo vya kunawia then ndan unaweka mchanga kiasi halafu weka mayai yako tayari kwa kuliwa na kuku. kiukweli njia hii nilitumia na imefanikiwa. kwa wafugaji wenzangu jaribuni muone maajabu yake.
Kitu kingine ni utunzaji wa vifaranga baada ya kutotolewa napo hapa kuna changamoto wakati wa usiku kutokana na barid kwa vifaranga hasa kwa wafugaji wa hali ya chini,mm mwanzo nilihangaika but nikapata njia nyingine bora ya kutunza vifaranga wakati wa usiku,nilitenga sehm ya kuwalaza. Hapa unaweza chukua hata box kubwakubwa la kuwatisha vifaranga then nikatafuta chungu!! Nikaweka majivu ndani kwa hio kila usiku nilikua unaweka mkaa wa moto mle ndani ya chungu na kufunika na majivu!! Nakwambieni ndugu zangu wafugaji vifaranga hawapati barid kabisaaa! Na huo moto ulioko ktk hilo jivu utaukuta mpka asubuhi na utatumia kwa kuwashia moto hapo kwa nyumba yako. jaribuni na njia hii muone mafanikio yake na si kukaa ohhh nitanunua vifaranga 500 nianze hapana anza hata na kuku 2 au 3 baada ya mda utakuja nambia. Yangu ni hayo labda hujaelewa uliza tupeane maujuzi.
Hongera mkuu! Huna hiyana Mungu atakuongezea! Mm sio mfugaji wa kuku, na wala sitegemei kufuga kuku kwa maengo ya biashara, ila nimeukubari mchango Wako!
 
Nashukuru kwa kukubali kupokea challenge,
kwa ufupi andiko lako limejaa upotoshaji mkubwa na linalenga kuwakatisha tamaa, wajasiriamali wadogo wadogo ambao wanapendelea kufuga kuku wa kienyeji.
Pia nimegundua mambo makubwa mawili,
1. Bila shaka utakuwa unauza hiyo aina ya kuku amabayo unadai kuwa ni wazuri.
2. Bado hujajua mbinu mbali mbali za ufugaji wenye tija.

Hebu tazama hapa, ulichoandika.

Kwa asili ya kuku wa kienyeji,huwa wanatabia ya utagaji wa mayai 7-10 na mara nyingi ni siku kwa siku 10 mfululizo, utamiaji -siku 21, na uleaji wa vifaranga - siku 50-60. Hii inampelekea kwa kuku mmoja kuweza kutaga wastani wa mayai 35-50 kwa mwaka kwani anapoteza muda mwingi kwa shughuli za utamiaji na malezi ya vifaranga badala ya kutaga. Idadi hii ya mayai haina tija kibiashara kwani kuku mmoja anaweza kukuzalishia tray 1 mpka mbili kasoro pekee kwa mwaka ambayo kwa bei ya soko si Zaidi ya shilingi za kitanzania 20,000 tu kwa mwaka.

kuku wa kienyeji wanataga mayai 15 hadi 20 na sio kwa siku za mfululizo kuna siku nyingine huwa hatagi na hii inatokana na kutokushiba vizuri, nakubali kuhusu muda wa kulea kuwa ni siku 50 hadi 60. unachotakiwa kufanya siku tatu baada ya kuku kutotoa vifaranga, mnyang'anye vifaranga na uviweke mbali nae huko vipatie chakula cha kukuzia stater, maji ya kunywa changanya na glucose, pia weka na chanzo cha joto kama ile mtungi wenye mkaa wa moto ndani yake.
ukifanya hivyo itamchukua kuku huyo uliemnyang'anya vifaranga wiki mbili na kuanza tena utagaji.
kwa mwaka atatoa kati ya mayai 100 hadi 160 kwa uhakika.

Tizama na hapa.

'Mayai ya kienyeji ni kati ya bidhaa ngumu Zaidi kuhifadhika. Ikumbukwe kuwa tofauti na mayai ya kisasa, mayai ya kienyeji huwa yamerutubishwa na majogoo. Hivyo kuharibika ndani ya muda ya week moja au pungufu kama hayatatuzwa katika mazingira salama kwaajili ya utunzaji. Kipindi cha joto kali, mayai haya huanza kujitenenezea kifaranga au mishipa ya damu ambayo baada ya muda mfupi hugeuka viza na kutofaa kwa matumizi tena.

uhifadhi wa mayai ya kienyeji sio mgumu, yanakaa bila ya kuharibika kwa muda wa mwezi mmoja, unachotakiwa kufanya, hifadhi mayai yako ktk trey ya mayai, pia chunguza kama yai lina ufa hilo usilihifadhi litumie kwa kula mwenyewe na familia, pia weka mayai yako sehemu ya wazi ambayo ina mwangaza wa kutosha, kuyaweka mayai sehemu isiyo na mwangaza kutapelekea mayai kuanza kutunga kifaranga ndani yake (hiyo ni kwa mayai ya kuuza kwa matumizi ya lishe)
kama unahifadhi yai la kutotolesha hilo halitakiwi lizidi siku 14 uwe tayari ushampa kuku kwa ajili ya kuatamia.
kwa faida yako na wengine si lazima kuku wa kienyeji apandwe na jogoo ndio atage, umri wake wa kutaga ukifika tu ataanza kutaga, ambao ni miezi sita hadi saba.

Pia bei ya kuku wa kienyeji zaidi kutokana na ladha yake na wala sio kilo zake.

Mwisho.

Ningefarijika sana kama unge declare interest kuwa wewe ni mfanya biashara wa hao kuku uliowapigia debe, hata ukaweka na picha zao na namba yako, kuliko kuwakatisha tamaa wafugaji waliojikita ktk ufugaji mdogo mdogo wa kuku wa kienyeji.
Pia nawatia moyo wafugaji wote wasikatishwe tamaa na maandiko kama hayo bali yawe chachu ya wao kujua zaidi mbinu mbali mbali za kupata kuku wengi ndani ya muda mfupi na wasichoke kujifunza.

kama utanataka kujua chochote kuhusu kuku wa kienyeji njoo in box nitakusaidia bila ya malipo yoyote, mimi sio mfanya biashara, nami nakaribisha kukosolewa.

mkuu naomba nitolee maelezo maeneo machache kuhusu bandiko lako hapo juu ulilokuwa kwa wema kabisa ukikosoa baadhi ya Hoja zangu. nashukuru sana kwa maelezo yako mazuri yaliyojitosheleza, ila ningependa kuzungumza mambo machache juu ya hoja zako kama ifuatavyo

“Ningefarijika sana kama unge declare interest kuwa wewe ni mfanya biashara wa hao kuku uliowapigia debe, hata ukaweka na picha zao na namba yako, kuliko kuwakatisha tamaa wafugaji waliojikita ktk ufugaji mdogo mdogo wa kuku wa kienyeji.
Pia nawatia moyo wafugaji wote wasikatishwe tamaa na maandiko kama hayo bali yawe chachu ya wao kujua zaidi mbinu mbali mbali za kupata kuku wengi ndani ya muda mfupi na wasichoke kujifunza.

kama utanataka kujua chochote kuhusu kuku wa kienyeji njoo in box nitakusaidia bila ya malipo yoyote, mimi sio mfanya biashara, nami nakaribisha kukosolewa. “




Kwa namna dunia na taifa linavyohimiza juu ya kilimo cha kibiashara, nitashangaa sana kama mfugaji au mkulima aone aibu kukiri kuwa yeye ni mfanyabiashara ya kilimo na ufugaji.

Dunia ya sasa tunaondokana na dhana ya kilimo na ufugaji wa mazoea ambao umekuwa unatumika na kwa miaka kadhaa, na kufanya shughuli hizi kuwa rasmi na kufuga au kulima kwa kulenga soko.

Nitoe angalizo tu, kwa wafugaji na wakulima, kama utaingia kwenye shughuli hizi za kilimo na ufugaji bila ya kuwa na mpangilio mzuri wa namna ya kuendesha shughuli hizi kibiashara nakuhakikishia unafanya mchezo wa mdako. Utatelekeza shamba kama wakulima wa nyanya uko dumila

Ifikie hatua hizi shughuli zifanyike kibiashara, wakulima wawekeze kwenye mbinu za kuendesha miradi yao kibiashara Zaidi na si kwa mazoea. Hivyo basi, naomba nikuunge mkono kwa hoja yako ya kudeclare interest ya kuwa mfanyabiashara.



I declare interest: “Mimi ni mfanya biashara ya ufugaji, najitahidi kuepukana na mbinu za ufugaji zisizo na tija. Nimejitajidi kuepukana na madalali waliokuwa wakirudisha nyuma jitihada zangu za biasahra hii ya ufugaji kwa kujijengea utegemezi kwenye mnyororo wote thamani.



Namiliki kampuni ya ufugaji, Backyard (T) LTD, inayojishughulisha na ufugaji mdogo mdogo wa majumbani hasa at the backyards, hivyo basi,ufugaji wangu ni biashara rasmi kabisa na naiiendesha kitaalamu.



Ili kuondokana na utegemezi katika ufugaji, nimeweza kufungua kiwanda kidogo kwa ajili ya uzalishaji wa vifaranga na kwa sasa nazalisha wastani wa vifaranga 1000 chotara kila wiki (kila jumatatu).



Pili,nimekuwa nanyonywa sana na madalali wa kuku hasa wanapokuja kununua kwa bei isiyo ya soko. Kutatua hili, nimefanikiwa kumiliki machinjio yangu ya kisasa kwaajili ya kuprocess nyama ya kuku na kusambaza kwenye masoko rasmi hasa high profile hotels, restaurants supermarkets etc. brand yangu ya kuku inaitwa backyard frozen chicken. Machinjio yangu si makubwa sana,ila yana uwezo wa kuprocess mpaka kuku mia tatu kwa saa. Kwa mahitaji yangu yanatosha kwa sasa.

Mimi si mfugaji, ila Ninafanya biashara ya ufugaji, na ninajivunia hili.



“kuku wa kienyeji wanataga mayai 15 hadi 20 na sio kwa siku za mfululizo kuna siku nyingine huwa hatagi na hii inatokana na kutokushiba vizuri, nakubali kuhusu muda wa kulea kuwa ni siku 50 hadi 60. unachotakiwa kufanya siku tatu baada ya kuku kutotoa vifaranga, mnyang'anye vifaranga na uviweke mbali nae huko vipatie chakula cha kukuzia stater, maji ya kunywa changanya na glucose, pia weka na chanzo cha joto kama ile mtungi wenye mkaa wa moto ndani yake.ukifanya hivyo itamchukua kuku huyo uliemnyang'anya vifaranga wiki mbili na kuanza tena utagaji.kwa mwaka atatoa kati ya mayai 100 hadi 160 kwa uhakika.”



Nakubaliana na wewe kuhusu kutumia mbinu mbadala kumfanya kuku aongeze Zaidi utagaji, ikiwa ni pamoja na kumnyanganya vifaranga kila baada ya siku tatu baada ya utotoleshwaji. Swali, does it worth your efforts? Wakuu tusiangalie ule ufugaji wa mazoea ambao tumeshauzoea hapa nchini wa kuwa na kuku wawili mpaka kumi bandani ambao mbinu hizi zinaweza kuwa applicable, tuzungumzie kwa context ya ufugaji wa kibiashara, pale unapokuwa na kuku 500-1000 bandani, kwenye hali kama iyo tunafanyaje. Tuzungumzie kuhusu efficiency katika utotoleshwaji wa mayai, tujiulize kuhusu variation ya umri wa vifaranga, maana kwa mbinu iyo unaweza ukawa na batch Zaidi ya nne kwa week ya vifaranga vilivyotofautiana umri, vipi kuhusu kuwahudumia kwa vitu kama chanjo na madawa etc. Mkuu master the trade. Ufugaji ni biashara.





“uhifadhi wa mayai ya kienyeji sio mgumu, yanakaa bila ya kuharibika kwa muda wa mwezi mmoja, unachotakiwa kufanya, hifadhi mayai yako ktk trey ya mayai, pia chunguza kama yai lina ufa hilo usilihifadhi litumie kwa kula mwenyewe na familia, pia weka mayai yako sehemu ya wazi ambayo ina mwangaza wa kutosha, kuyaweka mayai sehemu isiyo na mwangaza kutapelekea mayai kuanza kutunga kifaranga ndani yake (hiyo ni kwa mayai ya kuuza kwa matumizi ya lishe)
kama unahifadhi yai la kutotolesha hilo halitakiwi lizidi siku 14 uwe tayari ushampa kuku kwa ajili ya kuatamia.
kwa faida yako na wengine si lazima kuku wa kienyeji apandwe na jogoo ndio atage, umri wake wa kutaga ukifika tu ataanza kutaga, ambao ni miezi sita hadi saba
.”


Kinachofanya yai la kuku wa kienyeji liharibike ni kwa vile liko fertilized. Its just a simple biology na iko wazi kabisa. Mara nyingi yai la kuku wa kienyeji huwa limerutubishwa na jogoo. (nikimanisha lina mbegu). Hivyo yai hili lililorutubishwa linahitaji kiasi flani cha joto ili zile mbegu kuanza kujijenga na kuwa zygote, embryo na baadae kuwa kifaranga kamili.

Nitaweka attachment ya stages za ukuaji wa kifaranga ndani ya yai hapa baadae kidogo, ila ni siku ya nne tu kama eneo lina joto la juu, (kwanzia nyuzi joto 30 kuendelea) yai huanza kutengeneza mishipa midogo ya damu na siku ya sita baadhi ya viungo vya kifaranga vinaanza kuonekana. Hivyo basi, kuweza kulihifadhi yai hili, ni lazma lihifadhiwe kwenye mazingira yenye baridi ikiwezekana chini ya nyuzi joto 26 ili kusimamisha development ya kifaranga ndani ya yai.

Ili yai liwe kifaranga, linahitaji kiwango cha nyuzi joto cha 37.8 kisichobadilika sana kwa muda wa siku 21, kwa vile joto la mazingira hupanda na kushuka, na mara nyingi haifiki kiwango kinachohitajika ili kifaranga kizidi kujijenga, maendeleo ya ukuaji wa kifaranga husimama ndani ya yai na baada ya muda uoza na kuywa viza.



Uwezo wa wafugaji kuweza kumaintain kiwango hiki cha joto si mkubwa, kwa wakazi wa maeneo yenye joto ni ngumu sana kuhifadhi mayai haya bila kuwa na chumba kilichofungwa air condition.

Kwaiyo kwa hili la uhifandhi kuwa changamoto sitafuta kauli yangu.



Pia bei ya kuku wa kienyeji zaidi kutokana na ladha yake na wala sio kilo zake”.



Ndugu yangu, kilimo na ufugaji ni biashara, liweke hili kichwani kwanza ndipo uchallenge baadhi ya hoja zangu. Kama hutakuwa na malengo ya kufuga kibiashara kamwe hatuwezi kuongea lugha moja. Naomba nikujibu kama ifuatavyo.



Ladha ya kuku hutokana na chakula anachokula na si vinginevyo. Leo hii ukichukua kifaranga wa kuku asilia toka singida mfano, ukamlisha chakula cha layers kwa muda wake wote wa ufugaji, hatakuwa na ladha ya kuku wa kienyeji, hivyo hivyo kuwa kuku wa kisasa, ukimchukua broiler leo, au layers, kwanzia akiwa kifaranga akawa anafugwa ka mazingira asilia, kumwachia nje akala majani, panzi na wadudu wengineyo, ukija kumla kuku huyu akishakomaa ladha yake haitakuwa tofauti na kuku wa kienyeji. Kuna baadhi ya wafugaji wanawapa kuku wao wa kisasa majani tu ilimradi kiini cha mayai yao kiwe cha njano na iwe na ladha asilia. Kwaiyo ndugu yangu ladha hutokana na unachomlisha kuku na wala haitokani na aina ya kuku.



Pili umezungumzia bei ya kuku, kwa hapa sitatumia nguvu nyingi kutoa maelezo kwani umeshadeclare interest kuwa, wewe si mfanyabiashara.

Ukiwa mfanyabiashara ya ufugaji soon or later, utagundua soko la kuku si hili la kumuuzia jirani yako kuku wawili kwaajili ya sikukuu kwa sh 30,000 ukaona inalipa, kwani soko la mtaani halina standards.

Mfanyabiashara ya ufugaji huu ni wakati wa kufikiria kupata soko la rasmi la hotels au super markets wanaotaka mzigo wa Zaidi ya kuku 500 kwa week au kwa mwezi.

Au soko la export ambalo wao wanasema supply tani tano za kuku wala hawako interested kujua watakuwa kuku wangapi, kama ni wawili sawa, kama ni 20,000 sawa ila wanataka uzito. Sasa ndugu sijajua unafanya ufugaji kwa malengo gani na unatarget soko gani, nisingependa kukupinga maana sijajua malengo yako ya ufugaji ni ya nini, either ni kwaajili ya passion tu ya kuona kuku wako bandani au unalenga soko.





Pamoja na hayo yote, nashukuru sana kwa challenge, kwenye biashara si vyema kuwa na rigid mind, lazma kusikiliza wengine wanafanya nini iliujifunze Zaidi. Nakiri nimejifunza mengi kwa hoja zako na ninaahidi kuzifanyia kazi.

Pia nashauri, wanajaamii kupima, kwamba wapi wanaweza kufanya study za mbinu za ufugaji holela na wapi wanaweza kupata mbinu za ufugaji wa kibiashara.
 
Mkuu kwanza nikupingeze kwa makala yako nzuri.

Ila mimi niko katika kufanya utafiti na hawa kuku wa kienyeji na nimechagua kuku 7Majike na jogoo mmoja. Nimefanikiwa kwa mwezi wa nne sasa kupata mayai 5 kila siku yakishuka ni 4 kuku hupunzika kidogo na kuendelea siwalazishii naweka mayai kwenye mashine.

Tunachotakiwa ni kubuni mbinu za kuwafuka kuku wa kienyeji kwa maslahi na sio kuwaacha.

Pia ninao wengine nafuga ila nitatoa taarifa kamili baada ya utafiti kufika kikomo.
Ginner amenikosha, ila nawe umenikuna haswaaa! Sasa nakupataje?​
 
Mkuu ningeanza kukupongeza kwa makala au tafiti yako hii. Kisha ningependa nitoe maoni yangu kama mfugaji anaejifunza kufuga kuku wa kienyeji (pure). Kuhusu muda wa kuharibika mayai imekuwa tofauti kwa upande wangu, hukaa zaidi ya wiki mbili bila kuharibika kwa kipindi chote cha kiangazi sijui nisubiri msimu wa joto kali. Kuhusu bei pia ya kuku wa kienyeji nadhani koo/mtetea anaanzia 14,000/- hadi 17,000/- kutegemea na mahali unapouzia na matukio ya nyakati kama sherehe za kidini. Bei hiyo ni kwa Dar na kuku sio lazima azidi uzito 1kg. Wateja wako kama ni supermarkets au hotel labda ndio hupima uzito lakini masokoni kama Kisutu, Mwenge, na mitaani hawapimi uzito kwa mizani wakati wa kununua. Majogoo waliokomaa vizuri bei ni 17,000/- hadi 25,000/- bila kujali uzito bali umbo. Huwa wananuliwa sana hivyo soko sio tatizo. Changamoto kubwa kuliko zote ni malisho/chakula ni gharama kubwa sana ukizingatia inabidi wafungiwe ktk sehemu flani lakini wale pumba na majani/nyasi pamoja na wadudu ili kutunza ladha yao na rangi ya mayai yao. Pia bei za samaki ulizosema ni za zamani sana kwani sasa 1kg ya samaki aina ya tilapia(sato) inafika 10,000/- lakini siku chache zijazo itashuka kufika 8,000/- hadi 9,000/-. Mwisho wa yote ningependa kuuunga mkono mengi uliyoyaeleza katika tafiti yako. Angalizo ni kuwa mimi ndio kwanza nimeanza ufugaji wa kuku wa kienyeji miezi michache hivyo mengi siyajui. Hapo awali nilianza kununua vijijini na kuwauza moja kwa moja nikaona bora nianze kufuga.
 
Kwa nyongeza ningependa nimuunge mkono mdau "Mfuga kuku" maelezo yako ya kuku mbadala kiasi fulani na baadhi ya hoja zako zimekuwa na mlengo wa kufanya PROMO ya bidhaa zako yaani hao Cross breed e.t.c. Kitu ambacho sio dhambi lakini ingekuwa vema ungekuwa neutral flani au ungeweka tangazo lako la hao kuku kule jukwaa la matangazo ya biashara. Pili kulikuwa hakuna ulazima wa kusema umri wako kujaribu kuonesha mafanikio uliyopata haraka kwa hii biashara na elimu yako, hii ni kama aina ya majivuno/majigambo flani. Kwani sisi tunaweza kuthibitisha vipi umri wako hapa JF? Na je ulifanikiwa haraka bila kuwezeshwa na mtu/familia? Pia hatuwezi kuthibisha kama umefanikiwa kiuchumi ktk biashara zako kwani kuwa na kampuni au kiwanda haimaanishi vinaleta faida kubwa na havileti madeni makubwa kwako. Kumalizia sio dhambi kuwa na majigambo na mafanikio yako kiuchumi na kielimu lakini it sounds unprofessional, though it might inspire young fellows.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom