Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,946
- 38,658
Tumesikia na kuona hivi karibuni kwa jirani zetu Uganda. ambapo rais wa nchi hiyo akisaini kuidhinisha kuanza kutumika kwa sheria dhidi ya matendo ya ushoga nchini humo. Ikumbukwe kwamba adhabu kali zitawaandama ikiwemo vifungo vya maisha kwa wanaojiushisha na mapenzi ya jinsia moja. Ingawa sambamba na hilo, sheria hiyo imewabana wanawake ambao uvaaji wao unakiuka maadili kwa kuwawekea vifungu vya adhabu.
Mwangwi wake umesikika dunia nzima ambapo tayari sasa nchi wahisani (wanavyopenda kujiita) wameanza kuondoa kitu kinachoitwa misaada kwa serikali ya Museveni. Waholanzi wamekenda mbali zaidi kwa kusema fedha walizoziondoa kwenye bajeti ya serikali watazielekeza kwenye taasisi zinazofanya kampeni za haki za binadamu (hasa hasa zinazotetea maslahi ya mapenzi ya jinsia moja)....
Turudi hapa nchini kwetu. Ambapo kumesikika wanaharakati wakipambana na mawazo ya jamii kuhusiana uhalali na uharamu wa mapenzi ya jinsia moja. Tayari tangu kale yameshajitokeza mashirika ambayo yameoneshwa wazi wazi na mengine kwa kificho kuunga kwao mkono kampeni hizi za kutaka kuhalalisha mapenzi hata ndoa za jinsia moja. Hapa ikumbukwe kuna ushoga na usagaji ambapo wahusika wakuu wanapiganiwa hakii zao waweze kuendesha shughuli zao wazi wazi bila kuchukuliwa hatua za kisheria na jamii isione kwamba ni kinyume na maadili.
Hebu tutazamane usoni sasa...
Kwa mtazamo wangu,
Ni kwamba mahusiano ya kingono hata kuingia kwenye ndoa za jinsia moja hatima yake ni hitimisho la mwendelezo wa kizazi. Ambapo katika mahusiano ya ndoa (tafsiri yangu) ni lazima mwenza mmoja awe na uwezo wa kutoa mbegu ambazo zinaweza kurutubishwa ktk viungo vya uzazi wa mwenza mwingine ili kutunga mimba hatimaye kizazi kuendelea kwa kupata mtoto ama watoto... Lakini mwanaume anapomaliza tamaa zake za ngono kwa mwanaume mwenzake kisha tunalazimishwa kuhalalisha uhusiano huo kama njia mojawapo ya asili katika kutendea haki hisia zetu ni wazi tunaliangamiza taifa.
Pia tujadili hizo tabia zinazopelekea uwepo na ukuaji wa wasagaji na mashoga nchini.

- Nini mantiki ya mataifa yenye nguvu kubwa kiuchumi kulazimisha maadili yao kuwa sheria kwenye nchi zingine hususani Afrika?
- Ni kweli maisha ya mashoga na wasagaji yapo hatarini kiasi ya kutungiwa sheria ya kuwalinda?
- Kuna ukweli kiasi gani kisayansi kwamba ushoga ni tatizo la kitabia na si kijenetiki?
Kwa mtazamo wangu,
Ni kwamba mahusiano ya kingono hata kuingia kwenye ndoa za jinsia moja hatima yake ni hitimisho la mwendelezo wa kizazi. Ambapo katika mahusiano ya ndoa (tafsiri yangu) ni lazima mwenza mmoja awe na uwezo wa kutoa mbegu ambazo zinaweza kurutubishwa ktk viungo vya uzazi wa mwenza mwingine ili kutunga mimba hatimaye kizazi kuendelea kwa kupata mtoto ama watoto... Lakini mwanaume anapomaliza tamaa zake za ngono kwa mwanaume mwenzake kisha tunalazimishwa kuhalalisha uhusiano huo kama njia mojawapo ya asili katika kutendea haki hisia zetu ni wazi tunaliangamiza taifa.
Pia tujadili hizo tabia zinazopelekea uwepo na ukuaji wa wasagaji na mashoga nchini.
Jambo linalostua zaidi kwa mtazamo wangu ni kwamba,
Katika nchi zetu za kiafrika, mashoga walikuwepo tangu kale na jamii haikuwatenga na wala hawakuwa hatarini kimaisha. Nadhani wale waliokulia Dar miaka ya 80 hamtamsahau Aunty Mudy ambaye alikuwa maarufu sana Dar enzi hizo...
Kinachostua sasa ni kwamba, nchi za Magharibi zimeanza kushinikiza mataifa yetu kutambua haki za wapenzi wa jinsia moja kwa miongo kadhaa sasa. Najiuliza haya maslahi ya kuunga mkono tabia zinazopingana na maadili, utamaduni na mapokeo yetu ni ya nani? Kwa nini tulazimishwe kuishi kama watakavyo wao? Ni jambo gani Magharibi imewahi kukubali kutoka Afrika? Kwa nini Afrika ilazimishwe kukubali kila la kwao?
Maswali haya na mengine tunaweza kujibu na kupata mwelekeo mzuri kwa vizazi vyetu