Niliahidi kuwa kipindi hiki cha Pasaka hatutakuwa na mada zetu zile , kwahiyo hii moja isifananishwe na zile japo ina muktadha unaofanana ni zile.....
Ni hili jambo la kubeba mitunguli na midubwana mingine na kumepelekea mgonjwa wako aliyelazwa kwenye hospital ya tiba za kisayansi, kwa nia ya kumkinga au kuwadhuru wengine.....
Kama huko alikotoka alikosa hii kinga na tiba mpaka akaumwa kufikia ya kulazwa kwenye hii tiba mbadala!faida gani sasa kuendelea kujidanganya kuwa huko kwingine bado kuna nguvu na msaada? ??
Siku hizi kwenye hospitali zetu kuna utaratibu mzuri sana wa kuwapekua ndugu jamaa na marafiki wanaokuja kutazama wagonjwa ni utaratibu mzuri kwakuwa umepunguza tatizo na wengi wamenyakwa
Lakini kuna la ziada serikali inapaswa kulifanya..kutafuta utaratibu wa kuwapekua hata watokao sio na magari tuu bali hata raia
Hospitali ni chimbo moja murua sana lenye utajiri wa malighafi za kufanyia ushirikina, kuanzia mabendeji yenye damu, mambo yote yanayohusika kwenye wodi za wazazi na watoto, wodi za wagonjwa wa ajali mpaka mochwari na mabaki yoyote yale ya mgonjwa au chochote alichokitumia mgonjwa hata kama ni chakula
Tunakumbuka vema sakata la Rama mla vichwa na kuku wenye hirizi Muhimbili.... Serikali ilitafakari hili