Ushirikina kibaha

mhh mpaka leo kuna watu wana haya maimani,huoni aibu hata kuutaja tu nini kuonyesha unauamini
Ndio jamii zetu hizi, hayo mambo yapo mubashara mitaani. Natamani serikali iweke nguvu kwenye kuyapiga marufuku, bahati mbaya walioko serikali kuu ndio wabobezi!
 
Kwa asili Wagweno hapo kale walikuwa Wapagani wanaoabudu mungu jua [RUBHA], pamwe na mwandani wake MWIRI [MWEZI], mkewe jua, sanjari na watoto wao nyota.

Ibada hii ya kuelekea jua iliambatana na kuabudu mizimu na ndiyo maana kuhani wa Kigweno alipochinja mnyama na kumchuna ngozi yake aliweza kutazama maini kupiga ramli kwa kutumia viungo kwenye tumbo la mnyama.

Tena wanyama hao walichinjwa kwenye eneo maalumu liitwalo kwa Kigweno Ngondinyi. Mara nyingi eneo hili walihusika wanaume bighairi wanawake kwa sababu kwa mila ya Kigweno wanaume ndio makuhani. Mara nyingi katika eneo la kuzunguka Ngondinyi kulipandwa mimea maalum iitwayo Mathale, ambayo kwa mujibu wa mapokeo ya Wagweno ni mimea mitakatifu.

Mnyama anapochinjwa kuhani hukata vipande vidogovidogo na kuviweka eneo husika, kisha huchukua pombe ama mbege au dengelua kisha atatazama mbinguni huku ameshika mkononi pombe kama ishara ya tambiko na kusema RUBHA KAGHU NGOMA MBAI; yaani, naamini mungu yuko juu, lakini chini kuna mizimu. Kisha humwaga pombe na kusema anachokusudia, kama anataka mvua inyeshe au anakusudia kuondosha MSINYANYO [mkosi].

Kwa maana kwa mujibu wa mapokeo ya Wagweno mkosi kwao ulikuwa jambo kubwa sana na ndiyo maana hata mtoto aliyezaliwa na ulemavu wa aina yoyote alitolewa kafara kwenye jiwe la watoto, kwa Kigweno IGHWE YA BHANA.

Mhanga alikuwa anachukuliwa kwenye jiwe husika, mamaye humbembeleza, akiisha kulala hulazwa kwenye kilele cha jiwe na anapoamka ghafla huporomoka na kufa na watakuwa wameondoa mkosi katika jamii na kumfurahisha mahoka.

Kuna kisa kimoja cha kale juu ya bwana mkubwa mmoja aliyeitwa Kindobhai wakati anafukuzwa na maadui kunako eneo ambalo kwa sasa kuna hifadhi ya wanyama ya Tsavo karibia na ziwa Jipe. Inasemekana alipiga fimbo yake kwenye maji na yeye, mifugo na wafuasi wake wakavuka salama!

Masimulizi juu ya Wagweno ni mengi sana, kiasi kwamba unaweza ukastaajabu. Mpaka leo kuna mawe ya ajabu ambayo yako mithili ya watu; inasemekana maadui hapo kale walikuwa wanakuja kuiba mifugo huko, lakini kulingana na ujuzi wa wazee wakageuzwa mawe kwa njia ya miujiza.
 
Back
Top Bottom