Ushindi wa maonyesho ya nanenane | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushindi wa maonyesho ya nanenane

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Umutimbaru, Aug 9, 2011.

 1. Umutimbaru

  Umutimbaru Member

  #1
  Aug 9, 2011
  Joined: Jul 22, 2011
  Messages: 91
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Maonyesho ya Nanenane ni maonyesho ambayo wakulima huwa wanonyesha mzao yao. Wataalamu wa zana mbalimbali na wafanya biashara kuonyesha zana zitumikazo kurahisishia wakulima hao kupata mazao yaliobora kwa gharama ndogo. Wana JF shida yangu ni namna gani hawa wanaoandaa maonyesho haya na nivigezo gani wanavyovitumia katika kuchaguwa washindi. Ni wakulima gani wagani wanaoshindanishwa. Na mshindi anapopatikana huwa Anakuwa amefundisha nini jamii ya wakulima ambao niwengi wenye uwezo wao ni mdogo na wakati.Mwaka Fulani nilitembelea kiwanja kimoja cha maonyesho na ilikuwa ni siku ya kutangaza Mshindi wa maonyesho ya kilimo cha bustani na kweli aliechaguliwa bustani yake ilipendeza ilikuwa nzuri sana kuliko zote katika uwanja huo, kwani mchicha ilipendeza sana sukuma wiki ilipendeza sana na mazao yote yalioandaliwa yalikuwa mazuri sana yalivutia.Shida ya hawa wanao pima matokeo haya wanazingatia gharama ya kuzalisha hayo mazao. Mkulima wakawaida baada ya kuona mazao haya anafaidika nini? au anajifunza nini?.Kwa mawazo yangu hawa wanaotadhimini ushindi wa hao wataalamu wangelikuwa wanalenga ni njia ipi mkulima wakawaida anaweze kulima kwakuzingati hali halisi ya eneo, upatikanaji wa mahitajio mfano maji, mbolea, mbegu bora na vinginevyo na kupata mazao Kama yao. Likini unakuta Mshindi anatumia gharama kubwa ambayo hata hailingani na zao Hilo likiuzwa katika soko la kawaida.Wana JF Mnaonaje hilo wazo.
   
 2. BiMkubwa

  BiMkubwa JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2011
  Joined: Jan 9, 2007
  Messages: 530
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Mawazo yako ni ya msingi hasa ukizingatia safari hii mshindi alikuwa wizara ya afya. Imagine, wizara kama hii itashindaje maonyesho ya wakulima?
   
 3. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #3
  Aug 9, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 589
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  kama imeruhusiwa kushiriki kwanini isipate nafasi sawa ya ushindi kama washiriki? Kama ni makosa basi yameanzia mbali.
   
 4. Umutimbaru

  Umutimbaru Member

  #4
  Aug 10, 2011
  Joined: Jul 22, 2011
  Messages: 91
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Ni kweli maonyesho wa wakulima ya itukuwaje ishindanishe hospitali
   
 5. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #5
  Aug 10, 2011
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Ni kama mashindano ya urembo. Anayeshinda siyo lazima au kweli kuwa ndiye mzuri kuliko wote katika eneo husika.
   
 6. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #6
  Aug 10, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,129
  Trophy Points: 280
  Wakuu tujiulize Hivi wizara ya Afya inaingiaje kwenye maonyesho ya kilimo? Na c hiyo tu kulikuwa na tume ya Taifa ya kuratibu filamu Tanzania je tume ya kuratibu filamu na kilimo wapi na wapi?

  Hapa Arusha kulikuwa na maonyesho kama hayo, ila cha ajabu TASO wameruhusu waachuzi na maonyesho yalijaa mabanda ya Vitu vya kichina kama nguo, vyombo vya ndani na kazalika. na mabanda ya kupromot pombe ndo yalikuwa mengi sana kwenye maonyesho haya pamoja na mabanda ya makampuni ya simu yalikuwa kila kona.

  HAYA YANAWEZEKANA KWA TANZANIA TU, NCHI NYINGINE MAONYESHO YA KILIMO NI KILIMO TU
   
 7. Umutimbaru

  Umutimbaru Member

  #7
  Aug 11, 2011
  Joined: Jul 22, 2011
  Messages: 91
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Maonyesho ya wakulima yawe yanazingati uhalisia wa eneo. Unapoonyesha kilimo cha mboga na umwagiliaji kwa kutumia zana ambazo hata huyo unaemonyesha hawezi kukimiliki sijui kuna maana ipi ya monyesho. Nashauri waandaji wazingatie uhalisia.
   
 8. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #8
  Aug 11, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  lengo limeshapotoshwa zamani saaaaana. huwa naona ni km sehemu ya waandaaji kuiba pesa tu na si kutafuta tija. kila mwaka mashindano sijui maonesho yanafanyika lkn hatuoni faida yake. wizi mtupu!
   
Loading...