Ushindi wa Magufuli utaletwa na UKAWA

Ushindi wa Magufuli utaletwa na UKAWA

Manelezu

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2015
Posts
1,906
Reaction score
2,777
Kwa muda mrefu nimekua nikifuatilia pilika pilika za vyama vya siasa kuelekea October ambapo utafanyika uchaguzi mkuu, na kupata rais wa awamu ya tano. Kwa mtazamo wangu ukawa watashindwa vibaya na Mh. John Pombe Magufuli. Sababu kubwa ninazoziona ni hizi hapa.
1. Ukawa ikiongozwa na chama kikuu cha upinzani kimekosa sura ya kitaifa
Kwa kiasi kikubwa viongozi wa ukawa hususani chadema kilichotoa mgombea urais kimekosa sura ya kitaifa. Viongozi wengi wa chadema wanatoka kaskazini, hii ni weakness kubwa sana kisiasa,, chama cha siasa kwa mazingira ya Tanzania kama kinataka kuchukua dola ni sharti kiwe chama cha siasa chenye sura ya kitaifa ili kipate support kutoka sehemu mbalimbali ya jamhuri ya muungano.

2. Dhana mfu ya mabadiliko
Kwa mtu mwenye civic competence kubwa na anauwezo mkubwa wa kuchambua mambo atakubaliana na mimi hakuna uhusiano wowote wa maana kati ya kubadili chama ili upate mabadiliko, nakubali kabisa kua na upinzani wenye nguvu ni kitu bora katika kujenga utawala bora lakini uhusiano na mabadiliko ni mdogo au hakuna kabisa. Nitatoa mfano: Japani toka mwaka 1955 kimeongozwa na chama kimoja cha siasa LDP TOKA mwaka 1955 mpaka 1993 kikatolewa madarakani kwa mda wa miezi 11 kikarudi tena madarakani mwaka 1994 mpaka 2009 kikatoka tena madarakani, mwaka 2012 kikarudi tena mpaka leo. LPD ndio chama kilicholeta mabadiliko makubwa ya kiuchumi kutokana na sera nzuri za kujenga uchumi. Chama cha kikomunisti cha China kimekaa mda mrefu sana na CHINA ipo hapo ilipo leo.

Tatizo kubwa la UKAWA ni kudai mabadiliko kwa kuwaaminisha wananchi kwamba CCM ikitoka madarakani maisha yatakua mazuri. Kuna tofauti kubwa ya ahadi, kwa maana ya kuleta mabadiliko na kuja na mikakati mizuri ya kiuchumi na kijamiii ili waaminiwe kuongoza nchi, sera zao hazieleweki na wanatumia matatizo ya vijana kwa kuwadanganya kua maisha yatabadilika CCM ikitoka madarakani.

3. Udhaifu wa Mgombea wa UKAWA
Ukawa nawamgombea urais dhaifu, hana uwezo wa kujenga hoja na haelezi vitu vya msingi ili kujenga uchumi na taifa hili na kuleta hayo “MABADILIKO” Lowassa kwa mda mrefu jukwaani ameshindwa kujieleza vizuri na nimtu anaeonekana ana matatizo ya kiafya, amekua haelezi nini atafanya zaidi ya kuhamasisha vijana wadai mabadiliko, LOWASSA NI DHAIFU SANA KUJENGA HOJA UKILINGANISHA NA JOHN MAGUFULI, hili litawaletea matatizo makubwa mbele ya safari kampeni zikipamba moto c z magufuli anauwezo mkubwa wa kujenga hoja na kuitetea vizuri.

Naomba kuwasilisha.
 
Ushindi wa magufuli utaletwa ma kuacha matusi, mihemko, papara kwenye kampeni na kueleza kwa undani atafanya nini, la sivyo ni ukawa kilunda kura kwa nguvu na watu wakabidhi nchi, la sivyo ICC itawahusu watu..
ukawa hakuna kucheka na haya manyani, ni kukaza mwanzo mwisho..
 
Hebu tueleze kinaga ubaga! Jana Mh: JP Magufuli katika dhana ya kuondoa umasikini, alionyesha njia au mkakati upi atakaotumia kuondokana na umasikini?
 
Sio suala la ukaskazini tu, tazama na udini pia, katika wabunge wa Chadema nchi nzima wataogombea 154 kuna wabunge 9 tu waislamu hii imekaa kijuha kabisa, niiteni mdini lakini chama cha kitaifa kuwa hivi kwenye nchi yenye idadi karibia sawa ya Waumini uniambie hakuna wenye vigezo ila wao tu kwangu naona ni maagizo toka kwa wafadhili CDU chama cha kijerumani, tujikumbushe mzee wao Mtei aliposema wakati wa katiba, wajumbe wengi wa katiba ni waislamu, Leo mbona hasemi wagombea wengi waislamu?
 
sura ya kitaifa???? huu uchambuzi peleka lumumba labda watakuamini
 
:sly:😱:thumbdown:😱😡🙄😛😀🙁:what:🙂:beer:😎:banghead::banghead::banghead::banghead::banghead:
 
Ushindi wa magufuli utaletwa ma kuacha matusi, mihemko, papara kwenye kampeni na kueleza kwa undani atafanya nini, la sivyo ni ukawa kilunda kura kwa nguvu na watu wakabidhi nchi, la sivyo ICC itawahusu watu..
ukawa hakuna kucheka na haya manyani, ni kukaza mwanzo mwisho..

Hebu acheni kauli za kijuha ICC inaingiaje hapa?
Tatizo mnapenda kutumia lugha za vitisho na visivyo na staha badala ya kujibu hoja!
 
Manelezu mkuu, umefanya uchambuzi mzuri na mifano yako ni mizuri.
Ila ningeongezea kuwa Ukawa pia imekosa dira na organizational skills. Zaidi ya kumobilize maelfu kwa mkutano wa kumtukuza Lowassa hakuna cha ziada. Wanashindwa hata kupanga mkakati katika mashina. Walitaka kuwalazimisha Sikonge wamsimamishe Said Nkumba!
 
Udini na ukabila pelekeni lumumba. Sisi wengine hatuangalii vitu vidogo hivyo. Dini au kabila havimfanyi mtu akawa mchapakazi au mwadilifu. Watanzania kama mnataka maendeleo ya kweli acheni kabisa kuongelea udini na ukabila. Kwanza ni mtu mpumbavu tu atakayewaza ukabila na udini.
 
Sio suala la ukaskazini tu, tazama na udini pia, katika wabunge wa Chadema nchi nzima wataogombea 154 kuna wabunge 9 tu waislamu hii imekaa kijuha kabisa, niiteni mdini lakini chama cha kitaifa kuwa hivi kwenye nchi yenye idadi karibia sawa ya Waumini uniambie hakuna wenye vigezo ila wao tu kwangu naona ni maagizo toka kwa wafadhili CDU chama cha kijerumani, tujikumbushe mzee wao Mtei aliposema wakati wa katiba, wajumbe wengi wa katiba ni waislamu, Leo mbona hasemi wagombea wengi waislamu?

hatuangalii udini wala ukanda CCM ITOWEKE KWANZA
 
Udini na ukabila pelekeni lumumba. Sisi wengine hatuangalii vitu vidogo hivyo. Dini au kabila havimfanyi mtu akawa mchapakazi au mwadilifu. Watanzania kama mnataka maendeleo ya kweli acheni kabisa kuongelea udini na ukabila. Kwanza ni mtu mpumbavu tu atakayewaza ukabila na udini.

Kwahiyo mtei ni mpumbavu? Aliposema wajumbe wa bunge la katiba wengi wao waislamu?
 
kenya wamebalisha vyama sio chama na uchumi wao juu,tembelea maduka yenu yajumla na supermarket na angalia mtandao wao wa mabenki hapa tanzania......crdb iko nairobi au mombosa?.
 
Udini na ukabila pelekeni lumumba. Sisi wengine hatuangalii vitu vidogo hivyo. Dini au kabila havimfanyi mtu akawa mchapakazi au mwadilifu. Watanzania kama mnataka maendeleo ya kweli acheni kabisa kuongelea udini na ukabila. Kwanza ni mtu mpumbavu tu atakayewaza ukabila na udini.

Haijatokea bahati mbaya CHADEMA kikawa kina viongozi wa CHAMA karibu wote wanatoka kaskazini, sasa unafikili watu hawalioni hilo? hawalihoji? haya ni mawazo yanayojenga..chama kikikosa sura ya kitaifa ni ngumu kushika dola. hamna mtu anaongelea ukabila hapa, au udini tunaongelea kuimalisha umoja wa kitaifa na kua na vyama vya siasa vinavyojenga huo umoja kwa mifano sio maneno.
 
Kwa muda mrefu nimekua nikifuatilia pilika pilika za vyama vya siasa kuelekea October ambapo utafanyika uchaguzi mkuu, na kupata rais wa awamu ya tano. Kwa mtazamo wangu ukawa watashindwa vibaya na Mh. John Pombe Magufuli. Sababu kubwa ninazoziona ni hizi hapa.
1. Ukawa ikiongozwa na chama kikuu cha upinzani kimekosa sura ya kitaifa
Kwa kiasi kikubwa viongozi wa ukawa hususani chadema kilichotoa mgombea urais kimekosa sura ya kitaifa. Viongozi wengi wa chadema wanatoka kaskazini, hii ni weakness kubwa sana kisiasa,, chama cha siasa kwa mazingira ya Tanzania kama kinataka kuchukua dola ni sharti kiwe chama cha siasa chenye sura ya kitaifa ili kipate support kutoka sehemu mbalimbali ya jamhuri ya muungano.

2. Dhana mfu ya mabadiliko
Kwa mtu mwenye civic competence kubwa na anauwezo mkubwa wa kuchambua mambo atakubaliana na mimi hakuna uhusiano wowote wa maana kati ya kubadili chama ili upate mabadiliko, nakubali kabisa kua na upinzani wenye nguvu ni kitu bora katika kujenga utawala bora lakini uhusiano na mabadiliko ni mdogo au hakuna kabisa. Nitatoa mfano: Japani toka mwaka 1955 kimeongozwa na chama kimoja cha siasa LDP TOKA mwaka 1955 mpaka 1993 kikatolewa madarakani kwa mda wa miezi 11 kikarudi tena madarakani mwaka 1994 mpaka 2009 kikatoka tena madarakani, mwaka 2012 kikarudi tena mpaka leo. LPD ndio chama kilicholeta mabadiliko makubwa ya kiuchumi kutokana na sera nzuri za kujenga uchumi. Chama cha kikomunisti cha China kimekaa mda mrefu sana na CHINA ipo hapo ilipo leo.

Tatizo kubwa la UKAWA ni kudai mabadiliko kwa kuwaaminisha wananchi kwamba CCM ikitoka madarakani maisha yatakua mazuri. Kuna tofauti kubwa ya ahadi, kwa maana ya kuleta mabadiliko na kuja na mikakati mizuri ya kiuchumi na kijamiii ili waaminiwe kuongoza nchi, sera zao hazieleweki na wanatumia matatizo ya vijana kwa kuwadanganya kua maisha yatabadilika CCM ikitoka madarakani.

3. Udhaifu wa Mgombea wa UKAWA
Ukawa nawamgombea urais dhaifu, hana uwezo wa kujenga hoja na haelezi vitu vya msingi ili kujenga uchumi na taifa hili na kuleta hayo “MABADILIKO” Lowassa kwa mda mrefu jukwaani ameshindwa kujieleza vizuri na nimtu anaeonekana ana matatizo ya kiafya, amekua haelezi nini atafanya zaidi ya kuhamasisha vijana wadai mabadiliko, LOWASSA NI DHAIFU SANA KUJENGA HOJA UKILINGANISHA NA JOHN MAGUFULI, hili litawaletea matatizo makubwa mbele ya safari kampeni zikipamba moto c z magufuli anauwezo mkubwa wa kujenga hoja na kuitetea vizuri.

Naomba kuwasilisha.

Meeeen you've said it right.... Magufuli ni jembe na ukimsikiliza anajenga mantiki kupitia hoja zake za Msingi juu ya namna Tanzania aitakayo itakavyo-happen. quite different from huyu mzee..... Mi nasikia anatetea tu anasubiri kutaga October 25th
 
kenya wamebalisha vyama sio chama na uchumi wao juu,tembelea maduka yenu yajumla na supermarket na angalia mtandao wao wa mabenki hapa tanzania......crdb iko nairobi au mombosa?.

China na Singapore hawajabadilisha chama. Sasa unataka tuendelee na mifano? Tatizo hoja iliyoletwa na mtoa mada ni nzito na mna majibu mepesi.
Watanzania wengi tunapenda kuona umoja wetu na tunataka kuona sura ya kitaifa. Sasa hii ni changamoto kubwa kwa Chadema na ilitarajia itakuwa addressed kupitia Ukawa. Cha ajabu Chadema imehodhi Ukawa na kutaka kuwalazimisha CUF (bara) na NCCR waende wanavyoamrisha. Ona majimbo ya kusini walivyoshindwa kuheshimiana.
 
Haijatokea bahati mbaya CHADEMA kikawa kina viongozi wa CHAMA karibu wote wanatoka kaskazini, sasa unafikili watu hawalioni hilo? hawalihoji? haya ni mawazo yanayojenga..chama kikikosa sura ya kitaifa ni ngumu kushika dola. hamna mtu anaongelea ukabila hapa, au udini tunaongelea kuimalisha umoja wa kitaifa na kua na vyama vya siasa vinavyojenga huo umoja kwa mifano sio maneno.

hata kwenye kata za udiwani anatolewa mtu ambaye hajatoka kskz anawekwa aliotoka kskz hii ni shidaaaaaa!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom