Mwana Mtoka Pabaya
JF-Expert Member
- Apr 22, 2012
- 15,117
- 16,506
3. Udhaifu wa Mgombea wa UKAWA
Ukawa nawamgombea urais dhaifu, hana uwezo wa kujenga hoja na haelezi vitu vya msingi ili kujenga uchumi na taifa hili na kuleta hayo MABADILIKO Lowassa kwa mda mrefu jukwaani ameshindwa kujieleza vizuri na nimtu anaeonekana ana matatizo ya kiafya, amekua haelezi nini atafanya zaidi ya kuhamasisha vijana wadai mabadiliko, LOWASSA NI DHAIFU SANA KUJENGA HOJA UKILINGANISHA NA JOHN MAGUFULI, hili litawaletea matatizo makubwa mbele ya safari kampeni zikipamba moto c z magufuli anauwezo mkubwa wa kujenga hoja na kuitetea vizuri.
Naomba kuwasilisha.
Asante kwa hizi ngonjera, Lumumba Elites katika ubora wao. Acha sasa nikueleze UBORA wa mgombea urais wa UKAWA.
Si mtu mwenye kujieleza saaaana kama walivyo Wamasai wengi, yeye ni mtu wa vitendo. Kamuulize yule Engineer aliyejenga jengo lililoanguka na kuua watu Chang'ombe, huyo atakwambia kwa nini Lowassa hana maneno mengi. Kwa kifupi, shida za Watanzania zinaletwa na maneno yasiyo na utekelezaji. Ndugu yangu unayetafuta umaarufu usio na tija: NCHI HAIONGOZWI JUKWAANI.
Mbili, uwezo wako wa kufikiri na kujenga hoja ni mtihani kwako zaidi ya unaoongea nao. Acha nikunukuu halafu uone jinsi ulivyo nyuma kimawazo.
Tatizo kubwa la UKAWA ni kudai mabadiliko kwa kuwaaminisha wananchi kwamba CCM ikitoka madarakani maisha yatakua mazuri. Kuna tofauti kubwa ya ahadi, kwa maana ya kuleta mabadiliko na kuja na mikakati mizuri ya kiuchumi na kijamiii ili waaminiwe kuongoza nchi, sera zao hazieleweki na wanatumia matatizo ya vijana kwa kuwadanganya kua maisha yatabadilika CCM ikitoka madarakani.
Ni wewe yule yule uliyemponda Lowassa kuwa hajielezi vyema jukwaani, na kuwasifia CCM kuwa wanajieleza vyema (pengine matusi ndio ubora kwako, yale ya Mkapa), sasa najiuliza swali kupima akili yako: walichokuwa wanakifanya CCM pale ni nini tofauti na kutoa ahadi? Je walikuwa wanajenga hivyo viwanda hapo au walikuwa wanaahidi kama ilivyo kawaida tangu uhuru wa nchi hii?
Hivi kwa akili yako, Lowassa huyu unayemjua, leo hii akimkamata mfanyabiashara wa mafuta anachakachua DIESEL kwa mafuta ya TAA, atalipeleka suala hilo bungeni likapigiwe kura za ndio kuongeza bei ya mafuta ya taa au huyo muuza mafuta yatamkuta ya yule Engineer wa Chang'ombe?
Hii nchi wala haihitaji maajabu ndugu yangu. Tuna rasilimali za kutosha, tuna watu wa kutosha, ardhi yetu ni nzuri. Anahitajika kiongozi ambaye atafanya kazi na sio kulalamika.