Ushindi si LAZIMA - Kinana

Ushindi si LAZIMA - Kinana

Kigarama

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2007
Posts
2,492
Reaction score
1,239
Asubuhi ya leo wakati akiwa kwenye mdahalo na Dr. Slaa, mdahalo ulioendeshwa na Star tv kwenye kipindi chake cha "tuzungumze asubuhi", Meneja wa kampeni wa mgombea Urais wa Chama Chama Mapinduzi Abdul Rahaman Kinana amesema kwamba ili uchaguzi wa mwaka huu uwe wa haki, huru na kumalizika kwa salama ni lazima kwa vyama vyote vinavyoshiriki vijue kwamba ushindi si lazima.

Sasa ile kauli mbiu yao ya mwaka huu kwamba "USHINDI NI LAZIMA" haina maana tena!!??
 
Asubuhi ya leo wakati akiwa kwenye mdahalo na Dr. Slaa, mdahalo ulioendeshwa na Star tv kwenye kipindi chake cha "tuzungumze asubuhi". Meneja wa kampeni wa mgombea Urais wa Chama Chama Mapinduzi Abdul Rahaman Kinana amesema kwamba ili uchaguzi wa mwaka huu uwe wa haki,huru na kumalizika kwa salama ni lazima kwa vyama vyote vinavyoshiriki vijue kwamba ushindi si lazima.

Sasa ile kauli mbiu yao ya mwaka huu kwamba "USHINDI NI LAZIMA" haina maana tena!!??

Wamekamatwa pabaya hao.

Hapo utasikia mtu atachukuliwa hatua.
 
Kwa kasi hii wanayopelekwa kwa wananchi kuamka, unafikiri wanatumia tena akili zao? Wanakurupuka kurupuka tu hawa, wanabwabwaja hovyo na kuweweseka kwa sana!
 
Meneja wa kampeni wa mgombea Urais wa Chama Chama Mapinduzi Abdul Rahaman Kinana amesema kwamba ili uchaguzi wa mwaka huu uwe wa haki,huru na kumalizika kwa salama ni lazima kwa vyama vyote vinavyoshiriki vijue kwamba ushindi si lazima.

Sasa wapigakura tutamwambia siku ya kupiga kura Kinana na JK wake USHINDI KWA DR. SLAA NA CHADEMA NI LAZIMAAAAAAAA
 
wameishiwa hao ndio maana wanakanusha kauli zao za mwanzoni
 
Kweli, USHINDI sii Lazima kwao - maana wamekuwa wakiufanya lazima katika chaguzi nyingine zote zilizopita maana hawakupata watu makini na wachungu kwa nchi yao'...

Sasa wamekalia miiba, wanatamani uchaguzi uahirishwe...maana wanajua hata wakisabaisha tena sokomoko, watanzania ni makini, Kesi -Mahakama ya Kimataifa itawafuata popote, O' Campo wanamjua vyema...na sasa yupo njiani, hapo Kenya, ni kuvuka mpaka tu...! Wameshaona dalili zote!
 
mwananchi ashapigwa mkwara wa karipio bado waamie kwenye JF..
 
Sasa ile kauli mbiu yao ya mwaka huu kwamba "USHINDI NI LAZIMA" haina maana tena!!??
Mkuu, haikuwa rahisi kwa Kinana kutamka hivyo. Alilazimika kusema hivyo baada ya Dr. Slaa kutoa maana ya kauli "ushindi ni lazima", kwa hiyo Kinana akawa na wakati mgumu, na njia rahisi iliyokuwa imebaki ni kukubaliana na Dr. wa ukweli kwamba Ushindi si Lazima ! Nina wasi wasi jamaa ataitwa na Makamba ili ajibu ni kwa nini amefanya mjadala katika TV na hali CCM ilishawapiga marufuku wanachama wake kushiriki aina yoyote ya mdahalo (kwani ilijua watabanwa na kuongea wasichotarajia kama ilivyomtokea Kinana). Sidhani kama JK atasimama kuongea tena kwamba "ushindi ni lazima" kwani meneja wake ameshamsaliti!
 
Kama wameanza kutafuta wachawi namna hii, mambo sio mazuri kwao! Eti gazeti la mwananchi haliisifu serekali!!
 
Kinana: Sasa, Ushindi si Lazima...............Duh, Hawakutarajia kama waTZ wapole wanaweza kuwageuka kirahisi hivyo.

Watu wamechoka sana na dhuluma na umaskini. wakati tuna kila kitu TZ. MUNGU AMESHAIBARIKI TZ:
 
Wenye akili tulishaona...kwetu nimeagiza familia nzima+++ wampigie dr wa Ukweli SILAAA kura ya ndio....na bahati njema pale kijijin mzee akishauri ni Amri......tehetehetehte.....SISIYEMU OYEEEEEE?????????:mmph::mmph::mmph::mmph::mmph::mmph::mmph::mmph::mmph::mmph::mmph:
CHADEMA...??????///:A S thumbs_up::A S thumbs_up::A S thumbs_up::A S thumbs_up::A S thumbs_up::A S thumbs_up::A S thumbs_up::A S thumbs_up::A S thumbs_up::A S thumbs_up::A S thumbs_up::A S thumbs_up::A S thumbs_up::A S thumbs_up:
 
Asubuhi ya leo wakati akiwa kwenye mdahalo na Dr. Slaa, mdahalo ulioendeshwa na Star tv kwenye kipindi chake cha "tuzungumze asubuhi". Meneja wa kampeni wa mgombea Urais wa Chama Chama Mapinduzi Abdul Rahaman Kinana amesema kwamba ili uchaguzi wa mwaka huu uwe wa haki,huru na kumalizika kwa salama ni lazima kwa vyama vyote vinavyoshiriki vijue kwamba ushindi si lazima.

Sasa ile kauli mbiu yao ya mwaka huu kwamba "USHINDI NI LAZIMA" haina maana tena!!??

mweeeee!!!!!!!!!!!!!!! hata mimi nashangaa.hivi jamani mbona hawa watu wanajikanyagakanyaga hivi? "UKIWA MUONGO UWE NA KUMBUKUMBU.Hawa watu wanasahau waliyokwishayasema awali ndo maana tunatakiwa tuwasamehe bure.kukataliwa kubaya jamani.
 
Kinana (Kindizi) lazima ataitwa kujieleza. Nina hakika atakanusha jioni hii. Kamata singo yake, weweeeeee... tamu hiyo.
 
Nakuhakikishia kwamba atasema amenukuliwa vibaya si unajua ubabe wa sisiem
 
Alienayo hii historic video ya mdahalo huu wa mwishoni mwishoni aweke kweney you tube tuchambue kuchanganyikiwa kwa ccm
 
Alie nayo hii historic video ya mdahalo huu wa mwishoni mwishoni aweke kweney you tube tuchambue kuchanganyikiwa kwa ccm

Leo saa tano usiku mdahalo huo utarudiwa (replayed) tena Star tv. kwa wale wenzangu na miye ambao hatujauona asubuhi ya leo basi tukeshe tujipakulie wenyewe.
 
Kinana: Sasa, Ushindi si Lazima...............Duh, Hawakutarajia kama waTZ wapole wanaweza kuwageuka kirahisi hivyo.

Watu wamechoka sana na dhuluma na umaskini. wakati tuna kila kitu TZ. MUNGU AMESHAIBARIKI TZ:
Kwa matamshi ya Kinana nadhani wao wameshaona kwamba wanashindwa lakini lengo lao ni kupotosha matokeo ya kura zitakazopigwa. kama wao walishachapisha vipeperushi vyao na kusema kwa hakika kabisa kwamba "USHINDI NI LAZIMA" kwani kimetokea nini hadi waanze kuvisihi vyama vingine kukubali "kushindwa" kama wao hawana nia mbaya ya kuiba kura?
 
Angalia alivyokuwa amekaa unajua kabisa kuwa wameshakata tamaa... Body language yake inasema kila kitu..

Wameshaonywa na OBama kuwa wasivuruge hali ya watanzania na amani yetu kwa tamaa ya madaraka.

Walisema ushindi ni lazima leo imekuwa siyo lazima sasa tuwaeleweje... Makaratasi yameshikwa Tunduma hali ni tata na ni aibu ya serikali...

Sisi wana Slaa tunasema Chadema ushindi ni lazima...
 
Back
Top Bottom