Ushindi mtamu ni ushindani katika uwanja sawa, sio ule wa mezani. Magufuli, kasi yako ni ushindi wa kishindo. Ruhusu ushindani wa haki, sawa na wazi

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,896
114,609
Wanabodi,

Tangu kuanza kwa pilika pilika za uchaguzi wa Serikali za Mitaa, sijawahi kuzungumza lolote kuhusu uchaguzi huu kutokana na kuwa bize na shughuli za kitaifa, kwanza ni Wiki ya Msaada wa Kisheria iliyofanyika kitaifa mjini Bariadi Mkoani Simiyu na kufuatiwa na Wiki ya Azaki iliyomalizika jana Jijini Dodoma, hivyo leo ndio nimepata fursa kuendelea na zile makala zangu za " Kwa Maslahi ya Taifa".

Mada kuu kuhusu makala ya leo ni hizi figisu figisu za uchaguzi serikali za mitaa zinazoendelea na zilizopelekea Chama kikuu cha upinzani kwa huku bara, Chadema, kujitoa kikifuatiwa na Chama cha ACT Wazalendo kwa hoja za kutotendewa haki. This is not good at all kwa mustakabali mwema wa taifa letu, kwasababu kama ni kweli hawakutendewa haki, machozi ya kilio cha haki husababisa a very bad karma kwa taifa letu, na ubaya wa karma sio tuu inaweza ku hit taifa letu kama taifa, lakini karma ina tabia ya ku hit kwa baadhi ya viongozi individuals if they have a hand kwenye yanayotokea.
Hapa naomba kukumbusha tena kuhusu ile sauti nilio isikia kuhusu uendeshaji wa chaguzi zetu, nikatoa ushauri huu Ombi Maalum, Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa 2020, Uendeshwe kwa Ceteris Peribus, Sio Kwa Mutatis Mutandis. Tutabarikiwa!

Sitaki kuingia ndani kwenye technicalities zilizopelekea wagombea wa upinzani wote kuenguliwa, bali natoa wito kwa rais Magufuli aingilie kati hali hii au yeye mwenyewe kama rais wa JMT, au kupitia kwa msaidizi wake Waziri Jaffo wa Tamisemi, ayafumbie macho makosa yote madogo madogo ya wagombea wote wa vyama vyote vya upinzani walioenguliwa kwa sababu zozote, ziwe ni za kweli za halali au ni figisu tuu, ayafute na watoe a general amnesty ya jumla kwa kila aliyegombea apitishwe tuu hivyo hivyo despite all the odds ili Tanzania tuingie kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu mwakani kwa ushindani wa haki, uwazi na usawa kwa vyama vyote kutendewa haki sawa, kwa demokrasia kuachwa kufuata mkondo wake, hivyo hawa waliosusa wote kwa kuweka mpira kwapani warudi uwanjani kipute kipigwe mechi ichezwe watu washindane.

Ushindi mnene, mnono, mtamu wa raha ni ule ushindi unaotokana na kupatikana kwa ushindani halali wa haki unaopatikana na kuendeshwa kidemokrasia kwenye uwanja ulio sawa, a level playing ground na sio ushindi wa uwanja tenge!, wala sio ushindi wa mezani!. Ushindi wa dhulma, unabeba a bad karma repercussions, hivyo ukifika muda wa karma pay back time, mtashangaa tuu watu wanapukutika, bila kujua sababu kumbe ni karma inakula vichwa!.

Kwa observation yangu, kwa kasi ya rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli, JPM, kwa haya tuu aliyowafanyia Watanzania kwa miaka hii minne tuu tangu alipoingia madarakani, na mambo anayoendelea kuyafanya kila uchao, ni mambo mkubwa kuliko rais mwingine yoyote aliyewahi kufanya, ukimuondoa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliyetupatia uhuru na kutujengea umoja, usawa, upendo na mshikamano miongoni mwa Watanzania kama binadamu wote ni sawa kwa kuwa kitu kimoja, Taifa moja lenye umoja, lisilo na ubaguzi rangi, udini, ukabila, jinsia na hali, hivyo Rais Magufuli na CCM inakwenda kushinda a clear victory ya ushindi wa kishindo cha wazi wa over 90%!, hivyo hakuna haja wala sababu yoyote za kutumia figisu figisu zozote!.

Kutokana na kasi ya rais Magufuli kutuletea maendeleo ya vitu vya kuonekanika, kuhamia Dodoma, Midege, Reli ya SGR, Mabarabara nchi nzima, madaraja ya juu kwa juu, mradi wa umeme wa Stigler's, Tanzania ya viwanda, elimu bure, vituo vya afya, zahanati na mahospitali kila kona, etc, etc, just to mention but few, vinaipa CCM fursa ya ushindi wa kishindo cha wazi kabisa katika uchaguzi wowote huru na wa haki nchini Tanzania kati ya sasa hadi 2025, hivyo mamlaka zinazosimamia uchaguzi huu, waruhusuni wagombea wote wa vyama vyote waliopitishwa na vyama vyao wapite tuu bila kujalisha kama wanekidhi sifa na vigezo, ili tuu kuruhusu ushindani wa haki, ushindani wa uwazi na Uchanguzi wa kidemokrasia huru na wa haki na mshindi apatikane kihalali, ki haki, ki demokrasia kupitia uchaguzi huru na wa haki!.

Nakumbuka wakati naanza kujenga familia nilipokuwa Baba Kijana, nilikuwa nikicheza na watoto wangu michezo mbalimbali kama mashindano ya kukimbia, mnashindana kukimbia, ili kumjengea mtoto ari ya kushinda, wewe unakimbia mdogo mdogo ili usimshinde mtoto ukamvunja moyo, unamuacha mtoto akupite na akushinde na akiisha shinda, mtoto anafurahi kweli kweli kuwa amemshinda baba!.

Hivyo tukubali tukatae, kwa hali ya sasa ya siasa za nchi yetu Tanzania kwa hii kasi ya JPM, Magufuli ni game changer wa the political dynamics za siasa za nchi yetu, ambapo rais Magufuli akiendelea kutawala, CCM itakomba kila kata, na kila jimbo!, hivyo ili Tanzania tuendelee kuwa ni nchi ya vyama vingi, kuna maeneo CCM inabidi tuu ijifanye kama baba anayecheza na watoto wake kwa kuwaachia tuu watoto washinde, yakiwemo majimbo uanayogombewa na wenyeviti wa vyama vikuu vya upinzani, majimbo ua Mbowe, Mbatia, Mrema, Zitto, Lipumba, Cheyo etc vinginevyo uchaguz Mkuu wa mwakani, 2020, Tanzania tunarudi kuwa nchi ya chama kimoja!.

Hivyo natoa wito kwa serikali ya CCM, chini ya Jemedari wake, JPM, kiukweli labisa, hata kabla ya uchaguzi, CCM tayari imeishashinda kwa ushindi wa kishindo sio tuu huu Uchanguzi wa Serikali za Mitaa, bali hadi Uchanguzi Mkuu ujao wa mwakani 2020 kutokana na sababu za ki political social dynamics ya Magufulification nilizoeleza lakini ili CCM iweze kuufurahia huo ushindi kwa furaha ya kweli na hivyo kusheherekea ushindi huo, lazima CCM ishinde kwenye ushindani wa kweli, ushindani wa haki na ushindani wa usawa na sio kupata ushindi kwa kufanya figisu ili washindani wako wasuse, watie mpira kwapani na wewe upewe ushindi wa mezani!. Ushindi wa hivi sio ushindi mtamu, wala hauleti raha ya kudumu kwasababu karma itaingilia kati kuja kuikatisha hii raha kwa kula vichwa!.

Nakuomba Rais Magufuli na Waziri Jafo, jifanyeni kama mnacheza na watoto, kwanza wafungulieni njia watoto wote washindane kwa haki, washiriki kwenye uchaguzi huu na wa haki kwa uhuru na kwa haki sawa kwa vyama vyote despite mapungufu walionayo ili hata uchaguzi Mkuu wa mwaka kesho, wakati Watanzania watakapo irejesha Tanzania kwenye mfumo wa Chama kimoja CCM, iwe ni Watanzania wenyewe ndio wameamua kuichagua CCM kwa haki kupitia uchaguzi huru na wa haki ulioendeshwa na Tume Huru na Shirikishi ya Uchaguzi ulioendeshwa kwenye uwanja sawa na tambarare wa ushindani, na sio CCM ishinde katika ule ushindani wa kugombea kisu cha makali kuwili, huku mshindani mmoja ameshika kwenye mpini na mshindani mwingine kwenye makali. Hivyo CCM ishinde kihalali kwa kufuatia kazi nzuri ya rais JPM na serikali yake na sio kwa sababu CCM ndio iliyokamata mpini!

Tena kwa maoni yangu uchaguzi huu wa serikali za mitaa unaosimamiwa na TAMISEMI ndio uwe wa mwisho kusimamiwa na Tamisemi, tubadili sheria zetu za uchaguzi, uchaguzi zote zisimamiwe na sheria moja, chini ya Tume Huru na Shirikishi ya Uchaguzi, zuio la mikutano ya siasa liondolewe, wagombea huru waruhusiwe ili hata watu kama akina sisi wenye vyama tujitoe na kusimama as independent candodates tuweze kushiriki kugombea, hivyo uchaguzi wa 2025 tuchague viongozi wa serikali za mtaa, madiwani, wabunge na rais kwa siku moja. Hoja kuwa zitakuwa kura nyingi haina mashiko. Kwenye uchaguzi Mkuu wa Zanzibar kila mpiga kura anapiga kura 5 kuchagua
  1. Diwani, Shehia
  2. Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi
  3. Mbunge wa Bunge la JMT
  4. Rais wa Zanzibar
  5. Rais wa JMT
Hivyo Tanzania tukiamua kufanya uchaguzi huru na wa haki, unaofuata mfumo wa uchaguzi wa kidemokrasia ya ukweli, tunaweza. Mimi naamini kabisa kwa mambo makubwa na mazuri ya Rais Magufuli anayoyafanya, we have nothing to loose rais Magufuli akiruhusu demokrasia ikashamiri, akatoa haki sawa kwa vyama vyote kufanya siasa ikiwemo kuondoa zuio batili la mikutano ya siasa, bado rais Magufuli anaweza kuyaleta maendeleo yote aliyo yakusudia at the same time huku akiruhusu demokrasia nayo ikashamiri, ila ukweli utaendelea kubaki ni ukweli daima kwa katiba hii, Tume hii, sheria hii ya uchaguzi na kasi hili ya rais Magufuli, CCM bado itaendelea kutawala Tanzania kwa miaka mingi ijayo, kama sio milele!.

Naomba nimalizie kwa ile kauli ya thread hii
"Ushindi Mtamu ni ushindi unaopatikana kwa ushindani wa haki kwenye uchaguzi huru na wa haki, unaaendeshwa na Tume huru na shirikishi ya uchaguzi na unaofanyika kwenye uwanja sawa wa ushindani wa kisiasa, sio huu uwanja tenge tulionao, na kupata ushindi wa mezani!.

Mheshimiwa Rais, wetu, Dr. John Pombe Magufuli, aka.JPM, kasi yako ya maendeleo ya Tanzania unaoifanya, ina ku guarantee utailetea CCM ushindi safi wa kishindo cha halali katika uchaguzi wowote, tunakuomba sana!, sana!, sana!, "Please! Please! Please!, ruhusu tuu ushindani wa haki, wazi na usawa kwa vyama vyote, kushiriki uchaguzi kwa uhuru na haki sasa kwa wote!, utabarikiwa zaidi na zaidi, na Tanzania tutabarikiwa!, ukiruhusu hizi figisu zinazoendelea, hazina hatima njema kwako, kwa chama chako wala kwa nchi yetu, kwasababu kuna lijamaa fulani linaitwa karma'hilo linataka haki bin haki!, usipotenda haki, lenyewe linaingiliaga kati na halijuagi cha nani wala cha nini!, lenyewe ni haki haki tuu bin haki usipotenda haki!, karma itaingilia kati, na kwa vile no one knows what karma will do, it's better kutenda haki kuiepuka adhabu ya karma !.

Nawatakia Jumapili Njema
Na mimi nawahi kanisani
Misa ya Kwanza pale kanisa langu la St. Peters

Paskali
 
Paskali,

"Law of probability," inakataa kuwa katika makundi mawili mathalan yanajaza form zilizo sawa na wajazaji wa makundi hayo wawili wanafanana kwa kila hali katika sifa zao pakawa makosa yawe yanafanywa na kundi moja tu.

Hili kisayansi haliwezekani kabisa kwa asili 100.

Lakini tujaalie kuwa hili limewezekana ingawa sijui "control" gani itumike.

Tatizo litakuwa limehamia kwenye "Law of Probability," itabidi sheria hii yenyewe iangaliwe upya ili paweze kupatika maelezo na huu si utafiti mdogo.

Kwa ajili hii basi ya hayo niliyoeleza hapo juu hivyo vifungu vya sheria havina maana yeyote ikiwa utatumia, "Law of Probability," nikikusudia sayansi namba kutegua tatizo hili.

Kwa nini basi hayo yametokea?

Jibu ni kuwa kutakuwa na, "intervening cause."

Sasa hapa mwanasayansi uwanja ushafunguka atakapofikia kujua hili katika utafiti wake kitakachofuatia ni kutafuta sababu ya matokeo haya ya makundi mawili yaliyo na sifa sawa lakini moja lijitokeze na kuonekana hodari na hili lingine liwe "mbumbumbu," limesheheni watu wajinga hawawezi hata kujaza taarifa nyepesi za majina na anuani za nyumba zao wenyewe wanazoishi miaka na miaka.

Hawa "mbumbumbu," kwa miaka mingi wamekuwa viongozi katika jamii wakiwaongoza watu.

Hapa yanahitajika maelezo.
 
Pascal, hayo unadhani yametokea kwa bahati mbaya?

Unamuomba waziri Jafo ambaye juzi kasema ''figisu' ni jambo la kawaida

Kurudisha waliokatwa si suluhisho, wanaweza kurudishwa, kura zikahesabiwa ''kilatini''

Kinachotakiwa ni ushindi wa asilimia 98 kwenda mbele, na hiyo haipatikani bila ''namna''

Hivi kama mambo yanafanyika vema, maendeleo yanaonekana kwa wananchi hii hofu ya uchaguzi inatoka wapi? Inasababishwa na nini? Nini kinawafanya waogope wapinzani?

Ili kuokoa rasiliamali za wananchi, Waziri atangaze matokeo yoyote anayojua!
 
Hilo la ushindani wa haki, sawa na uwazi haliwezi kutokea kwa serikali hii kwa sababu ni serikaki iliyojikita kwenye uongo na propaganda, hivyo kuweka uwazi na usawa ni kwamba unataka hii serikali ife.

Serikali isiyotaka challenge ni serikali ya hovyo sana.

Hii ni serikali inayotaka ikisema inajenga reli kwa pesa za ndani basi mtu asitokee kuhoji hizo pesa za ndani ni zipi kama makusanyo tu hayatosho kulipa madeni ya mikopo, mishahara na matumizi mengine, inataka ikisema ni pesa za ndani kila mtu akubali, ukihoji mbona deni la taifa linakua hizo pesa za ndani ni zipi utaitwa sio mzalendo,utapewa kesi ya kua sio raia.

Serikali inayotaka ikipika takwimu mtu asitokee kuzichallenge, ikisema umasikini umepunguankwa 80% kila mtu akubali, hakuna kupinga wala kuuliza maana akili za kuhoji sio za wazalendo wa nchi hii, wazalendo wa nchi hii wao ni kukubali kila kitu.

Mimi nashauri hata mwakani vyama vingine vya siasa visishiriki uchaguzi serikali ya wanyonge ishinde kwa kishindo maana ndio lengo lao hivvyo wasaidiwe kutimiza lengo lao.
 
Waziri Jaffo yupo katika wakati mgumu, linalokuja kinywani analitamka halafu anafikiri baadaye.

Alipoambiwa kuna matatizo ya kucharangana mapanga na kunyimwa fomu, waziri kasema ''kila uchaguzi una figisu pote duniani''

Yaani anakiri kuna matatizo halafu anayajengea uhalali wa dunia bila kujali madhara yake

Waziri kasema waliokosea kujaza fomu wameenguliwa kwa mujibu wa sheria.

Sheria inampa haki ya kuwaengua halafu anavunja sheria ya kuengua kwa kuweka majina yao!

Waziri anaelewa hakuna mgombea binafsi anaruhusiwa.

Kwa mantiki hiyo waombea wanapitia vyama vyao vinavyowadhamini.

Sasa wadhamini wamejiondoa hayo majina anayobandika ni ya wagombea binafsi?

Anachotaka ni majina ili kuhalalisha ushindi. Hana sababu za kuhangaika hivyo!

Wapinzani wamerahishia kazi, wamejitoa wenyewe!

Yeye atangaze tu namba yoyote inayokuja kichwani. Muhimu aweke %
 
Yani CCM wangesoma case study ya Gaddafi،aliwafanyia kila kitu ila aliwaminya katika uhuru wao. Kwahiyo yote mazuri hayakuonekana na wakamuua.

Sasa reli, madaraja, mabarabara hayataonekana katika hizi figisu.

Kuna tetesi za ugonjwa badala ya kusikitika watu walifurahi hio ilokua indicator mbaya. Hatujifunzi. Owky hakuna marefu yasio na mwisho.
 
Pascal kiukweli pamoja na yote jpm aliyoyafanya uliyoyataja hapo huyu mtu HAKUBALIKI, na hili yeye mwenyewe analifahamu fika na watu wake Serikalini, na pale Lumumba wanalifahamu fika.

Sasa vigisu zote hizi za nini basi.. anajua fika kwenye free and fair election (ambayo kwanza haipo) kwenye Uchaguzi unaosimamiwa na TAMISEMI ambayo ipo Ofisi yake atashindwa tu.

Ndio chanzo cha kufanya ujinga wote huu.

Niliwahi kuandika huko nyuma, naomba niandike tena hapa, wagombea Urais wa Nchi wawe seriously wanapimwa AFYA ya akili kabla ya kupitishwa na NEC. Nchi inaweza kuongozwa hihivi na KICHAA.
 
Back
Top Bottom