Ushindani huru kwa walimu wa serikalini

Mkola Tz

Member
Sep 10, 2021
15
14
Kulingana na ongezeko la walimu wengi kuwepo mtaani serikali ingechukua hatua stahiki katika kuendeleza sekta ya elimu hapa nchini. Kwa kuja na mikakati Bora zaidi ya kukuza sekta hiyo hii inatokana uzembe uliopo kwa baadhi ya wa walimu hasahasa shule za sekondari. Kwani imekua Kama mazoea mwalimu wa somo husika wanafunzi wakifeli hashtuki kwa lolote na serikali haimchukulii hatua zozote zile hivyo na huwaambia wanacunzi "nyie hata mkifeli Mimi mshahara wangu utabaki pale pale."

Katika kuchukua hatua stahiki kwanini serikali isianzishe huru kwa walimu waliopo tayari kwenye ajira. Endapo mwalimu wa somo husika akiongoza kwa kufelisha katika somo lake kwenye mitihani kitaifa aletwe mwingine wa kuchukua nafasi yake.

Kwa kuangalia taasisi za elimu za shule binafsi endapo mwalimu wa somo husika atashindwa kufaulisha wanafunzi katika Hilo somo lake huondolewa shuleni hapo, kwa kuangalia dhana kwanini serikali isianzishe ushindani huru wa namna hii ukizingatia Kuna wimbi kubwa Sana la walimu waliopo mtaani hawana ajira.

Ushindani huu utasidia kuinua sekta ya elimu hapa nchini, hata hivyo njia hii ingewagusa walimu wa sekondari kwani hapa ndio Kuna idadi kubwa ya wanafunzi wanao feli sana. Kwani endapo mwalimu ambae atashika nafasi ya mwisho katika somo lake atakaa akijua kwamba nafasi yangu itakuja kuchukuliwa na mtu mwingine.

Hii itasaidia kwa walimu waliopo kazini kuongeza bidii katika ufundishaji, kutokua wazembe, wavivu, kujiingiza katika shughuli nyingine ambazo huwabana kuingia darasani kwa wakati na kususia vipindi. Hivyo Basi ushindani huu utachangia maendeleo makubwa katika sekta ya elimu yetu hapa nchini.
 
Back
Top Bottom