6 Pack
JF-Expert Member
- Apr 17, 2022
- 3,653
- 8,000
Niaje waungwana
Ni nature kwa kila binadam kufa au kufiwa. Nikimaanisha kuwa kila mwana JF anaesoma, na asiesoma thread hii including myself tutakufa, tutafiwa au pengine tayari wengine tumeshafiwa.
Sasa kwa wale ambao tumeshawahi kufiwa na wapendwa wetu mfano mzazi, mke, mume, mtoto, ndugu au rafiki, kuna hali fulan ya maumivu humtokea mfiwa. Na hali hii hutokea kama yule aliekufa alikuwa ni mtu wako wa karibu uliempenda na yeye akakupenda, uliemthamini na yeye akakuthamini, uliemjali na yeye akakujali, na sometimes uliemtegemea na yeye akakutegemea.
Binafsi nimeshafiwa na ndugu zangu wa damu akiwemo mzazi. Vifo vyao viliniumiza sana lakini naweza kusema kwamba kifo cha marehemu mdogo wang ndio kimeniumiza zaidi na mpaka leo siwezi kupitisha mwezi au week 2 sijamuwaza au kumuota.
Huyu mdogo wang ni mtu ambae kiukweli tulipendana, tuliheshimiana, tulisaidiana na kujaliana sana. Alikuwa hawezi kufanya jambo lake la maana bila kuniomba ushauri. Na mimi pia ilikuwa ni hivyo hivyo.
Hata wazazi wetu sometimes walipotaka wamwambie dogo jambo lolote la serious, ili akubali ilibidi sometimes wapitie kwangu ili iwe rahisi jambo hilo kulikubali.
Dogo alikuwa fundi mekanika mzuri sana kiasi ya kwamba mpaka baadhi ya watumishi wa serikali, including viongozi wa jeshi walikuwa wanaleta magari kwake awatengenezee.
Siku mbili kabla ya kifo chake alinipigia simu kuniomba ushauri, kwamba kuna mteja wake mmoja (mjeshi) alimuomba waende nae bagamoyo wakachukue mkaa ili walete Dar kuja kuuza.
Kwanza nilisita kwa sababu huko wanapokwenda ni mbali na yeye ana mke tena mjamzito. Lakin pia niliogopa watu wa maliasili wanaweza kumkamata na kumfunga kutokana na kutokuwa na vibali vya biashara hiyo. Ila dogo akanambia kwamba mmiliki wa gari hilo ni mjeshi mwenye cheo cha kanali, hivyo haitokuwa rahisi yeye kukamatwa na maliasili yeyote, ukizingatia na mjeshi mwenyew atakuwa ndani ya gari.
Kusikia hivyo nikaafiki ila nikamwambia awe makini barabarani maana gari itakuwa imebeba mzigo mkubwa, akasema poa.
Safari ikafika dogo na mjeshi wakaingia Bagamoyo. Kweli walifanikiwa kupata mkaa wakajaza fuso na kuanza safar ya kurudi Dar. Ilikuwa usiku kama mida ya saa 4 hivi. Walivyofika karibu na mpaka wa Mkoa wa Pwani na Dar, gari ikapata pancha.
Dogo kwa vile ni fundi akaegesha gari pembeni ya barabara akatoa jeki na kuanza kupiga ili wabadilishe tairi. Walikuwa na spea tairi ndani ya gari hivyo dogo akatoa pancha akaweka zima. Ile ashamaliza kufunga anashusha jeki huku yule mjeshi akiwa amemshikia tochi ili aone vizur, ghafla bodaboda hata ilipotokea haijulikani akawapitia wote wawili, yani dogo na mjeda.
Ajali ile ikasababisha watu wajae kuangalia kuna nini. Wakati huo mjeda alikuwa hajitambui, bodaboda nae kazimia, ila mdogo wang yeye alikuwa fresh. Ni kama vile hakuguswa na kitu.
Baada ya pilika pilika za hapa na pale trafiki wakafika na kuchukua maelezo ambapo dogo ndio alikuwa anampa yule trafiki maelezo, na kueleza kuwa mmiliki aliekuwa pale chini ni afisa wa jeshi.
Hivyo ikabidi ifanyike juhudi za kuwawahisha hospital ya wilaya ya Bagamoyo yeye (mjeshi) na bodaboda huku dogo akiendesha lile gari akifuatana na trafiki hadi hospital kuandika maelezo.
Baada ya maelezo, yule mjeda ikaonekana hali yake sio nzuri hivyo inabidi awahishwe hospital ya jeshi Lugalo mara moja, na yule bodaboda nae apelekwe muhimbili. Mpaka hapo nyumbani tulikuwa hatujui kinachoendelea japo mimi nilikuwa naifahamu hiyo safari yake ya Bagamoyo.
Mida ya saa 7 usiku akanipigia sim kunijulisha kilichotokea, nikamuuliza kama yeye kwa upande wake yupo salama, akasema yeye yupo salama salmin, japo alichubuka kidogo mguuni lakini washamuweka dawa anataka apumzike pale Hospital, kisha asubuhi ndo ataanza safari ya kuja Dar. Kumbuka hapo ilikuwa ni saa 7 usiku, hivyo ilibaki masaa ma4 tu kupambazuke, ndomaana akaona bora alale tu pale kisha asubuhi aanze safari. Nikamshauri asimwambie kwanza mkewe kuhusu hiyo ajali mpaka atapofika nyumbani ili asije akampa wasiwasi na ukizingatia mkewe ana mimba.
Dogo akaniaga fresh nikakata simu na kulala.
Asubuhi mapema nilipoamka nikachukua sim kumpigia ili kujua ameamkaje, na safari ameshaanza au bado. Sasa kila nlipopiga sim ilikuwa inaita tu ila haipokelewi. Nikajua labda bado analala au anaendesha gari so anaogopa kupokea asifanye ajali nyingine.
Ilipofika mida ya saa 2 asubuhi nikaona anapiga sim nikapokea haraka haraka, ila nilichokisikia sitokuja kukisahau. Yani nilisikia sauti ya mtu mungine ambayo iliniambia kuwa mdogo wangu alifariki asubuhi ya siku ile, yani alifariki saa 10 ya asubuhi baada ya hali yake kugeuka ghafla. Inasemekana aliumia ndani kwa ndani bila mwenyewe kujua.
Aisee nilihisi kama jamaa anatania nikamwambia naomba niongee na mwenye sim mwenyewe. Jamaa akanambia utaongea na mwenye sim gani wakati ameshafariki. Japo sikuamini ila ikabidi nipige sim kwa mzee kumuelezea kilichotoea. Hata mzee nae alishtuka sana kwa habari ile. Ila tukapanga tuanze safari ya kuelekea Bagamoyo ili kwenda ku confirm kama kile nilichoambiwa ni kweli au stori.
Baada ya kufika hospital kujitambulisha tukapelekwa monchwari kuhakikisha na kuthibitisha kama ni yeye kweli au wamejichanganya. Aisee tulipoingia na kuoneshwa maiti ya mdogo wang akiwa amekaushwa na balafu na wakati masaa kadhaa niliongea nae, nilitaka kuumwa kichaa, ilibidi nikamatwe na kupelekwa katika chumba fulan ambapo nilipewa vidonge vya usingizi. Nilipoamka kuna ndugu wengine walikuwa wameshafika ikabidi tufanye mpango wa kurudi na maiti nyumbani kwa ajili ya mipango ya mazishi.
Ni miaka 8 sasa imepita ila picha yake haifutiki kichwani kwangu.
Je wewe ushawahi kufiwa na mtu wako wa karibu ambae mpaka leo haujasahau ulivyoumizwa na kifo chake?