SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 5,146
- 7,909
Mpaka sasa katika hatua ya makundi hakuna matokeo ya Yanga ambayo yamekuwa tofauti au ya kushangaza sana tofauti na yale tuliyoyatarajia. Labla yale ya kushindwa kupata point 3 kutoka kwa Medeama kule Ghana. Kutoka suluhu na mwarabu kwa Mkapa si matokeo ya kushangaza, Yanga alihitaji ushindi katika mechi ile kama ambavyo Al Ahly alihitaji sare.
Kundi la Yanga lilikuwa linatabirika na mpaka sasa limevurugwa na mechi moja tu, ule ushindi wa Medeama dhidi ya CRB na ndiyo ambacho kimekuja kuipa matumaini Yanga mpaka sasa.
Yanga ikielekeza nguvu kule shirikisho, kwa kikosi ilichonacho na wakiongeza nguvu maeneo machache wana nafasi ya kufanya vizuri kutokana na aina na quality ya timu zilizoko kule. Huku Klabu Bingwa kuna wenyewe na wenyewe ndiyo sisi.
Shida ni kwamba kwenda shirikisho inabidi ipunguze nguvu kwenye kutafuta ubingwa wa NBC na wakati mwingine ijipige shoti ishike nafasi ya 3 au ya 4 ili iwe inadondokea huko Shirikisho kwa sababu kuna dalili zote Simba itaendelea kuipatia Tanzania nafasi za kutosha kimataifa.