Ushauri: Watoto wametugombanisha

Ushauri: Watoto wametugombanisha

habari wanajamvi, aisee ugomvi wa watoto siyo wa kuingilia, kuna siku mwanangu RIZUGE wa miaka minne alikuja kunishtakia kuwa amepigwa na mwenziwe PIZAULO ambaye umri unakaribiana. mimi kwa hasira na uchungu wa mwana nikaenda kumzaba kibao yule mtoto wa jirani aliyempiga mwanangu. baba yake Pizaulo hakukubali na ikapelekea ugomvi mkubwa sana kati yetu sisi watu wazima, cha ajabu jana nimemkuta mwanagu Rizuge na mwenziwe Pizaulo(yule mtoto aliyempiga) wakicheza pamoja!!!, yaani wakati sisi wakubwa hatuongei lakini wao washapatana wanacheza. je sisi wakubwa tuendelee kuchuniana?.
Ndio shida ya kua na fafafafaaaa huwezi kubebeka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huna akili wewe
 
Umewakuta Rizuge na Pizaulo washapatana, lakini hutaki kuamini kuwa aliyewapatanisha ni Baba yake Pizaulo, bila kuja kupatana na wewe kwanza!

Steve Jobs - Giant Of Technology.
 
Kupatana sio kushikana mikono tuu, ni ya moyoni zaidi. Haya tuone kama wataendelea na ushirikiano, wakiendelea vyema sana.
 
Nimesoma, sio kuchuniana tu, ningehama hata hapo, siwezi kaa na mtu anayemwazibu mtoto wangu kijinga hivyo kwa ajili hiyo. Yani wewe umetumia judgement ya mtoto kuchukua action, ina maana Baba yake naye alipoenda mwambia angekuwa mtu mwenye tabia yako angekuja kukupiga wewe au mke wako? just imagine....
hujanielewa,mleta maada anamaanisha ruge vs bashite.
 
Mwalimu wao wa darasa amewalazimisha RIZUGE NA PIZAULO kupatana ili waweze kucheza na kusoma kwa pamoja.
Nadhani lengo la mwalimu ni kutaka kumtumia Rizuge, kumsaidia Pizaulo kwenye somo la kuonekana, Mahudhurio ya Pizaulo darasani ni mazuri ila kwenye somo la kuonekana anafeli kila siku.

Hapo wazazi sijui mtatumia mbinu gani, kujipatanisha na kujiongelesha tena.
 
Huyu jamaa hapa anamuoengelea PAUL MAKONDA NA RUGE...NYIE MNA COMENT TU...ANAWAENJOY
 
Ukiambiwa ruge na makonda ndo watauona ufalme wa mbinguni hiyo ndo maana yake ukiweza kujifunza kutoka kwa mtoto basi ujue utakuwa na moyo safi sana in fact wazazi tunapoanza kuwapangia pangia watoto cha kufanya ndo uwaga tunaharibu kabisa furaha zao..una machuki yako unaanza kumuambukiza na mtoto namna ya kuishi matokeo yake nae anakuwa na michuki kama yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kanuni:-

Ugomvi wa Watoto hauingiliwi hata siku moja
 
Nimesoma, sio kuchuniana tu, ningehama hata hapo, siwezi kaa na mtu anayemwazibu mtoto wangu kijinga hivyo kwa ajili hiyo. Yani wewe umetumia judgement ya mtoto kuchukua action, ina maana Baba yake naye alipoenda mwambia angekuwa mtu mwenye tabia yako angekuja kukupiga wewe au mke wako? just imagine....
Mkuu bado hujasoma between the lines, some comments za members ujue hao watoto ni Akina Nani.
Read between the lines mkuu
 
Mkuu hao watoto hawakupatana kwa hiari yao,.
Wamelazimishwa kupatana na mwenyekiti wa Mtaa
 
WEWE NI WA KUFUNGA KABISA, UNAPIGAJE KIBAO MTOTO ASIYE KUWA WAKO? HUYO MTOTO ANGEKUWA WANGU MIMI WALA NISINGEKUFANYA KITU, NI KITUONI TU .. NA UNGEINGIA KWENYE SHIDA, MIMI SIWEZI PIGA MTOTO ASIYE KUWA WANGU, WATOTO WANA MAMBO YAO MENGI SANA .....
Fact
 
Umenikumbusha hata mimi iliwahi kutokea nilipigwa na mtoto mwenzangu aliyekuwa ananizidi umri kidogo, mlezi wangu alimfokea yule mtoto mama yake akaingili si wakaanza kuporomosheana matusi na kuanzia siku hiyo hawakuongea tena japo walikuwa ni marafiki wakubwa...wakatupiga stop na sisi kucheza pamoja ila tukawa tunacheza kwa kuibia maana mkionekana kila mtu kwao ataenda kulamba stick. Ugomvi wa watoto sio wa kuingilia kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom