hiram
JF-Expert Member
- Aug 1, 2013
- 267
- 394
Habari wanajamvi,
Aisee ugomvi wa watoto siyo wa kuingilia, kuna siku mwanangu Rizuge wa miaka minne alikuja kunishtakia kuwa amepigwa na mwenziwe Pizaulo ambaye umri unakaribiana. Mimi kwa hasira na uchungu wa mwana nikaenda kumzaba kibao yule mtoto wa jirani aliyempiga mwanangu.
Baba yake Pizaulo hakukubali na ikapelekea ugomvi mkubwa sana kati yetu sisi watu wazima, cha ajabu jana nimemkuta mwanagu Rizuge na mwenziwe Pizaulo (yule mtoto aliyempiga) wakicheza pamoja, yaani wakati sisi wakubwa hatuongei lakini wao washapatana wanacheza.
Je, sisi wakubwa tuendelee kuchuniana?