zito nakushauri urudi ccm na ukagombee ubunge kwa kupitia huko au vyama nipya vilivyoanzishwa na ccm kwa ajili ya kuikabili chadema ambavyo ni chauma ,adc na vingine wanavyovijua wao. nasema hayo sababu nyingi lakini nitasema chache.
1.wakati viongozi wa juu wote wa chadema wanapambana kwa kutumia m4c zito haujaonekana hata kwenye mkutano mmoja ikiwa kama ni kutotaka kutamka maneno ya kuwaudhi waliokutuma kuichafua chadema.
2.zito unapopeleka hoja yoyote bungeni inakuwa ya kujijenga binafsi na si kwa maslahi ya wanyonge wengi na wabunge wa upinzani hususani chama chako na hii ni pamoja na kutokutoka nje ya ukumbi wa bunge pale chadema wanapofanya hivyo kwa maslahi ya chama chao.
3.umejisifu sana kuwa wewe ni muadilifu na unao uwezo wa kuwa rais wa nchi 2015 kwa hili umekosea maana njia uliyoitumia ni mbovu sana maana kuna vikao vya chama ambavyo ungevitumia kueleza hoja yako lakini kwa kutumia waandishi wa habari na bunge na vijana wako wa kigoma halitakusaidia kufika huko maana nyuma yake inaoonekana kuna baraka za bwana mkubwa ili muivuruge chadema.
4.taarifa zisizo rasmi zinaonyesha urafiki wako wa karibu na jakaya na ridhiwani ni mashaka makubwa sana maana hakuna sehemu yoyote ambayo umemlaumu rais wa nchi kwa udhaifu wake bali amekutumia kumdhalilisha waziri mkuu kwa maslahi ya ikulu na si kwa upinzani unaposema serikali haiko makini bado unaficha kumtaja jakaya moja kwa moja sababu ya agenda zenu za siri ambazo wana ccm na wanachadema wengi wameliona.
Umeingizwa kwenye orodha ya wala rushwa wabunge kwa makusudi tu kuichafua chadema na si vinginevyo na hili unalijua vizuri.sidhani kama kupitia chadema utafanikiwa ndoto zako maana chadema wako makini ndio maana hakuna kiongozi wa juu wa chama aliyejibu hoja zako za kuutaka uraisi kiurahisi ushauri wangu kwako utangaze adharani kujiunga kwako na kundi la shibuda nakutakia safari njema.m4c daima.
umeandika vizuri lakini hiyo point ya kwanza nadhani hujamtendea haki maana huu ni wakati wa bunge na yuko dodoma, hayo mengine sina comment atajua mwenyewe kama hiyo roho ya unafiki ni kweli anayo