Ushauri wangu kwa TBC kuongeza rates ya watazamaji

Tatizo LA TBC ni kutokuwa wakweli hasa linaoikuja swala LA ccm na serikali

Hawatendi kwa kujiamini wala kwa haki

Ili waonekane wanajali habari za vyama vya siasa

Watatangaza tadea na ccm updp na ccm UDP na ccm pppt maendeleo na ccm lakini habari za chadema ukawa au cuf never never ever sasa hapa wananchi wanaona kuna upendeleo wa dhahiri na habari za kweli ambazo ni negative kwa gvt hutazisikia kule

TBC ni TV ya uma ila mmmh
 
Siku ukisikia habari za cuf au chadema ujue ni zile mbaya tu baaasiiii mfano wanachama 7000 wachadema wahamia ccm hapo ndio utaisikia chadema ila miradi ya maji rea vijijini hapo utaisikia ccm tu sasa hii sio haki mnafanya hata wale wanaoiona serikali haina upendeleo iingie DOA

Kwakifupi TBC ni DOA kwa serikali yetu
 
Naungana na ushauri wako (ingawa si katika vipengele vyote) kwa mantiki ya kuamsha ari ya wananchi kupenda na kuitazama TV ya Taifa. Menejimenti inapaswa kusoma/kufahamu na kuzingatia mahitaji ya washika dau wao, na kuweka mikakati ya kufikia mahitaji yao kwa kuzingatia vipaumbele vya kila kundi na kujitahidi kugusa hisia za wanajamii kuanzia ngazi ya chini mpaka Taifa.
Zaidi pia iwajengee uwezo hata watangazaji wake, uwezo wa kuhoji, kutoa hoja, kuteka hadhira, kudadisi, mwonekano, kujali muda, kuburudisha nk! Na hata kuwaboreshea uchumi/wawezeshwe ili kuwapa nafasi ya kujifunza kutoka vyombo vyingine vinavyofanya kazi (wapate muda/uwezo wa kuangalia TV stesheni zingine duniani hata wakiwa manyumbani.
 
Back
Top Bottom