Ushauri wangu kwa Mzee Samuel Sitta

Ushauri wangu kwa Mzee Samuel Sitta

Manyerere Jackton

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
2,438
Reaction score
4,461
Awali ya yote niseme watu wanaothubutu kuitibua JF ili isiwe hewani, ni wa kulaaniwa.
Nchi inayoamini katika uhuru wa habari haiwezi kuwavumilia watu wa aina hiyo.

Pili, leo kwenye magazeti mengi, Mzee Samuel Sitta, ametamba kweli kweli. Anautaka u-Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mzee Sitta, anajijengea umaarufu mkubwa wakati wa uongozi wake wa Bunge mwaka 2005-2010. Kipindi kilichofuata alipambana na sifa ngumu ya ama kubadili jinsi ili awe na sifa ya kuwania tena u-Spika, au aendelee na jinsi yake na kwa hiyo aukose u-Spika. Akaukosa.

Akaingia kwenye Bunge la Katiba kama Mwenyekiti (Spika). Huko akafanya madudu kadri alivyoweza.
Alichuma aibu kubwa kwa kufinyanga mapendekezo murua yaliyokuwa kwenye Tume ya Jaji Warioba. Baada ya hapo akawa hana amani. Akawa mtu wa kushambuliwa kwa maneno makali.

Serikali ya Awamu ya Tano ndiyo hiyo imeshabisha hodi. Sitta, ameibuka kwa kasi ya aina yake akiutaka u-Spika. Licha ya umri wake kumtupa mkono, bado anaamini ni yeye mwenye uwezo wa kulimudu hili Bunge jipya.

Sijui kitu gani kimemvuta (ulevi wa madaraka?), labda anataka "kufukia mashimo" aliyosababisha kwenye Bunge Maalum la Katiba.
Ushauri wangu: Sitta aachane na madaraka haya anayotaka. Atachuma aibu kama wazee wenzake-Piusu Msekwa, John Malecela, na juzi tu; Mzee Steven Wasira.

Mabadiliko wanayotaka Watanzania hayawezi kuletwa na watu wa aina ya Mzee Sitta. Tangu Awamu ya Kwanza hadi Awamu ya Tano awe kiongozi tu-haiwezekani. Kibaiolojia, umri mkubwa unapunguza na hata kuondoa uwezo wa nguvu kimwili na kiakili. Watanzania hawawezi kuyapata mabadiliko wanayoyataka kama wataendelea kuongozwa na mashine zile zile za tangu Uhuru.

Kama Mzee Sitta, anapita humu Jukwaani, apokee ushauri wangu. Kama hapiti, basi afikishiwe ujumbe huu. Ameshakuwa Agazo la Kale, na sasa Watanzania wanataka Agano Jipya! Wanaomtakia heshima njema aliyobaki nayo kazi alizolifanyia Taifa watamwambia: "Mzee pumzika, usimalizie heshima kidogo iliyobaki baada ya kuvurunda kwenye Bunge la Katiba".

Nawasilisha.
 
Bunge la 12 samweli sita hatoliweza, na kwa vile ccm watapeleka jina hilo na kuambiwa wamchague, nashauri na chadema wampendekeze james lemebeli akapambane na sita. Hii itakuwa hatua nzuri ya kulitabiri bunge lijalo...
 
Huyu Ana zindiko gani na nchi yetu?
Mi nafikiri asishauriwe Bali akatazwe.
 
hafai kuwa spika,alivuruga sana wakati wa bunge la katiba..hana msimamo yake ile ya mwanzo.
 
kama Sitta atagombea basi hakuna wa kumzuia , wabunge wengi wanampenda sana Sitta kwa sababu anawajali sana wabunge
 
angestaafu tu kwa amani .ajifunze kwa mrema aliyeng'ang'ania madaraka hatimae kastaafishwa kwa aibu pamoja na heshima kubwa aliyojipatia miaka ya nyuma .
 
Mleta mada umeiandika vizuri kweli. Laki mbona miezi michache iliyopita haukuandika hivi kuhisu mgombe urais aliekuwa mzee kuliko wote na ndo alieleta sera za mabadiliko? Au kuna vyeo vitakavyo vijana na vipo vya wazee?😁
 
Huyu mzee hata kama akiwa spika bila kulipwa mshahara hafai na hatumataki kabisa,toka enzi za nyerere yumo tuu serikalini!!!!! hivi vijana wanaosoma wafanye kazi gani kama wao hawataki kufika mwisho wa kikomo cha uongozi?
Mzee Sitta imetosha tuachie nchi yetu uliyoyafanya yanatosha sasa zamu zenu zimepita
 
Manyerere Jackton unahoja, lakini Bunge la sasa linahitaji mtu aliyebobea kwenye sheria!
 
Last edited by a moderator:
Ukishakuwa mwanasiasa uchu wa madaraka unazidi kukutafuna, no wonder hata wanaokufa watoto wao wanateuliwa,
 
Manyerere hivi kwa akili zako unadhani kuna mabadiliko ndani ya ccm? Hizo ni ndoto, spika awe sita au mwingine yeyote ndani ya hicho chama ulishaambiwa ccm ni ileile siku zote.
 
Sitta pumzika huoni aibu miaka 72 umekuwa kikongwe pumzika ulee wajukuu.
Asha rose Migiro,George Simbachawene na wengineo ndio wanaofaa kuwa spika

mwili umechoka akili imechoka,pumzika mzee,utapata aibu kama Wasira.
 
Huyu mzee baada ya kufanya ubabe wa hali ya juu na kufuja mabillioni ya hela ya walipa kodi kwenye bunge la katiba na kupindisha kanuni kwa maslahi yake binafsi na chama chake badala ya maslahi ya taifa ni vizuri atumie busara na akaamua kukaa pembeni.
 
Sioni kama hoja ulizoziandika zina mashiko. Kwani mtu kuwepo tangu enzi za Mwl ni dhambi kuwa spika. Kinachoangaliwa ni umri au weledi. Kumbe wanaijeria ni "Malofa" kumchagua Bhuhari.
 
Back
Top Bottom