Vyombo vya habari gani vya kumhoji Lowassa? Waandishi wa habari gani wa kufanya mdahalo na Lowassa wakati wahariri wengi tayari wako mfukoni mwa Lowassa? Hii itakuwa danganya toto tu! Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, Absalom Kibanda, ambaye pia ni mhariri wa Tanzania Daima ni mfanyakazi wa Lowassa. Saeed Kubenea wa MwanaHALISI ambao wengi mnamuona ni shujaa wenu naye kanunuliwa na kuwekwa mfukoni na Lowassa.
Huo mdahalo na waandishi wa habari si utakuwa stage managed tu? Hapa ni usanii tu, sina imani na waandishi wa habari wa Tanzania kutenda haki mbele ya fisadi Lowassa.
Kama mdahalo uwe hivi, kambi ya mafisadi ( Edward Lowassa, Rostam Aziz na Andrew Chenge) vs kambi ya wapambanaji (Samuel Sitta, Dr. Harrison Mwakyembe na Nape Nnauye). Huo ndio utakuwa mdahalo wa kweli, si wa wahariri walionunuliwa na Lowassa.
Njia pekee ya Lowassa ya kujisafisha ni kupelekwa mahakamani kama Jacob Zuma wa Afrika Kusini, akishinda kesi ya ufisadi wa abuse of public office kwa kutoa tenda kwa richmond na kuwa na utajiri usioelezeka (unexplained wealth) basi hata mimi nitamkubali.
Mamluki wanaolipwa vijisenti ili kumtetea fisadi Lowassa wana kazi kweli kweli....