Ushauri wangu kwa Lowassa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri wangu kwa Lowassa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mtamanyali, Dec 15, 2011.

 1. mtamanyali

  mtamanyali JF-Expert Member

  #1
  Dec 15, 2011
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Habari ndugu zangu wana JF. Kwa mara ya kwanza najitokeza kwenye jukwaa hili, kwa muda mrefu nimekua nikisikia tuhuma nyingi zikielekezwa kwa aliyekua waziri mkuu wa jamhuri ya Tanzania Mheshimiwa Lowasa, yeye binafsi anapinga tuhuma hizi na kusema kua sio za kweli.

  Ushauri wangu kweke ni kwamba naomba aitishe mdahalo wa wazi utakaompa nafasi ya kujibu maswali mbalimbali yatakayoulizwa kwake ili watu tujue ukweli ulipo.

  Binafsi namkubali sana ila nakua namashaka sana na hizi tuhuma zinazoelekezwa kwake kwa hiyo naomba aje ajieleze mbele wa wananchi tujue ukweli uko wapi. Naomba kuwasilisha.
   
 2. ntogwisangu

  ntogwisangu JF-Expert Member

  #2
  Dec 15, 2011
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 516
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  ushauri mzuri huu kuliko maelezo!!!!kuna vyombo vya habari,atoke aruhusu kadamnasi imuulize maswali impe ushaidi!!!hapo ndipo atakuwa amejisafisha!!otherwise jf au nec kwa kugawa hela hatoweza!!!!
   
 3. mtamanyali

  mtamanyali JF-Expert Member

  #3
  Dec 15, 2011
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  kweli kabisa anaweza kutumia pesa nyingi sana kwa njia anayoitumia ila mimi binafsi naona kujitokeza hadharani na kujibu maswali kwa watanzania itakua ni njia bora zaidi kwake. Kama kweli anasema tuhuma hizo hazimhusu basi itakua ni kazi rahisi sana kwake.
   
 4. s

  sindo Senior Member

  #4
  Dec 15, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 135
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Jamani Mnyonge mnyongeni
  haki yake impeni, angekuwa na kosa asingesubutu kuwaambia waache kupindisha mambo
  KILICHOMNYAMAZISHA MZEE WA KAYA NINI
  LOWASA ALISEMA MZEE WA KAYA ANAJUA KILA KITU UMESIKIA KAKANUSHA?
  KITU YA MZEE WA KAYA HIYO NDIO MAANA ALINYAMAZA,
  WAWEZA THIBUTU KUSEMA BABA YAKO NDIO ANAKOJOA KITANDAJI NA SIO WEWE
   
 5. OTIS

  OTIS JF-Expert Member

  #5
  Dec 15, 2011
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Dawa ya maiti ni kuzika
  Tafakari
  OTIS
   
 6. ntogwisangu

  ntogwisangu JF-Expert Member

  #6
  Dec 15, 2011
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 516
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  aombe air time tv zote,aende jangwani na maswali yaulize na yeyote!!sio dk 7 za nec huku wamejipanga!!!!!
   
 7. M

  Mbalinga JF-Expert Member

  #7
  Dec 15, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 1,382
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  Hiyo haipo, atangojea mpaka 2015 atakapochukua fomu ya kugombea uraisi
   
 8. kanta

  kanta JF-Expert Member

  #8
  Dec 15, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 343
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hata akijisafisha kwa njia hiyo haitaweza kumsaidia, mnasema hiyo issue ya mkuu wakaya lakini na yeye mwenyewe yumo.ukiambiwa na mtu nenda kaibe unadhani huo msala ni wa aliyekutuma?msala unakuwa wenu wote,pambaf.wote mafisadi hao hata aite cnn kumhoji.
   
 9. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #9
  Dec 15, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ndo alivyokutuma uje ueleze ujinga hapa? kamwambie hivi "We are no long with him". Full stop.
   
 10. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #10
  Dec 15, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hivi nyinyi wapumbavu mnaoshughulishwa na Lowassa hamuwaoni watu wengine? mbona Tz kuna watu wengi tu tena wazuri na waadilifu. kuna haja gani ya kuhangaika na mtu ambaye si muadilifu? Hebu tuangalie wenzetu walioendelea kama wanaendekezaga upumbavu kama huu. Huyo akiingia madarakani sana sana atakuwa na kazi ya kulipiza visasi tu, mara sita, mara mwakyembe et al, badala ya kututumikia sisi.
   
 11. mtamanyali

  mtamanyali JF-Expert Member

  #11
  Dec 15, 2011
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  hajanituma mtu kaka mimi ni mtanzania wakawaida tu na ninahaki ya kutoa maoni yangu.
   
 12. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #12
  Dec 15, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mkuu hata kama unamkubali ila kusema kweli Lowasa ni mchafu na hata akitumia vyombo vyote duniani kujisafisha hatotakata ng'o hata kama serikali ingempeleka mahakamani ili maakama imsafishe bado tu asingesafishika kwani mahakama huwa matajiri na watu maarufu siku zote hawakutwi na makosa
   
 13. fige

  fige JF-Expert Member

  #13
  Dec 15, 2011
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 376
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapa jf watu wanataka kuhakikisha theory ya kikwete aliyowahi sema.
  Nanukuu
  'jambo ukilisema sana hata kama ni uongo,ile kurudiarudia inalifanya jambo hilo ni la kweli'

  Hili naliona kwa bidii ya nyuzi zinazomhusu huyu bwana.kwani hata kama hamna kipya cha maana watu hawaishi kuanzisha nyuzi za kumsifu.

  Labda wanataka watu wote jf waanze kumsifia ndio waache.je itawezekana ?
   
 14. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #14
  Dec 15, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Unaonaje ukimtumia PM ili umpatie huu ushauri, anaweza kuukubali
   
 15. mtamanyali

  mtamanyali JF-Expert Member

  #15
  Dec 15, 2011
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  hapo sawa kabisa
   
 16. mtamanyali

  mtamanyali JF-Expert Member

  #16
  Dec 15, 2011
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  nimekupata ndugu, ila nimeweka jamvin ili watu wengine waongezee nilichosahau. Na ajue watu wengine wanaupokeaje ushauri wangu.
   
 17. mtamanyali

  mtamanyali JF-Expert Member

  #17
  Dec 15, 2011
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  watu wengi wanajua lowasa ni mchafu hata mwenyewe pia kutokana na tuhuma nyingi zinazoelekezwa kwake cha ajabu yeye anakataa ndio maana naona ni bora aulizwe mbele ya wananchi na ajibu maswali ili tumwone kama mkweli.
   
 18. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #18
  Dec 15, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Nani hasiyekuwa na tuhuma awe wa kwanza kumrushia jiwe Lowassa! Nchi hii kuna baadhi ya watu mnasikiliza na kuamini fitina na majungu.
   
 19. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #19
  Dec 16, 2011
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  EL hana uchafu wowote zaidi ya chuki,fitna,wivu mnaoaminishwa
   
 20. F

  Fareed JF-Expert Member

  #20
  Dec 16, 2011
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Vyombo vya habari gani vya kumhoji Lowassa? Waandishi wa habari gani wa kufanya mdahalo na Lowassa wakati wahariri wengi tayari wako mfukoni mwa Lowassa? Hii itakuwa danganya toto tu! Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, Absalom Kibanda, ambaye pia ni mhariri wa Tanzania Daima ni mfanyakazi wa Lowassa. Saeed Kubenea wa MwanaHALISI ambao wengi mnamuona ni shujaa wenu naye kanunuliwa na kuwekwa mfukoni na Lowassa.

  Huo mdahalo na waandishi wa habari si utakuwa stage managed tu? Hapa ni usanii tu, sina imani na waandishi wa habari wa Tanzania kutenda haki mbele ya fisadi Lowassa.

  Kama mdahalo uwe hivi, kambi ya mafisadi ( Edward Lowassa, Rostam Aziz na Andrew Chenge) vs kambi ya wapambanaji (Samuel Sitta, Dr. Harrison Mwakyembe na Nape Nnauye). Huo ndio utakuwa mdahalo wa kweli, si wa wahariri walionunuliwa na Lowassa.

  Njia pekee ya Lowassa ya kujisafisha ni kupelekwa mahakamani kama Jacob Zuma wa Afrika Kusini, akishinda kesi ya ufisadi wa abuse of public office kwa kutoa tenda kwa richmond na kuwa na utajiri usioelezeka (unexplained wealth) basi hata mimi nitamkubali.

  Mamluki wanaolipwa vijisenti ili kumtetea fisadi Lowassa wana kazi kweli kweli....
   
Loading...