UCHAGUZI WA WABUNGE WA AFRIKA MASHARIKI
Nimetafakari sana juu ya ukuaji wa Demokrasia na Nafasi ya Upinzani Imara Wenye Mshikamano na Umoja. Wakati huu kama alivyosema Mh Lema wakati wa Kongamano la ACT juu ya Azimio la Arusha, Ndio wakati wa Muhimu sana kuungana kuliko ilivyowahi kutokea. Namna gani tunaungani ni kwa kwenda na dhana ya give and take ili tufaidike lakini tujiimarishe kwa mstakabali wa kukuza demokrasia na kuongeza nguvu ya Mapambano. Bado hatujachelewa kutengeneza kitu kizuri chenye umoja. Ifikie pahalatofauti zetu na historia zitupe fundisho na tuzizike.Tusipoangalia vizuri uchaguzi huu wa Wabunge wa East Africa utaacha umetugawanya kwelikweli na ikiwezekana kugawa hata UKAWA ili wafadhili wa Akina Bwana Yule Waendelee Kujenga nguzo za kubomoa Upinzani ambao ulikuwa unakua kwa kasi. Natumeshaanza kusikia Bwana Yule Karibuni Ataongeza nguvu ya Mjomba aliyeenda kupikwa kwenye Jungle. Mpaka imefikia Mjomba kutoka kwenye Jungle anasema Upinzani utakuwa umekufa kufikia 2020; Tungepiga picha ya mbeleni tungekuwa tumeona analenga nini.
Kama kanuni zinaruhusu na ACT na NCCR Mageuzi wawe na wagombea kwenye Bunge la Afrika Mashariki. Tukubaliene na Kugawana nafasi na mimi Sayansi Yangu inanituma Mgawanyo uwe hivi; Tuchukulie Nafasi Zile Tatu ni za Wapinzani na Wote Tuheshimu Uwakilishi Tulionao Tuitane na Tukae Pamoja na Kukubaliana kwamba. ACT na NCCR vyenye wabunge mmoja mmoja vitoe Majina Mawili halafu waje mbele ya wabunge wote wa Upinzani wajinadi halafu, wabunge wa Upinzani wapige kura apatikane Mtu mmoja ambaye vyama vyote viwili viridhie atakayeongoza ndo asimamishwe kugombea. Halafu zile nafasi mbili moja awepo Mgombea kutoka CHADEMA mmoja na Mwingine kutoka CUF mmoja. Na tutakachofanya sisi kama wapinzania tuwasilishe majina yetu hayo matatu tu. Tutakuwa tumeshinda fitina ya "Divide and Rule" Wagawe na Uwatawale.
Na Wagombea wetu watatu waende wakiwa ni wao tu na watapigiwa kura za ndiyo na Hapana na Ushindi Utakuwepo umefanyika Kimkakati lakini zaidi umoja uliokomaa miongoni mwa vyama vya upinzani utakuwa umeanza kujenga. Tusipofanya haya maana wapiga kura ndani ya Bunge si wabunge wa upinzani tu bali wabunge wote. Kuna Hatari ya kuamua kukomoana na kupandikiza Chuki ambazo hazipo. Yawezekana upande wa Pili wakajipanga kwamba Tupigie watu wa CUF tu na ACT ili CHADEMA ikose ili ujengwe mgogoro mwingine ndani ya UKAWA kuukomaza ule wa Bwana Yule na kuleta Mparaganyiko. Au Yawezekana wakaamua tumwangushe Mgombea wa ACT Wazalendo, Ili ACT aone anatengwa na Wenzie katika Upinzani na ageuke na kuwa Peke Yake. Yawezekana wakaamua tumpigie wa ACT au wa NCCR na wawili wa CHADEMA ili CUF waone wamehujumiwa na CHADEMA na hivyo kuleta Mgogoro kwenye UKAWA. Ebu Tushinde Kiakili na Tushinde kwa kuimarisha Mshikamano na Umoja.
Nimeandika haya ili tuone jinsi navyoweza kufumbwa macho na tukazalisha mparaganyiko na mwisho wa siku Bwana Yule na Mjomba aliyepo Mafichoni wakawa washindi na Upinzani Ukawa umefifia au umeanguka Ndembendembe kufikia mwaka wa 2020.
Hatujachelewa viongozi wote wa vyama vya upinzane na vyenye uwakilishi bungeni ebu kutaneni haraka kwa dharura, chagueni kujenga nguza na UKUTA Imara usioruhusu risasi nyepesi na ngumu kupenya kwa njia yoyote ile. Mtaniambia kama hamtachagua kujenga siko siyo chache nimeota limgogoro hilo likubwa linakuja. Mnakuwa mnapigwa hata kwa kiwembe na upinde wala haitahitajika risasi na mitutu kuwamaliza.
Mwisho na declare interest, Mimi ni Mkereketwa, Mwanachama na mwana mabadiliko kupitia CHADEMA