Ushauri Wangu Kwa ACT, CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi

Ushauri Wangu Kwa ACT, CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi

kwa hiyo sasa Zitto sio msaliti tena
Mbona unajitoa ufaham mkuu ww apo juu umesema eti tulikataa kuungana na mtu kisa msaliti na kwamba chadema sijui wanafki ssa na mmi ndo nmekukumbusha kuwa ccm waliwaita cuf chama cha sultan na waislam na magaidi ila bado mkawaomba wajiunge SUK ssa hilo wwe unalionaje kabla sijakupa sababu za kwanni kuna umuhim ukawa kuungana na kina zitto???
 
usihesabie majimbo ya Zanzibar mkuu huko tunaelewa siasa zake zilivyo!
basi ndio ujue bara CUF walikuwa na wabunge 2 tu leo hii ina wabunge 10 pia wakavuna halmashauri kitu ambacho hawakukifanikisha ndani ya miaka 20 !!! ssa unapata wapi hoja ya kusema wamenyonywa???

Yaani wamemzidi chadema wabunge eti wamenyonywa ssa ulitaka wapate ushindi wa aina gani muone kweli CUF inaheshimiwa na chadema???
 
UCHAGUZI WA WABUNGE WA AFRIKA MASHARIKI​
Nimetafakari sana juu ya ukuaji wa Demokrasia na Nafasi ya Upinzani Imara Wenye Mshikamano na Umoja. Wakati huu kama alivyosema Mh Lema wakati wa Kongamano la ACT juu ya Azimio la Arusha, Ndio wakati wa Muhimu sana kuungana kuliko ilivyowahi kutokea. Namna gani tunaungani ni kwa kwenda na dhana ya give and take ili tufaidike lakini tujiimarishe kwa mstakabali wa kukuza demokrasia na kuongeza nguvu ya Mapambano. Bado hatujachelewa kutengeneza kitu kizuri chenye umoja. Ifikie pahalatofauti zetu na historia zitupe fundisho na tuzizike.

Tusipoangalia vizuri uchaguzi huu wa Wabunge wa East Africa utaacha umetugawanya kwelikweli na ikiwezekana kugawa hata UKAWA ili wafadhili wa Akina Bwana Yule Waendelee Kujenga nguzo za kubomoa Upinzani ambao ulikuwa unakua kwa kasi. Natumeshaanza kusikia Bwana Yule Karibuni Ataongeza nguvu ya Mjomba aliyeenda kupikwa kwenye Jungle. Mpaka imefikia Mjomba kutoka kwenye Jungle anasema Upinzani utakuwa umekufa kufikia 2020; Tungepiga picha ya mbeleni tungekuwa tumeona analenga nini.

Kama kanuni zinaruhusu na ACT na NCCR Mageuzi wawe na wagombea kwenye Bunge la Afrika Mashariki. Tukubaliene na Kugawana nafasi na mimi Sayansi Yangu inanituma Mgawanyo uwe hivi; Tuchukulie Nafasi Zile Tatu ni za Wapinzani na Wote Tuheshimu Uwakilishi Tulionao Tuitane na Tukae Pamoja na Kukubaliana kwamba. ACT na NCCR vyenye wabunge mmoja mmoja vitoe Majina Mawili halafu waje mbele ya wabunge wote wa Upinzani wajinadi halafu, wabunge wa Upinzani wapige kura apatikane Mtu mmoja ambaye vyama vyote viwili viridhie atakayeongoza ndo asimamishwe kugombea. Halafu zile nafasi mbili moja awepo Mgombea kutoka CHADEMA mmoja na Mwingine kutoka CUF mmoja. Na tutakachofanya sisi kama wapinzania tuwasilishe majina yetu hayo matatu tu. Tutakuwa tumeshinda fitina ya "Divide and Rule" Wagawe na Uwatawale.

Na Wagombea wetu watatu waende wakiwa ni wao tu na watapigiwa kura za ndiyo na Hapana na Ushindi Utakuwepo umefanyika Kimkakati lakini zaidi umoja uliokomaa miongoni mwa vyama vya upinzani utakuwa umeanza kujenga. Tusipofanya haya maana wapiga kura ndani ya Bunge si wabunge wa upinzani tu bali wabunge wote. Kuna Hatari ya kuamua kukomoana na kupandikiza Chuki ambazo hazipo. Yawezekana upande wa Pili wakajipanga kwamba Tupigie watu wa CUF tu na ACT ili CHADEMA ikose ili ujengwe mgogoro mwingine ndani ya UKAWA kuukomaza ule wa Bwana Yule na kuleta Mparaganyiko. Au Yawezekana wakaamua tumwangushe Mgombea wa ACT Wazalendo, Ili ACT aone anatengwa na Wenzie katika Upinzani na ageuke na kuwa Peke Yake. Yawezekana wakaamua tumpigie wa ACT au wa NCCR na wawili wa CHADEMA ili CUF waone wamehujumiwa na CHADEMA na hivyo kuleta Mgogoro kwenye UKAWA. Ebu Tushinde Kiakili na Tushinde kwa kuimarisha Mshikamano na Umoja.

Nimeandika haya ili tuone jinsi navyoweza kufumbwa macho na tukazalisha mparaganyiko na mwisho wa siku Bwana Yule na Mjomba aliyepo Mafichoni wakawa washindi na Upinzani Ukawa umefifia au umeanguka Ndembendembe kufikia mwaka wa 2020.

Hatujachelewa viongozi wote wa vyama vya upinzane na vyenye uwakilishi bungeni ebu kutaneni haraka kwa dharura, chagueni kujenga nguza na UKUTA Imara usioruhusu risasi nyepesi na ngumu kupenya kwa njia yoyote ile. Mtaniambia kama hamtachagua kujenga siko siyo chache nimeota limgogoro hilo likubwa linakuja. Mnakuwa mnapigwa hata kwa kiwembe na upinde wala haitahitajika risasi na mitutu kuwamaliza.

Mwisho na declare interest, Mimi ni Mkereketwa, Mwanachama na mwana mabadiliko kupitia CHADEMA
utaandika hata page 200000000000, ila kanuni zitabadilika na ACT watagombea na wabunge walio wengi (ccm) watachagua wagombea wa CUF ya Lipumba na ACT tuu. Mgombea yoyote wa chadema hatapita..... subiri utaona
 
Ushauri huu mzuri lakini sioni ukifuatwa, CHADEMA tukubali kupoteza na kwa kuwa si mara ya kwanza tuendelee kujenga chama chetu
 
basi ndio ujue bara CUF walikuwa na wabunge 2 tu leo hii ina wabunge 10 pia wakavuna halmashauri kitu ambacho hawakukifanikisha ndani ya miaka 20 !!! ssa unapata wapi hoja ya kusema wamenyonywa???

Yaani wamemzidi chadema wabunge eti wamenyonywa ssa ulitaka wapate ushindi wa aina gani muone kweli CUF inaheshimiwa na chadema???
sehemu zote wabunge wa CUF waliposhinda na CHADEMA walisimamisha mgombea...hata MtatIro amekosa ubunge kwa fitina za CHADEMA...
 
Chadema kwenye uchaguzi mkuu walipewa wagombee majimbo mengi Zaidi ya wenzao hiyo ni dhuluma bado wanataka tena kwenye bunge la afrika mashariki wawe wao tu nawashauri CUF na NCCR wajitoe UKAWA wanadhulumiwa sana
Nadhani wasingeweza kulingana ki majimbo ya kugombea kwani kuna majimbo hawajui NCCR pia hata CUF haina nguvu, ila CHAADEMA ilikuwa imejitanua sana kuliko hivyo, usinibeze hii ni kwa mjibu wa uelewa wangu
 
uko sahihi....ndio maana tunataka wawaachie na vyama vingine ili na wao wajitanue
 
natamani viongozi wote wa upinzanj waone ujumbe wako. vinginevyo ni shiida....
 
Umeisha sema ACT NA NCCR wana mbunge mmoja mmoja ktk binge la Jamuhuri CDM na CUF wanao wengi hizo nafasi waachiwe ACT/NCCR na wao wapanuke kisiasa mtakuwa mmejenga Ukuta bora kuliko kuparaganyika na style iliyo tumiwa CDM kupata wa gombea ni ya kidikiteita tena Hawa kuzingatia Jinsia wajitafakari wachukue hatua
We unadhani ACT anategemea kura kutoka wapi kama sio CCM. Usitishwe na ACT angalia ni vp unaweza kuongeza idadi ya majimbo ktk chama chetu.
Mwisho Wa Siku Wote Mnaopiga Propaganda Mnaona Wakifanya Hili Wapinzania Watakuwa Wamevuka Kizingiti cha Kuwatengenezea Mpasuko Hivyo Siwashangai Bali Nitavishangaa Vyama vya Upinzani Pale Vitakapotoa Nafasi ya Kugawanya na Kufarakanishwa Bila Kujua na Mwisho Kukosa Nguvu.
 
sehemu zote wabunge wa CUF waliposhinda na CHADEMA walisimamisha mgombea...hata MtatIro amekosa ubunge kwa fitina za CHADEMA...
embu acha unafki wwe unajua sehem ngapi chadema tumepoteza kisa CUF?? matokeo ya kigamboni na ilala umeyaona??? je kira za CUF wangempa chadema unafkiri zungu angerudi bungeni??? kubenea je??? acheni kutafuta kichaka cha kujifichia UKAWA kma changamoto zilikuwa pande zote mbili lakini muhim ni kuwa CUF ilipata majimbo mengi kuliko chadema ssa iweje hilo hulioni ila unaona kwa mtatiro tu lakini hujaskia humu chadema tukilalamika kupoteza jimbo la ilala kisa mukadam wa CUF!!!!
 
We unadhani ACT anategemea kura kutoka wapi kama sio CCM. Usitishwe na ACT angalia ni vp unaweza kuongeza idadi ya majimbo ktk chama chetu.
Kwani CDM wanategea kura kutoka Wapi??
 
Ushauri wako nimeupenda sana, ukawa uchukueni huu ushauri wala msipoteze muda.

Mh.Zitto ungana na ukawa ili uwe na nguvu kubwa, ukipuuza huu ushauri kwa matamanio ya ubunge wa Afriaka mashariki ukasahau manufaa mapana zaidi 2020 utakuwa umejimaliza kabisa!
 
hakuna cha kuongea nae inafahamika wazi Mtatiro amekoseshwa ubunge makusudi na CHADEMA....CHADEMA walijua Mtatiro akiingia bungeni atawafunika sana walichofanya ni kumkosesha ubunge na aliemkosesha ubunge akazawadiwa viti maalum
Mkuu Mtatiro kaukosa ubunge kwa uroho wa CDM.
Anatropia alipata baraka zote kwa viongozi wa juu. Haingii akilini kwamba viongozi walishindwa kumdhibiti.
ACT WE MUST STAND ON LAWS. TUSIWE KAMA NCCR AMBAYO WANAKWENDA KUFA KWA KUJITOSA KWENYE UKAWA.
 
Lema ndio aliongoza mapambano ya kumtoa zitto ndani ya CDM na kila mahali walimuita msaliti!!

same Lema anahudhuria kongamano la chama kisaliti

watanzania ni wanafiki sana!!

Siasa kila jambo lina wakati wake. Huo mtindo wa kudhani maamuzi ni chuki na kuwa huwa haiondoki ni kupotoka. Hizo ni siasa za mzee wa Chato tuu, kwamba hasahau na mpaka leo wale walioimba ukumbini bado ana hasira nao.
 
IF WE ARE SERIOUS TUNATAKA KUITOA CCM MADARAKANI KWA NJIA YA UMOJA, NI VEMA TUUNDE UMOJA MWINGINE NA SI UKAWA.
UKAWA HAUNA MISINGI MIZURI YA KUACHIANA NAFASI. UKAWA ULIKUWA KWA AJILI YA KATIBA.
UKAWA UNAUA VYAMA VINGINE. MFANO KAFULILA KATOKA NCCR KAENDS CDM NDANI YA UKAWA.
UKAWA HAISEMI ADHABU GANI MTU APATIWE PALE ANAPONG'NG'ANIA NAFASI ALIYOACHIA MTU WA CHAMA KINGINE.
MBAYA ZAIDI UKAWA HAIPO KIKATIBA.

ZITTO ALIULIZA APEWE TARATIBU ZA KUJIUNGA UKAWA WALISHINDWA KUMPA.

SISI ACT TUMEAMUA KUKIJENGA CHAMA CHETU KTK MISINGI MADHUBUTI NA YA KUDUMU.
HATUTAKI UBABAISHAJI WA MAMBO.
 
Niambie CDM tuna wabunge wangapi?
Wabunge wa CDM hawanaidadi ya kuwezasha kumvusha mgombea yoyote.kura za CCM ndo majority ndo maana CDM wanajua ACT na CUF ya Lipumba wakiweka watu CDM haiwezi kupata japo kiti kimoja.
 
Siasa kila jambo lina wakati wake. Huo mtindo wa kudhani maamuzi ni chuki na kuwa huwa haiondoki ni kupotoka. Hizo ni siasa za mzee wa Chato tuu, kwamba hasahau na mpaka leo wale walioimba ukumbini bado ana hasira nao.

????????
 
IF WE ARE SERIOUS TUNATAKA KUITOA CCM MADARAKANI KWA NJIA YA UMOJA, NI VEMA TUUNDE UMOJA MWINGINE NA SI UKAWA.
UKAWA HAUNA MISINGI MIZURI YA KUACHIANA NAFASI. UKAWA ULIKUWA KWA AJILI YA KATIBA.
UKAWA UNAUA VYAMA VINGINE. MFANO KAFULILA KATOKA NCCR KAENDS CDM NDANI YA UKAWA.
UKAWA HAISEMI ADHABU GANI MTU APATIWE PALE ANAPONG'NG'ANIA NAFASI ALIYOACHIA MTU WA CHAMA KINGINE.
MBAYA ZAIDI UKAWA HAIPO KIKATIBA.

ZITTO ALIULIZA APEWE TARATIBU ZA KUJIUNGA UKAWA WALISHINDWA KUMPA.

SISI ACT TUMEAMUA KUKIJENGA CHAMA CHETU KTK MISINGI MADHUBUTI NA YA KUDUMU.
HATUTAKI UBABAISHAJI WA MAMBO.
Kafulila alitoka CHADEMA akaenda NCCR, sasa amerudi kwenye chama chake ACT mnatafuta nini UKAWA.
 
Back
Top Bottom