Ushauri Wangu Kwa ACT, CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi

Ushauri Wangu Kwa ACT, CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi

Hakuna CHADEMA walipowadhulumu wenzao kwenye uchaguzi wowote. Kumbuka Kinachojadiliwa mada iliyopo mezani ni Wabunge wa Afrika Mashariki. Rejea Mwongozo wa Spika halafu useme CHADEMA imewadhulumje wenzake. Argue with substance. Usidandie Gari kwa Mbele.
Chadema kwenye uchaguzi mkuu walipewa wagombee majimbo mengi Zaidi ya wenzao hiyo ni dhuluma bado wanataka tena kwenye bunge la afrika mashariki wawe wao tu nawashauri CUF na NCCR wajitoe UKAWA wanadhulumiwa sana
 
Maneno matamu lengo ni kuwarubuni ACT, Zitto komaa hawa Chadema wanajali maslahi yao tu...Wakiona wamezidiwa ndio wanakumbuka kushirikiana.
Tunajua Zitto ni msaliti mwache aendelee na usaliti wake lakini ajue atavuna alichopanda. Mkikaa kumbembeleza Zitto mnapoteza muda.
 
Maneno matamu lengo ni kuwarubuni ACT, Zitto komaa hawa Chadema wanajali maslahi yao tu...Wakiona wamezidiwa ndio wanakumbuka kushirikiana.
sasa mtu anajenga ushirikiano nyie mnataka kubomoa ssa chadema ana lipi la kupoteza hakuwa na mbunge last time out na pia bungeni chadema wamewaacha act zaid ya mara 70!! ssa kma mnaoma nafasi tatu hizo ndio zifanye zitto kuonekana steringi its fine afu 2020 tuanze kulalamika tena CCM wakichukua majimbo yote kigoma
 
Tunajua Zitto ni msaliti mwache aendelee na usaliti wake lakini ajue atavuna alichopanda. Mkikaa kumbembeleza Zitto mnapoteza muda.
mkuu naona ccm wanampa kichwa sana hawajui wanampoteza na fainali ni 2020...... amesahau ya kina kaborou mrema na shibuda na cheyo!
 
kwa wakienda hao wa ACT kuna ubaya gan?? ni lazima wawe chadema tu? alafu eti wenje na masha, hawa wote walikuwa wabunge tena walikuwa jimbo moja kwa nyakati tofauti, HAKUNA JIPYA WALILOKUWA NALO!
 
hakuna cha kuongea nae inafahamika wazi Mtatiro amekoseshwa ubunge makusudi na CHADEMA....CHADEMA walijua Mtatiro akiingia bungeni atawafunika sana walichofanya ni kumkosesha ubunge na aliemkosesha ubunge akazawadiwa viti maalum
Hivi unajua CUF ilipata majimbo mengi sana ya kuchaguliwa kuliko hta chadema??? ssa kma chadema waliwahujumu cuf ilikuwaje cuf wakawazidi chadema kwenye wingi wa majimbo??? tuanzie hapo
 
UCHAGUZI WA WABUNGE WA AFRIKA MASHARIKI
Nimetafakari sana juu ya ukuaji wa Demokrasia na Nafasi ya Upinzani Imara Wenye Mshikamano na Umoja. Wakati huu kama alivyosema Mh Lema wakati wa Kongamano la ACT juu ya Azimio la Arusha, Ndio wakati wa Muhimu sana kuungana kuliko ilivyowahi kutokea. Namna gani tunaungani ni kwa kwenda na dhana ya give and take ili tufaidike lakini tujiimarishe kwa mstakabali wa kukuza demokrasia na kuongeza nguvu ya Mapambano. Bado hatujachelewa kutengeneza kitu kizuri chenye umoja. Ifikie pahalatofauti zetu na historia zitupe fundisho na tuzizike.

Tusipoangalia vizuri uchaguzi huu wa Wabunge wa East Africa utaacha umetugawanya kwelikweli na ikiwezekana kugawa hata UKAWA ili wafadhili wa Akina Bwana Yule Waendelee Kujenga nguzo za kubomoa Upinzani ambao ulikuwa unakua kwa kasi. Natumeshaanza kusikia Bwana Yule Karibuni Ataongeza nguvu ya Mjomba aliyeenda kupikwa kwenye Jungle. Mpaka imefikia Mjomba kutoka kwenye Jungle anasema Upinzani utakuwa umekufa kufikia 2020; Tungepiga picha ya mbeleni tungekuwa tumeona analenga nini.

Kama kanuni zinaruhusu na ACT na NCCR Mageuzi wawe na wagombea kwenye Bunge la Afrika Mashariki. Tukubaliene na Kugawana nafasi na mimi Sayansi Yangu inanituma Mgawanyo uwe hivi; Tuchukulie Nafasi Zile Tatu ni za Wapinzani na Wote Tuheshimu Uwakilishi Tulionao Tuitane na Tukae Pamoja na Kukubaliana kwamba. ACT na NCCR vyenye wabunge mmoja mmoja vitoe Majina Mawili halafu waje mbele ya wabunge wote wa Upinzani wajinadi halafu, wabunge wa Upinzani wapige kura apatikane Mtu mmoja ambaye vyama vyote viwili viridhie atakayeongoza ndo asimamishwe kugombea. Halafu zile nafasi mbili moja awepo Mgombea kutoka CHADEMA mmoja na Mwingine kutoka CUF mmoja. Na tutakachofanya sisi kama wapinzania tuwasilishe majina yetu hayo matatu tu. Tutakuwa tumeshinda fitina ya "Divide and Rule" Wagawe na Uwatawale.

Na Wagombea wetu watatu waende wakiwa ni wao tu na watapigiwa kura za ndiyo na Hapana na Ushindi Utakuwepo umefanyika Kimkakati lakini zaidi umoja uliokomaa miongoni mwa vyama vya upinzani utakuwa umeanza kujenga. Tusipofanya haya maana wapiga kura ndani ya Bunge si wabunge wa upinzani tu bali wabunge wote. Kuna Hatari ya kuamua kukomoana na kupandikiza Chuki ambazo hazipo. Yawezekana upande wa Pili wakajipanga kwamba Tupigie watu wa CUF tu na ACT ili CHADEMA ikose ili ujengwe mgogoro mwingine ndani ya UKAWA kuukomaza ule wa Bwana Yule na kuleta Mparaganyiko. Au Yawezekana wakaamua tumwangushe Mgombea wa ACT Wazalendo, Ili ACT aone anatengwa na Wenzie katika Upinzani na ageuke na kuwa Peke Yake. Yawezekana wakaamua tumpigie wa ACT au wa NCCR na wawili wa CHADEMA ili CUF waone wamehujumiwa na CHADEMA na hivyo kuleta Mgogoro kwenye UKAWA. Ebu Tushinde Kiakili na Tushinde kwa kuimarisha Mshikamano na Umoja.

Nimeandika haya ili tuone jinsi navyoweza kufumbwa macho na tukazalisha mparaganyiko na mwisho wa siku Bwana Yule na Mjomba aliyepo Mafichoni wakawa washindi na Upinzani Ukawa umefifia au umeanguka Ndembendembe kufikia mwaka wa 2020.

Hatujachelewa viongozi wote wa vyama vya upinzane na vyenye uwakilishi bungeni ebu kutaneni haraka kwa dharura, chagueni kujenga nguza na UKUTA Imara usioruhusu risasi nyepesi na ngumu kupenya kwa njia yoyote ile. Mtaniambia kama hamtachagua kujenga siko siyo chache nimeota limgogoro hilo likubwa linakuja. Mnakuwa mnapigwa hata kwa kiwembe na upinde wala haitahitajika risasi na mitutu kuwamaliza.

Mwisho na declare interest, Mimi ni Mkereketwa, Mwanachama na mwana mabadiliko kupitia CHADEMA

Lema ndio aliongoza mapambano ya kumtoa zitto ndani ya CDM na kila mahali walimuita msaliti!!

same Lema anahudhuria kongamano la chama kisaliti

watanzania ni wanafiki sana!!
 
Tunajua Zitto ni msaliti mwache aendelee na usaliti wake lakini ajue atavuna alichopanda. Mkikaa kumbembeleza Zitto mnapoteza muda.
Mkuu mbona kama povu hivi.... Acheni ubinafsi kila chama kinataka kukua na kujitangaza....

Wote wanatamani ruzuku ya serikali ili kukua na kujiendesha.....Acha demokrasia utawala nafasi yake.!
 
kwa wakienda hao wa ACT kuna ubaya gan?? ni lazima wawe chadema tu? alafu eti wenje na masha, hawa wote walikuwa wabunge tena walikuwa jimbo moja kwa nyakati tofauti, HAKUNA JIPYA WALILOKUWA NALO!
Mkuu wameshauri tu ili kusitokee mgawanyiko..... kumbuka mwanzoni kabisa ilitolewa proportion na spika kuwa ccm 3 chadema 2 na cuf 1 sasa kosa la chadema likwapi??? hoja hapa ni kwa kuwa kanuni zimebadilika basi wapinzani wasigawanyike maana its obvious ccm watapiga kura za kishabiki either kukomoa cuf au chadema au act so lazma atakayekosa atapata kinyongo !!!
Hata kma watapitishwa act wote but wakubaliane wote ili kusiwe na kinyongo au beef za baada ya uchaguzi maana umoja ni muhim kwa upinzani
 
Mkuu mbona kama povu hivi.... Acheni ubinafsi kila chama kinataka kukua na kujitangaza....

Wote wanatamani ruzuku ya serikali ili kukua na kujiendesha.....Acha demokrasia utawala nafasi yake.!
we huoni kunaweza tokea mgawanyiko ikitokea mmoja ya vyama ikakosa nafasi ukizingatia wote wanaweka mgombea???? huoni umoja utakufa!!!! huoni faida ya maridhiano kwa wapinzani????
 
Zito achana na upuuzi huu ushindi ni wako kitila na msando lazima watuwakilishe

Komaa peke tako siku zote walikuwa wapi kukupa ushauri huu
hahhahahha ccm mnashabikia maana mnaona upinzani utagawanyika!! kma mnafkiri upinzani utagawanyika kisa viti 3 mnajidanganya sana....... bungeni moto ni uleule
 
Lema ndio aliongoza mapambano ya kumtoa zitto ndani ya CDM na kila mahali walimuita msaliti!!

same Lema anahudhuria kongamano la chama kisaliti

watanzania ni wanafiki sana!!
Mkuu pale alienda kwa lengo lililokuwepo hta mangula alikuja kwenye mkutano mkuu wa chadema hta kma chadema walidai ccm kinanuka ila bado walimualika!!!! muhim kwenye mambo ya kitaifa ushabiki wa vyama unawekwaga pembeni ssa asiende kwenye issue nyeti kma azimio la arusha kisa tu zitto ni msaliti!! ssa usaliti unahusiana nini na nyerereism ????
 
Mkuu mbona kama povu hivi.... Acheni ubinafsi kila chama kinataka kukua na kujitangaza....

Wote wanatamani ruzuku ya serikali ili kukua na kujiendesha.....Acha demokrasia utawala nafasi yake.!
Si aliona Chadema haifai. We ndo povu linakutoka, CHADEMA hatukuwa na mbunge ktk bunge la Afrika Mashariki tulipungukiwa nini? Ktk uchaguzi huo ACT inawapiga kura wangapi kama inamtegemea CCM. Aendelee asitafute sababu. Nakumbuka alisema UKAWA ni waganga njaa. Sasa leo anatafuta nini UKAWA.
 
we huoni kunaweza tokea mgawanyiko ikitokea mmoja ya vyama ikakosa nafasi ukizingatia wote wanaweka mgombea???? huoni umoja utakufa!!!! huoni faida ya maridhiano kwa wapinzani????
Wangekuwa wanaungana dhidi ya CCM ingukuwa sawa....Lakini huu ushawishi ni kuminya demokrasia kwenye uwanja wa vyama vya upinzani.

Huu uoga baada ya kuona CCM wanaweza wasiwape kura, sababu wao ndio wenye maamuzi kwa wingi wao.

Kwani mara ngapi ACT amepigwa chini Chadema na hatujasikia wakilalamika.......

Washawishini wabunge wa CCM wawape kura, sio kutaka njia za mkato.
 
Chadema kwenye uchaguzi mkuu walipewa wagombee majimbo mengi Zaidi ya wenzao hiyo ni dhuluma bado wanataka tena kwenye bunge la afrika mashariki wawe wao tu nawashauri CUF na NCCR wajitoe UKAWA wanadhulumiwa sana
walidhulumiwa??? yaani cuf kutoka wabunge 2 mpaka 10 bara walidhulumiwa?? cuf kumbuka imeshinda majimbo mengi kuliko hta chadema ssa walidhulumiwaje na wakapata zaidi yao???? hao nccr walidhulumiwaje wakati kesi ya ubungr kafulila waliibeba kma yao ssa kma wanaroho mbaya wangempa support kafulila???
 
Back
Top Bottom