Ushauri Wangu Kwa ACT, CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi

Ushauri Wangu Kwa ACT, CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi

Heee !ndugu mkeleketwa na kada wa cdm mmekubali kushirikiana na wasaliti!? hapo tu ndo tatizo la upinzani haswa CDM ndo maana sitakaa kuwaamini tena maana ni wanafiki sana linapokuja suala la madaraka...
 
UCHAGUZI WA WABUNGE WA AFRIKA MASHARIKI​
Nimetafakari sana juu ya ukuaji wa Demokrasia na Nafasi ya Upinzani Imara Wenye Mshikamano na Umoja. Wakati huu kama alivyosema Mh Lema wakati wa Kongamano la ACT juu ya Azimio la Arusha, Ndio wakati wa Muhimu sana kuungana kuliko ilivyowahi kutokea. Namna gani tunaungani ni kwa kwenda na dhana ya give and take ili tufaidike lakini tujiimarishe kwa mstakabali wa kukuza demokrasia na kuongeza nguvu ya Mapambano. Bado hatujachelewa kutengeneza kitu kizuri chenye umoja. Ifikie pahalatofauti zetu na historia zitupe fundisho na tuzizike.

Tusipoangalia vizuri uchaguzi huu wa Wabunge wa East Africa utaacha umetugawanya kwelikweli na ikiwezekana kugawa hata UKAWA ili wafadhili wa Akina Bwana Yule Waendelee Kujenga nguzo za kubomoa Upinzani ambao ulikuwa unakua kwa kasi. Natumeshaanza kusikia Bwana Yule Karibuni Ataongeza nguvu ya Mjomba aliyeenda kupikwa kwenye Jungle. Mpaka imefikia Mjomba kutoka kwenye Jungle anasema Upinzani utakuwa umekufa kufikia 2020; Tungepiga picha ya mbeleni tungekuwa tumeona analenga nini.

Kama kanuni zinaruhusu na ACT na NCCR Mageuzi wawe na wagombea kwenye Bunge la Afrika Mashariki. Tukubaliene na Kugawana nafasi na mimi Sayansi Yangu inanituma Mgawanyo uwe hivi; Tuchukulie Nafasi Zile Tatu ni za Wapinzani na Wote Tuheshimu Uwakilishi Tulionao Tuitane na Tukae Pamoja na Kukubaliana kwamba. ACT na NCCR vyenye wabunge mmoja mmoja vitoe Majina Mawili halafu waje mbele ya wabunge wote wa Upinzani wajinadi halafu, wabunge wa Upinzani wapige kura apatikane Mtu mmoja ambaye vyama vyote viwili viridhie atakayeongoza ndo asimamishwe kugombea. Halafu zile nafasi mbili moja awepo Mgombea kutoka CHADEMA mmoja na Mwingine kutoka CUF mmoja. Na tutakachofanya sisi kama wapinzania tuwasilishe majina yetu hayo matatu tu. Tutakuwa tumeshinda fitina ya "Divide and Rule" Wagawe na Uwatawale.

Na Wagombea wetu watatu waende wakiwa ni wao tu na watapigiwa kura za ndiyo na Hapana na Ushindi Utakuwepo umefanyika Kimkakati lakini zaidi umoja uliokomaa miongoni mwa vyama vya upinzani utakuwa umeanza kujenga. Tusipofanya haya maana wapiga kura ndani ya Bunge si wabunge wa upinzani tu bali wabunge wote. Kuna Hatari ya kuamua kukomoana na kupandikiza Chuki ambazo hazipo. Yawezekana upande wa Pili wakajipanga kwamba Tupigie watu wa CUF tu na ACT ili CHADEMA ikose ili ujengwe mgogoro mwingine ndani ya UKAWA kuukomaza ule wa Bwana Yule na kuleta Mparaganyiko. Au Yawezekana wakaamua tumwangushe Mgombea wa ACT Wazalendo, Ili ACT aone anatengwa na Wenzie katika Upinzani na ageuke na kuwa Peke Yake. Yawezekana wakaamua tumpigie wa ACT au wa NCCR na wawili wa CHADEMA ili CUF waone wamehujumiwa na CHADEMA na hivyo kuleta Mgogoro kwenye UKAWA. Ebu Tushinde Kiakili na Tushinde kwa kuimarisha Mshikamano na Umoja.

Nimeandika haya ili tuone jinsi navyoweza kufumbwa macho na tukazalisha mparaganyiko na mwisho wa siku Bwana Yule na Mjomba aliyepo Mafichoni wakawa washindi na Upinzani Ukawa umefifia au umeanguka Ndembendembe kufikia mwaka wa 2020.

Hatujachelewa viongozi wote wa vyama vya upinzane na vyenye uwakilishi bungeni ebu kutaneni haraka kwa dharura, chagueni kujenga nguza na UKUTA Imara usioruhusu risasi nyepesi na ngumu kupenya kwa njia yoyote ile. Mtaniambia kama hamtachagua kujenga siko siyo chache nimeota limgogoro hilo likubwa linakuja. Mnakuwa mnapigwa hata kwa kiwembe na upinde wala haitahitajika risasi na mitutu kuwamaliza.

Mwisho na declare interest, Mimi ni Mkereketwa, Mwanachama na mwana mabadiliko kupitia CHADEMA
Mkuu...sina chama...lkn ni mkereketwa wa mageuzi "pure & natural"...na si maigizo tunayoshuhudia..
Wazo lako, ni zuri...ni la kimapinduzi!
Lkn duh!
Mgawanyiko ktk upinzani uko bayana! Kuna ubinafsi, ktk vyama vya upinzani, kufikia kiwango, cha "mabubu kuanza, kusema, wakilalamika waziwazi"...
...hali kwa sasa, ktk kipindi hiki cha uchaguzi wa EALA, imefika mbali kiutengano, ktk upinzani, bahati mbaya, ni kama vile uongozi wa juu wa chadema, uliona "umeshakamata", wakati ACT, walikuwa "wamekaza mwendo kimya kimya na kutangulia"....mbele mbali kabisa hata kushindwa sikia kauli za "walobaki mbali nyuma"...
...it's a point of no return....tusubiri ona, CCM, itamnyoa nani sasa, maanake upinzani, tayari ushawakabidhi "mkasi, na mamlaka ya kunyoa"...
Tutie vichwa maji sasa!
 
Dr Slaa anakuja toka Canada masomoni,.
Ondoa shaka.
Wa mafichoni unamjua we we.
Ila nakupa pongezi.umetoa ushauri bora kabisa,kwa yeyote yule mwenye kuelewa siasa za nchi hii.
Big up man
 
Nimesema Post hii Si ya Chama Cha CHADEMA ni ya Mwanachama Mwenye Maono, Hivyo agument za CHADEMA inamrubuni Zitto siyo sahihi hata kidogo. Lakini Pia unapotafuta kujenga unaanza na rasilimali ulizo nazo ndani kabla hujaenda kuomba. Huwezi kwenda kuomba bati na Saruji huku huna kiwanja utakapojengea. Kujenga Umoja ndani ya upinzani ndiko kunaweza kuwasaidia kwa pamoja kuomba kura kwa wabunge wa CCM
Mkuu Chijande, umeeleweka vizuri sana ulichosema mkuu...wasikurushe stimu wapuuzi mkuu!
 
Lema ndio aliongoza mapambano ya kumtoa zitto ndani ya CDM na kila mahali walimuita msaliti!!

same Lema anahudhuria kongamano la chama kisaliti

watanzania ni wanafiki sana!!
Hivi Lema alialikwa nanani?
 
Wangekuwa wanaungana dhidi ya CCM ingukuwa sawa....Lakini huu ushawishi ni kuminya demokrasia kwenye uwanja wa vyama vya upinzani.

Huu uoga baada ya kuona CCM wanaweza wasiwape kura, sababu wao ndio wenye maamuzi kwa wingi wao.

Kwani mara ngapi ACT amepigwa chini Chadema na hatujasikia wakilalamika.......

Washawishini wabunge wa CCM wawape kura, sio kutaka njia za mkato.
uoga??? ssa chadema wabunge 70+ na halmashauri za kumwaga waone UOGA kisa viti vitatu???? mkuu hapa inaweza kuwa viti 3 ila vikaleta mgawanyiko wa miaka mingi maana kma ACT atapewa kura na ccm kwa misingi ya kukomoa chadema (ambacho ACT anategemea pia kimsaidie) italeta picha kuwa zitto ni ooportunist wa kisiasa ambaye yuko tayari kurisk chochote kupata maslahi yake na hapo tutazidi kujenga mgawanyiko kati ya ACT na wenzake bungeni ambako sio afya kabisa maana 2020 kigoma yote tutaipoteza kwa kugawana kura na za urais pia zinagwanyika!!! ssa huoni tunaweka upinzani rehani kwa sababu ya mtego huu wa EALA ??
 
Atakayepinga mawazo yako ni mchawi tu wa upinzani,hata awe kiongozi wa upinzani
 
Kalia hilo kwamba hawana strategy wakati hata hii iliyotolewa ni strategy tena ya Mwanachama wa Kawaida Kabisa Nisiyejulikana. Huku Kuna Hazina ya Strategy ndo Maana hata wakati wa Uchaguzi Mkuu kille Chama ambacho Leo Ilikuwa Ni Sikuku Yao Walilazimika Kuiba Kauli mbiu ya M4C na Chama cha CHADEMA kikawaachia kwa sababu hakuna great thinkers huko au hata wakiwepo lazima wafiche fikra zao nzuri mifukoni maana wakisema tu wanaitwa wasaliti. Ukitaka kujua Chama Chenu Kilivyo na Macoca ZERO kasikilize wimbo wa WAPO. AnyWay Heri Kwa Siku Yenu Ya Leo
Povu la nini ndugu, kwani ni lazima aunge mkono hoja yako?
 
Lema ndio aliongoza mapambano ya kumtoa zitto ndani ya CDM na kila mahali walimuita msaliti!!

same Lema anahudhuria kongamano la chama kisaliti

watanzania ni wanafiki sana!!

Wewe Walewale Wafitinishaji. Hakuna Ambaye Hakosei Ndo Maana Hata Kwenye Chama Chenu cha CCM wapo walioitwa wasaliti ati kwa kutaka kupanga kumtembelea Mh Lema Gerezani. Nyinyi si wakujenga bali kubomoa. Wenye Akili wanawasoma na kuwaelewa. Nyinyi MwanaCCM akiwa anasalimia na Upinzani Msaliti, Mbunge alimwachia mwenzake wa upinzani muda Msaliti. Mmewavua uanachama kina Sophia Simba ni Kazi ya Chama Chenu. Vyama Vingine Vikifanya Taratibu Zake ni Kazi ya Vyama na Taratibu Zake. Kumfukuza Sophia Simba na Msambatavangu ni Halali akikiuka maadili. Lakini Upinzani kumweka Kando Lipumba ambaye tena alijiuzulu mwenyewe au kuwajibisha ni kosa. Nyinyi watu nyinyi UBASHITEISM tu.

Lakini yote kwa yote yametokea Mh Zitto na Wenzake hawako tena CHADEMA kwa yaliyofanyika. Lakini Zitto ni Kiongozi na CHADEMA na vyama vingine vina viongozi. Na kuna wakati Mbowe akiwa na Zitto alisema yaliyopita yamepita ifikie mahala tuyaache na kujenga. Hicho ndo tunataka. Mnakutana na changamoto zinawapa funzo mnaamua kuzitatua na kujenga. Hata ndani ya Chama Chako CCM rejea kauli ya Mh. Nape aliwahi kufukuzwa uanachama na pia alikili hadharani kukipigania chama kishinde wakati kikiwa na hali ngumu mpaka akaumia wengine wakipiga mvinyo lakini ananyooshewa Bastola hadharani.

Hivyo Changamoto Zipo kwa kila Chama na Zikitatuliwa ndiyo jambo la Msingi, hakuna palipo na Malaika hata huko kwako CCM changamoto zipo na wanakaa wanatafuta ufumbuzi wa kuwafanya wasimame. Hivyo usitake kufanikiwa kupitia kutengeneza mgogoro au kupalilia migogoro iliyopo kwa mwenzio au iliyokwisha kuwepo. Propaganda hizo hazina nafasi. Bado upinzani utaendelea kupita pori lililojaa wingi wa wanyama wa kali wa kila aina wataumia watakwaruzana watakwazana lakini wakipata wasaa wa kufanyia kazi changamoto wataimarika zaidi ya Jana. "Esprit de Coup"
 
UCHAGUZI WA WABUNGE WA AFRIKA MASHARIKI​
Nimetafakari sana juu ya ukuaji wa Demokrasia na Nafasi ya Upinzani Imara Wenye Mshikamano na Umoja. Wakati huu kama alivyosema Mh Lema wakati wa Kongamano la ACT juu ya Azimio la Arusha, Ndio wakati wa Muhimu sana kuungana kuliko ilivyowahi kutokea. Namna gani tunaungani ni kwa kwenda na dhana ya give and take ili tufaidike lakini tujiimarishe kwa mstakabali wa kukuza demokrasia na kuongeza nguvu ya Mapambano. Bado hatujachelewa kutengeneza kitu kizuri chenye umoja. Ifikie pahalatofauti zetu na historia zitupe fundisho na tuzizike.

Tusipoangalia vizuri uchaguzi huu wa Wabunge wa East Africa utaacha umetugawanya kwelikweli na ikiwezekana kugawa hata UKAWA ili wafadhili wa Akina Bwana Yule Waendelee Kujenga nguzo za kubomoa Upinzani ambao ulikuwa unakua kwa kasi. Natumeshaanza kusikia Bwana Yule Karibuni Ataongeza nguvu ya Mjomba aliyeenda kupikwa kwenye Jungle. Mpaka imefikia Mjomba kutoka kwenye Jungle anasema Upinzani utakuwa umekufa kufikia 2020; Tungepiga picha ya mbeleni tungekuwa tumeona analenga nini.

Kama kanuni zinaruhusu na ACT na NCCR Mageuzi wawe na wagombea kwenye Bunge la Afrika Mashariki. Tukubaliene na Kugawana nafasi na mimi Sayansi Yangu inanituma Mgawanyo uwe hivi; Tuchukulie Nafasi Zile Tatu ni za Wapinzani na Wote Tuheshimu Uwakilishi Tulionao Tuitane na Tukae Pamoja na Kukubaliana kwamba. ACT na NCCR vyenye wabunge mmoja mmoja vitoe Majina Mawili halafu waje mbele ya wabunge wote wa Upinzani wajinadi halafu, wabunge wa Upinzani wapige kura apatikane Mtu mmoja ambaye vyama vyote viwili viridhie atakayeongoza ndo asimamishwe kugombea. Halafu zile nafasi mbili moja awepo Mgombea kutoka CHADEMA mmoja na Mwingine kutoka CUF mmoja. Na tutakachofanya sisi kama wapinzania tuwasilishe majina yetu hayo matatu tu. Tutakuwa tumeshinda fitina ya "Divide and Rule" Wagawe na Uwatawale.

Na Wagombea wetu watatu waende wakiwa ni wao tu na watapigiwa kura za ndiyo na Hapana na Ushindi Utakuwepo umefanyika Kimkakati lakini zaidi umoja uliokomaa miongoni mwa vyama vya upinzani utakuwa umeanza kujenga. Tusipofanya haya maana wapiga kura ndani ya Bunge si wabunge wa upinzani tu bali wabunge wote. Kuna Hatari ya kuamua kukomoana na kupandikiza Chuki ambazo hazipo. Yawezekana upande wa Pili wakajipanga kwamba Tupigie watu wa CUF tu na ACT ili CHADEMA ikose ili ujengwe mgogoro mwingine ndani ya UKAWA kuukomaza ule wa Bwana Yule na kuleta Mparaganyiko. Au Yawezekana wakaamua tumwangushe Mgombea wa ACT Wazalendo, Ili ACT aone anatengwa na Wenzie katika Upinzani na ageuke na kuwa Peke Yake. Yawezekana wakaamua tumpigie wa ACT au wa NCCR na wawili wa CHADEMA ili CUF waone wamehujumiwa na CHADEMA na hivyo kuleta Mgogoro kwenye UKAWA. Ebu Tushinde Kiakili na Tushinde kwa kuimarisha Mshikamano na Umoja.

Nimeandika haya ili tuone jinsi navyoweza kufumbwa macho na tukazalisha mparaganyiko na mwisho wa siku Bwana Yule na Mjomba aliyepo Mafichoni wakawa washindi na Upinzani Ukawa umefifia au umeanguka Ndembendembe kufikia mwaka wa 2020.

Hatujachelewa viongozi wote wa vyama vya upinzane na vyenye uwakilishi bungeni ebu kutaneni haraka kwa dharura, chagueni kujenga nguza na UKUTA Imara usioruhusu risasi nyepesi na ngumu kupenya kwa njia yoyote ile. Mtaniambia kama hamtachagua kujenga siko siyo chache nimeota limgogoro hilo likubwa linakuja. Mnakuwa mnapigwa hata kwa kiwembe na upinde wala haitahitajika risasi na mitutu kuwamaliza.

Mwisho na declare interest, Mimi ni Mkereketwa, Mwanachama na mwana mabadiliko kupitia CHADEMA
Sawa kabisa ingawa wapinzani wote ni waoga kabisa...Mfano rais amevunja sheria ya vyama vya siasa..mfano haki ya kufanya mkutano ya public sehemu yoyote ya Tanzania lakini kwasasa hairusiwi n.a. wapinzani wapo kimya
 
Ni Changamoto ambayo lazima uwashauri wafanye njia gani nzuri kuishinda ukishaona inawakabili, na mojawapo ni kuanza kwa kujenga umoja
 
Ukitaka kuijua vizuri issue ya Mtatiro Ongea Nae Vizuri Ujue Ilikuwaje. Pia Muulize Mtatiro faida na Hasara za UKAWA. Changamoto Zipo Penye Wengi na Zinatafutiwa Tiba ili Kwenda Mbele. Akikujibu Faida Za UKAWA utakuwa na jibu zuri la kama kweli CHADEMA huungana kuumiza vyama vingine.

Aidha kabla ya Muunga na Baada ya Muungano wa UKAWA fanya Objective Analysis uone kama kuna mabadiliko, faida na Hasara
Jibu swali mtatiro alishindwa kwa sababu gani, usilete hekaya za abunuasi
 
Mwisho Wa Siku Wote Mnaopiga Propaganda Mnaona Wakifanya Hili Wapinzania Watakuwa Wamevuka Kizingiti cha Kuwatengenezea Mpasuko Hivyo Siwashangai Bali Nitavishangaa Vyama vya Upinzani Pale Vitakapotoa Nafasi ya Kugawanya na Kufarakanishwa Bila Kujua na Mwisho Kukosa Nguvu.
 
we huoni kunaweza tokea mgawanyiko ikitokea mmoja ya vyama ikakosa nafasi ukizingatia wote wanaweka mgombea???? huoni umoja utakufa!!!! huoni faida ya maridhiano kwa wapinzani????
Umoja na ACT hauna tija. Kwanza si mwana ukawa. Yeye ni wakuharibu aendelee na uharibufu wake mki mleta karibu atawatia hasara kubwa baadae.
 
sawa lakini kumbuka CHADEMA iko kwenye muungano wa UKAWA ndio maana hata kwenye uchaguzi waliachiana majimbo na hata kwenye urais walimwachia mgombea wa CHADEMA huu ni muungano mkuu sasa huo muungano una maana gani kama kila chama kitaweka mgombea wake? hujui hata ruzuku ya CHADEMA nyingi imetokana na huu muungano? kwa nini inapokuja kwenye kugombea madaraka CHADEMA wanawadhulumu UKAWA wenzao?
Huyu jamaa hajui anachojadili lakini ni haki yake. Tumsaidie tu bila kuchoka
 
Hivi unajua CUF ilipata majimbo mengi sana ya kuchaguliwa kuliko hta chadema??? ssa kma chadema waliwahujumu cuf ilikuwaje cuf wakawazidi chadema kwenye wingi wa majimbo??? tuanzie hapo
Majimbo yapi unaongelea ndugu
 
Umeisha sema ACT NA NCCR wana mbunge mmoja mmoja ktk binge la Jamuhuri CDM na CUF wanao wengi hizo nafasi waachiwe ACT/NCCR na wao wapanuke kisiasa mtakuwa mmejenga Ukuta bora kuliko kuparaganyika na style iliyo tumiwa CDM kupata wa gombea ni ya kidikiteita tena Hawa kuzingatia Jinsia wajitafakari wachukue hatua
 
Wapinzani kukubali rais kufunja sheria inaonyesha kua wao wakichukua nchi watavunja sheria zaidi ya huyu alieko Ikulu
 
Umoja na ACT hauna tija. Kwanza si mwana ukawa. Yeye ni wakuharibu aendelee na uharibufu wake mki mleta karibu atawatia hasara kubwa baadae.

Upinzani Wana Akili Sana na Wanajua Lazima Ziwepo Propaganda Kama Hizi Kuhakikisha Hamsimami na Mimi Nimewambia Chagueni Kusuka Ama Kunyoa. Angalieni wapi patawapa faida au nguvu msiwasikilize propagandist hawa wanaoleta maneno mara kuungana na Msaliti. Nimesema Yaliyokwisha Pita Yamepita Nisikilizeni Mimi ninabii Mzuri na kwenye andiko langu mimi nimewapa resolution nzuri ya kukutana na kuja na Mkakati utakaowaweka pamoja zaidi. It is never too Late. I believe Mtaupokea Unabii Huu
 
Back
Top Bottom