Ushauri wangu kuhusu Kilimo cha Katani au Mkonge Tanzania

Jan 5, 2019
3
1
Ndugu nadhani sasa inabidi tubadilike na tujaribu kuangalia mazao mengine ya kibiashara Kimataifa. Na hapo nazungumzia mazao ndani ya mashauriano ya kilimo huku ndani ni kama hayajulikani na kama hayatuhusu lakini ni kilimo vizuri kibiashara kimataifa.

Natoa ushauri Serikali yetu tukufu kuhamasisha wananchi wake juu ya mazao ya kibiashara zaidi ambayo yanaingizia Taifa fedha za kigeni na pia kuwa tayari kutoa ushirikiano kwetu ambao tayari tumejitoa kujikita katika mazao hayo.
 
Mr Nchimbi, hebu dadavua zaidi. Tupe maelezo zaidi kuhusu kilimo cha Mkonge. Hili zao ninavyolijua ulimaji wake hausumbui kabisa. Hebu tupe mwelekeo wa soko lake likoje sasa hivi.

Zao hili kama nilivyotangulia kusema ni zao la kibiashara na linauhataji mkubwa nje ya nchi yetu maana nyuzi zake zinatumika kwa kutengezea bidhaa nyingi zinazohitajika na wanadamu.

Ziko nchi nyingi zinazohitaji malighafu hiyo hasa China na nyingine zenye viwanda vingi vikubwa.

Unawezajiuliza tu kidogo kwamba mbona kilimo hiki kinaonekana hakijulikani sana.Hii inatokana kwamba mwanzo kilionekana kama kilimo cha mabepari na cha kikoloni.

Kama utapenda kuanza kulima nikushauri tembelea chuo cha mlingano pale Tanga kwa ushauri wa kitaalamu zaidi ili uje kunufaika baadaye.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hebu niambie nawezaje kupata decorticator ( mashine ya kutolea nyuzi) ndogo. Ya umeme au ya diesel. Nimepita maeneo ya tanga nimeona katani zipo na zipo nyingine ambazo hata kuvunwa hazivunwi.
 
ninao uwezo wa kupata mashine ya kusindika nyuzi za mkonge vipi nawezapata mkonge kwa wakulima wadogo nchini na je wananunuaje mkonge kwa wenye mkonge
 
Mkuu hebu niambie nawezaje kupata decorticator ( mashine ya kutolea nyuzi) ndogo. Ya umeme au ya diesel. Nimepita maeneo ya tanga nimeona katani zipo na zipo nyingine ambazo hata kuvunwa hazivunwi.
mzee nenda sido au kama upo dar nikuelekeze upate wapi mashine hio
 
Nipo dar mkuu.
Mkuu pale napafahamu sana. Hapa sido vingunguti? Nimuone nani?
 
Back
Top Bottom