Stories of Change - 2023 Competition

jayboy

Member
May 26, 2023
19
15
Tanzania ni moja ya nchi zenye kilimo kikubwa barani Afrika na inachukuwa kama nguzo moja wapo ya uchumi wa nchi.Takribani asilimia 75 ya Watanzania wanajishughulisha na kilimo kinachotegemea mvua.Mazao yanayo limwa nchini ni pamoja na mahindi,mpunga,maharage,nyanya,viazi,mboga mboga matunda na mazao ya kudumu Kama vile pamba,kahawa,tumbaku ,korosho na chai.

Kilimo cha kisasa ni mfumo wa kilimo inayozingatia matumizi ya teknolojia ya kisasa na mbinu za kisayansi kwa lengo la kuzalisha mazao mengi na bora kwa njia endelevu na rafiki kwa mazingira.Kilimo cha kisasa kinahusisha matumizi ya zana na mashine za kilimo zilizoboreshwa zaidi,pembejeo za kilimo za kisasa, mbinu bora za kuhifadhi maji na udongo na mbinu za kuzuia magonjwa na wadudu kwa kutumia demokrasia. Pia kilimo cha kisasa kinahusisha matumizi ya teknolojia za ufuatiliaji na utambuzi wa hali ya hewa na uchanganuzi wake.Teknolojia za ufuatiliaji na utambuzi wa hali ya hewa Kama vile mifumo ya hali ya hewa isiyo na way a inaweza kusaidia wakulima kutabiri mvua na hali ya hewa na kuchagua mazao yanayofaa kwa haliya hewa.

Aidha,kilimo cha kisasa kinazingatia utunzaji wa mazingira na matumizi ya njia za kilimo endelevu Kama vile kilimo cha kikaboni,kilimo cha maji ya mvua ,kilimo cha mseto na kilimo cha udongo usio wa vurugwa.Matokeo yanayotarajiwa ya kilimo cha kisasa ni uzalishaji wa mazao mengi na bora,kuongeza kipato kwa wakulima, kupunguza utegemezi wa mazao ya chakula kutoka nje na kukuza uchumi wa nchi.Kilimo cha kisasa pia kinachangia kuboresha afya na lishe ya wakazi wa vijijini kupitia uzalishaji wa mazao yenye virutubisho na kuchochea upatikanaji wa chakula kwa wote.

Kwa upande wa masoko,kilimo cha kisasa kinaweza kusaidia wakulima kufikia masoko ya kimataifa kwa kuzalisha mazao yenye ubora na kuongeza thamani kwa kutumia teknolojia za kisasa Kama katika ufugaji wa nyuki na usindikaji wa mazao na uhifadhi wa mazao.

Hii itasaidia kupanua uwigo wa masoko ya wakulima na kuongeza mapato yao.Kwa upande wa mazingira, kilimo cha kisasa kinaweza kusaidia kupunguza matumizi ya kemikali habari Kama vile dawa za kuulia wadudu (viatilifu) na mbolea za viwandani kutumia njia mbadala za kilimo Kama vile kilimo cha kibiashara na utumiaji wa mbolea za asili.Hali hii husaidia kuongeza uzalishaji wa mazao kwa kipindi kirefu na kupunguza uharibifu wa mazingira unaosababishwa na matumizi ya kemikali.

Hata hivyo kuna changamoto nyingi ambazo zinaikabili sekta ya kilimo nchini Tanzania Kama vile uhaba wa maeneo ya kilimo yenye rutuba kutokana na uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabia ya nchi, pia wakulima wengi hawana elimu ya kutosha kuhusu teknolojia za kilimo kwani zinazotumiwa za kizamani.Hii inapunguza uzalishaji na kukifanya Kilimo kuwa tegemezi kwa hali mbaya ya uchumi.

Kutokana na changamoto mbalimbali za kilimo cha kisasa serikali inatakakiwa kuchukua jitihada za makusudi katika kuboresha utawala bora na uwajibikaji katika sekta ya kilimo kupitia kuanzisha vituo vya utafiti wa kilimo kila mkoa badala ya kanda ili kuunganisha nguvu ya pamoja katika kufanya tafiti za uchunguzi wa udongo,mbegu chotara,mbolea na wadudu waharibifu wa mazao.

Matokeo ya tafiti hizi kuwawezesha wataalamu mbalimbali katika kutoa matokeo ya namna ya kulima kisasa na kuachana na kilimo cha kawaida ili kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa,pia serikali inatakiwa kuwahamasisha wakulima kutumia mitandao ya kijamii Kama vile twitter, facebook,YouTube na Instagram katika kutafuta masoko ya bidhaa za kilimo kimataifa hali hii itasaidia kuimarisha solo la ndani na nje kupitia ushindani wa kidigitali na nchi nyingine Kama vile China,India na Marekani.Pia kuwashawishi wakulima kuuza mazao kupitia Vyama vya ushirika ili kuongeza thamani ya mazao yao na kuondoa ulanguzi unaofanywa na wafanyabiashara wakubwa kupitia kununua njia siziso rasmi(Kangomba au choma choma).

Kwa kumalizia sekta ya kilimo ni muhimu Sana katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya nchi yoyote. Serikali inapaswa kuzingatia umuhimu wa kukuza sekta hii kwa lengo la kuboresha usalama wa chakula na kuongeza kipato cha mtu mmoja mmoja na Taifa.Kwa kufanya hivyo,nchi itakuwa na uwezo wa kujitosheleza kwa chakula na kupunguza utegemezi wa chakula kutoka nje na kuboresha maisha ya wananchi.
 
Sawa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom