Ushauri wako, nini kifanyike? Vijana wanapukutika

Ushauri wako, nini kifanyike? Vijana wanapukutika

Jamaa yangu,katoka mishemisheni kafika NDA ghafla kaanguka na kukata roho. R.I.P Ally .vijana tunakwisha
 
Ni topic pana sana kuijadili ila kwa kifupi niseme kuwa imefikia wakati sasa vijana wanatakiwa kujitambua na kuthamini maisha yao. Hii ni pamoja na
  • Kuepuka tabia hatarishi zinazoweza kukuingiza kwenya magonjwa yasiyo na tiba kama UKIMWI
  • Kujitunza kiafya ikiwemo kula vizuri, kuepuka vyakula hatarishi au vilivyoandaliwa kihatarishi vyenye mafuta mengi au viungo kupita kiasi, kufanya mazoezi nk vitasaidia kuepuka magonjwa kama kisukari, BP, Magonjwa ya moyo nk
  • Kuepuka na kujiepusha na ulevi kupindukia ambao kimsingi huchangia kuleta ajali na matatizo yasiyo ya lazima
  • Kufanya kazi kwa bidii na kuwa wabaunifu ili kuiongezea kipato na kupunguza mawazo na tabia hatarishi kama wizi ambao waweza kusababishi kifo
  • Vijana wanaoendesha vyombo vya moto (Magari, pikipiki nk) wawe makini kama marubani wa ndege na kufuata sheria za barabarani kupunguza vifo kwa njia ya ajali
  • Kupata muda wa kupumzika na kufurahi ili kuondoa stress
  • Kumuomba Mungu aendelee kutulinda na pia kujiapesha na kushawishiwa viabaya ili pia tusiingie kwenye balaa la vita vya kidini maana hivyo ndo vitawamaliza vijana wote kabisa ...
  • .....

Nawasilisha,

HP
Ahsante mkuu kwa ushauri mzuri.
 
Back
Top Bottom